D
Deleted member 485868
Guest
Aiseee..pole sanaStory ya mshkaji inanikumbusha mambo haya
1. Mwaka 2006 wakati naingia form 5 nilianza mahusiano na mdada mmoja mwenyeji wa ARUSHA. Mchanganyiko wa mchaga na Msomali yule dada nilijipa matumaini kwamba ni mtu wangu kumbe bana nilikuwa nasaidiwa bila kujua wakati nasoma
2.Mwaka 2008 wakati namaliza form 6 huyo mdada akaanza dharau matusi,kejeli sms hajibu akabadili na namba.Mwezi wa tatu 2008 akanipigia nikaenda Kimara-Stop over alikodai kwa mamdogo wake kumbe wifi bana.Nimefika nikapewa FANTA halafu mamdogo feki akaja kuniuliza
Mamdogo deki "eeh kaka wewe ni nani na una mahusiano gani na huyu mtu?
MIMI:Huyu ni mtu wangu
mamdogo feki:Una uhakika?
MIMI:NDIO
Mamdogo feki:Mimi unajua nina uhusiano nae gani?
MIMI:Mamdogo wake ndivyo alivyonitambulisha.
Mamdogo feki:Nyumbani kwao ashakupeleka?
MIMI:HAPANA
Mamdogo feki:Sasa sikiliza nikwambie,mimi ni wifi yake huyu mwanamke na kakangu ameshamtolea mahari huyu.sasa hivi yupo madrasa anafundisha akirudi itakuwa tabu.wewe ni mtu mzima naamiz una akili za kuamua kitu sahihi.
Baada ya kupewa "MAKAVU"sikuwa na jinsi ilibidi nijiondokee zangu nikamwambia yule dada namtakia kila la kheri na anakaribia kuwa mke wa mtu kwa hiyo tuachane kwa amani.
Sasa hivi tunavyoongea yule dada mimi mwaka 2010 aliposikia nimeajiriwa na kampuni moja hivi alihakikisha ananitafuta kwa udi na uvumba na kutaka kuonana na mimi lakin hadi leo sijataka mawasiliano nae na namba nimebadili.Aliahidiwa vits,atafunguliwa M-PESA sasa kaishia kuzalishwa na mwanaume kamkimbia.
FUNZO
Nilichojifunza toka 2008 hadi leo mimi binafsi simuamini mwanamke yoyote zaidi ya mamangu aliyenizaa. Kwenye suala la mahusiano siwezi kumuwekea guarantee mwanamke kabisa sababu ya madhila niliyopitia.Ukijifanya unamwamini mtu zama hizi kwa 100%atakachokufanyia hutokaa ukaamini.