Badala ya kuumizwa nao, wapishe….

Badala ya kuumizwa nao, wapishe….

Yaani mie si kuwa nam monopolise rafiki au akiwa rafiki yangu basi asiwe na wengine, ambacho kilinishinda mie ni ile group na in btw kunakuwaga na final muongeaji au kiongozi yaani wote mnamfata yeye asemacho, yaani ule ushoga wa ufuasi ulinishinda.
Akiwa rafiki yangu mie ni wangu akija na rafiki zake wengine nakuwa very selective kuwakubali au kuwakataa na nakuwa muwazi kumwambia kwenye mijumuiko yenu nendeni mie siendi, sijui unanielewa au nimeshindwa kujieleza.
Anyway kifupi mie shosti wangu ni mmoja from primary school level, mmoja secondary school level, na mwingine chuoni, huwezi amini kazini sina shoga huku ni kila aina ya vituko nina staff mate tuu wa kushare here and there na sio rafiki kiviiileeee. Ni hayo tuu.
nimekuelewa mamiii
 
kuna siku rafiki yangu saaana ambaye ni mkaka aliamua kujisemesha kwa watu kuwa anatembea na mimi. watu wakaja kuniambia. na kwa sababu tupo jirani sana na kwa vile yeye mwenyewe ndo kajitangazia watu hawakuweza kufikiria kuwa anasema uongo, waliamini.
unajua nilichofanya! sikutaka kubishana/kujitetea kwa wale watu waliokuja kuniambia, niliwaambia tu ukweli tunaujua mimi na yeye. na pia nilipokuwa na yule kaka nikamwambia kuwa nimesikia watu wanasema umewaambia hivi, sijui kwa nini umeamua kufanya hivi lakini mimi na wewe ndo tunaujua ukweli. hiyo habari iliishia hapo, sikuisikia tena kwa mtu mwingine yeyote.
unajua wakati mwingine tunatumia nguvu nyingi sana kujieleza na kutaka watu watuoen kuwa sisi ni wema sana, wakati hiyo nguvu wala haihitajiki. ishi maisha yako, kama mtu kakufika shingoni achana naye, songa mbele
kwenye red hapo umenigusa.....kuna rafiki yangu nahitajika nimfanyie maamuzi magumu......ingawa itaniumiza lakini heri iwe hvyo.....
 
kwenye red hapo umenigusa.....kuna rafiki yangu nahitajika nimfanyie maamuzi magumu......ingawa itaniumiza lakini heri iwe hvyo.....
ili usiumie saaanaaaa, kabla hujafanya maamuzi magumu ongea naye. hakikisha huna swali wala nung'uniko juu yake na aliyokuwa anakutendea..... msamehe then fanya maamuzi magumu. bila hivyo litakusumbua sana maana utabaki na maswali kibao usiyokuwa na majibu
 
always formula yangu kwa mtu aliyenikwaza ni kumsamehe, napenda sana kusamehe kuliko kitu chochote, nisiposamehe huwa naumia sana na nashindwa kuendelea na mambo yangu. hata kama sitataka kuendelea urafiki na mtu aliyenikwaza, kwanza namsamehe ili nipate amani ya moyo....
ukisha samehe kunakuwa hakuna haja tena ya kulalamika kwa watu. unaangalia tu huyo mtu kama bado unataka kuendelea naye au la. kama umeamua kuachana naye kunakuwa hakuna biff tena kati yenu
yani una maisha mazuri sana ukiishi kwa kusamehe......hata Mungu anakuinua maishani.......kuna wimbo mmoja wa bahati bukuku unaitwa lazima usamehe.......huu wimbo nausikiliza kila siku mana kuna vitu vya nyuma watu walinikosea nashindwa kuwasamehe.......
 
ili usiumie saaanaaaa, kabla hujafanya maamuzi magumu ongea naye. hakikisha huna swali wala nung'uniko juu yake na aliyokuwa anakutendea..... msamehe then fanya maamuzi magumu. bila hivyo litakusumbua sana maana utabaki na maswali kibao usiyokuwa na majibu
nashukuru kwa hilo.....mana nikimfanyia kimya kimya bila ya kuongea nae inaweza ikanigharimu zaidi mimi mwenyewe.
 
yani una maisha mazuri sana ukiishi kwa kusamehe......hata Mungu anakuinua maishani.......kuna wimbo mmoja wa bahati bukuku unaitwa lazima usamehe.......huu wimbo nausikiliza kila siku mana kuna vitu vya nyuma watu walinikosea nashindwa kuwasamehe.......
sister, mimi ni mtu ambaye na-value sana watu ninaokutana nao maishani mwangu.... kila mtu najua ana mchango wake katika maisha yangu.
sipendi kabisa kugombana na mtu, na ikitokea nikagombana naye huwa naumia sana. nisiposamehe basi hali yangu inabaki kuwa mbaya siku zote. ili nisonge mbele ni lazima nisamehe
 
nashukuru kwa hilo.....mana nikimfanyia kimya kimya bila ya kuongea nae inaweza ikanigharimu zaidi mimi mwenyewe.
umeona eeh! hiyo ndo point yangu....
unaweza ukajikuta wewe ndo unabaki na hali mbaya ingawa maamuzi magumu umeyafanya wewe.
kama unanisomaga niliwahi kuandika nilifanya maamuzi magumu kwa mpenzi, niliumwa mpaka kulazwa ingawa mimi ndo nilimuacha
 
.. Mtambuzi pia tukumbuke binadamu hatuko perfect! Lessons of life zipo hadi siku kifo kinapotutenganisha na dunia yetu!
Kuishi na watu kazi (Mama nipe radhi)
 
Last edited by a moderator:
umeona eeh! hiyo ndo point yangu....
unaweza ukajikuta wewe ndo unabaki na hali mbaya ingawa maamuzi magumu umeyafanya wewe.
kama unanisomaga niliwahi kuandika nilifanya maamuzi magumu kwa mpenzi, niliumwa mpaka kulazwa ingawa mimi ndo nilimuacha

dada yangu hio avatar yako plus michango yako MMU unanipa picha ya PERFECT WIFE SENT FROM HEAVEN.....
 
Back
Top Bottom