Badala ya kuumizwa nao, wapishe….

Badala ya kuumizwa nao, wapishe….

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
story-pic1.jpg

Kwa kawaida katika maisha ya kila siku ya binadamu, hakuna aliyekamilika kwa kila kitu. Kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Kutokana na kuufahamu ukweli huo, ni jambo muhimu kwetu kutambua kwamba, tuna wajibu wa kutoa mchango wa kutosha katika kuboresha uhusiano wetu na watu wengine bila kuyapa uzito mapungufu yao.

Kutokana na hali hiyo basi, ni vizuri tukazingatia na kujiwekea nafasi au umbali sahihi na wa kutosha, kutoka kwa watu ambao tunahisi na kuona kuwa hatuwapendi au ni maadui kwetu. Bila kusahau wajibu wetu wa kuchangamana, kushirikiana na kuambatana na wenzetu kwa heshima na utulivu.

Ukweli ni kwamba, iwapo hisia zetu mbaya kuelekea watu wengine ambao tunawachukia tutashindwa kuzidhibiti na kuziondoa, basi ni bora kwetu kujiondoa kutoka kwenye uhusiano na watu hao. Lakini tunapaswa tufanye hivyo kwa hekima, uelewa wa kutosha na tahadhari kubwa.

Tunapaswa tutambue kwamba, kama tungekuwa na ufahamu wa kutosha, kasoro na mapungufu hayo ya wenzetu yasingetuathiri kwa njia yoyote ile. Hata kama tunawaona watu hao kuwa ni maadui kwetu na wafujaji, ni lazima tuwakwepe huku tukiwa na utambuzi wa kutosha, na huku tukijitahidi kwa kila hali kutafuta kiwango cha juu cha uelewa na kusamehe ikiwenzekana.
 
Umesema sawa kabisa shem.
Binafsi huwa sijutii kufahamiana na mtu, nafahamu kila mtu ambaye Mungu amenijalia kufahamiana naye ana kitu fulani ambacho kitanifunza katika maisha yangu, kiwe kizuri au kibaya.
Ukweli siyo wote tunaojaliwa kufahamiana nao wanaweza kuwa na fikira tulizo nazo. Hata wale ambao mnakubaliana kwa mambo mengi kuna mambo machache ambayo mtahitilafiana...... hili ni kwa kila binadamu linatokea, huwezi kuwa na amtu ambaye mnakuwa mnaendana kwa kila kitu.
Tatizo ambalo wengi wetu tunalo ni kutaka wale tuliokutana nao wabadilike na kuwa kama sisi, kitu ambacho hakiwezekani. Kikawaida mtu binafsi unajiona upo sahihi kuliko wengine, na ungetamani watu waige toka kwako, tunajisahau kuwa na sisi ni binadamu na hatupo perfect.
Nakubaliana nawe shem, kama mtu unaona yule uliyenaye makwazo ni mengi kuliko maelewano basi ukajitenga naye ili upate amani ya moyo. kwa kuendelea kuwa na mtu ambaye wakati wote anakufanya ukwazike unakuwa hujitendei haki.
 
urafiki wa makundi siupendi mimi yaani mko group moja kisha ndani ya group wawili au watatu wanjitenge na kunena au kuteta mbali na wewe yaani mambo haya yalinishinda tangu niko primary rafiki mmoja tuu na akileta za kuleta nae namtimua sitaki unafiki mie. Yaani huyo mdada mwenye blouse nyeupe alivyo mzuri na anavotia huruma wenzake wanamtenga sijui anasubiri nn hapo? ushoga kazi sana mie ulinishinda kabisaaaa.
 
Umesema sawa kabisa shem.
Binafsi huwa sijutii kufahamiana na mtu, nafahamu kila mtu ambaye Mungu amenijalia kufahamiana naye ana kitu fulani ambacho kitanifunza katika maisha yangu, kiwe kizuri au kibaya.
Ukweli siyo wote tunaojaliwa kufahamiana nao wanaweza kuwa na fikira tulizo nazo. Hata wale ambao mnakubaliana kwa mambo mengi kuna mambo machache ambayo mtahitilafiana...... hili ni kwa kila binadamu linatokea, huwezi kuwa na amtu ambaye mnakuwa mnaendana kwa kila kitu.
Tatizo ambalo wengi wetu tunalo ni kutaka wale tuliokutana nao wabadilike na kuwa kama sisi, kitu ambacho hakiwezekani. Kikawaida mtu binafsi unajiona upo sahihi kuliko wengine, na ungetamani watu waige toka kwako, tunajisahau kuwa na sisi ni binadamu na hatupo perfect.
Nakubaliana nawe shem, kama mtu unaona yule uliyenaye makwazo ni mengi kuliko maelewano basi ukajitenga naye ili upate amani ya moyo. kwa kuendelea kuwa na mtu ambaye wakati wote anakufanya ukwazike unakuwa hujitendei haki.

Sasa nauona uhalisa wako!
 
Nimefurahi kuona kwamba umeelewa point yangu....
Ahsante sana Fixed Point
 
Last edited by a moderator:
Nimefurahi kuona kwamba umeelewa point yangu....
Ahsante sana Fixed Point
ha haaa, umesahau mimi ni kimbilio la wengi?
yaani nikikufungulia moyo wangu unaweza kunihurumia, sometimes najiuliza kwa nini inakuwa hivi? sipati jibu.
utakuta unaona watu mtaani/ofisini kuwa ni marafiki saaanaaaa, yaani wapo pamoja kwenye karibia kila unapowaona. lakini kila mtu kwa wakati wake, karibia kila siku, anakuja kukulalamikia kuhusu mwenzie, unashangaa kwa nini inakuwa hivi? kwani huyo ni mzazi/sibling/mwanao? hao pekee naamini siwezi kutengana nao, wengine woote can go to hell.
kama naona huyu mtu naweza kuongea naye na tukaelewana haina shida, akinikwaza naongea naye tunaelewana. lakini kama kila siku lazima anikwaze kwa nini nisimpishe tu? unaweza jikuta unazeeka moyo kabla ya mwili..... sijui moyo nao unazeekaga? maana wengine sayansi ilitutupa mkono
 
Nimependa sana pale uliposema kuwa kule kukerwa na mapungufu ya wenzio ni ishara ya wewe kuwa na mapungufu
'
Huu ni ukweli mkubwa sana,hatujui kuwa wote tumepungua kama tumepungua wote hatuna budi kuvumiliana
'
Kama tumeshindwa basi tuachane kwa amani kwenye ndoa,urafiki n.k sio ugomvi
'
Tupendane kiukweli!
 
urafiki wa makundi siupendi mimi yaani mko group moja kisha ndani ya group wawili au watatu wanjitenge na kunena au kuteta mbali na wewe yaani mambo haya yalinishinda tangu niko primary rafiki mmoja tuu na akileta za kuleta nae namtimua sitaki unafiki mie. Yaani huyo mdada mwenye blouse nyeupe alivyo mzuri na anavotia huruma wenzake wanamtenga sijui anasubiri nn hapo? ushoga kazi sana mie ulinishinda kabisaaaa

Katika maisha kutofautiana kupo sana si majumbani, makazini na hata huko mitaani, kamwe hatuwezi kuridhika na jinsi mambo yaliyotuzunguka yanavyokwenda. Muhimu kwetu ni kujua namna ya kuishi kwa tahadhari ili kuepuka kukanyagwa au wenzetu kutugeuza mabusati ya mlangoni.

@Sakapal mara nyingi kwenye maisha yetu huwa inatokea tukaangushwa na pengine kugalagazwa kwenye vumbi la fedheha na dhalilisho kwa uamuzi ambao huwa tunauchukua na mazingira ambayo huja au kutujia kwenye njia zetu kimaisha. Katika nyakati kama hizi hutokea tukajihisi kuwa hatuna thamani. Lakini tusichokijua ni kwamba, hata kama kingetutokea kitu gani, hatuwezi kamwe kupoteza thamani zetu.

Thamani yetu iko ndani mwetu. Tukiamua kwamba thamani yetu iko nje yetu, ni wazi tukikejeliwa au kuvurugwa kwenye dhalilisho na dharau, tutajikuta tukijidharau na kudharauliwa kikweli na hata wale waliokuwa wakituheshimu.

Tukitukanwa, tukasingiziwa, tukaharibiwa jina, tukaaibishwa na kufanyiwa ubaya, bado thamani yetu itaendelea kuwepo. Kama tutalijua hilo, basi hakuna dhalilisho au kashfa ambayo itaweza kutufanya tuone kwamba tumevunjiwa heshima au kudhalilishwa. Hii ni kwa kuwa thamani yetu haiwezi kuguswa na mtu kwani iko ndani mwetu.

ujumbe muzuri sana asante kwa kusema nami leo na kuniweka sehemu ambayo sikutarajia kuwekwa Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Nimependa sana pale uliposema kuwa kule kukerwa na mapungufu ya wenzio ni ishara ya wewe kuwa na mapungufu
'
Huu ni ukweli mkubwa sana,hatujui kuwa wote tumepungua kama tumepungua wote hatuna budi kuvumiliana
'
Kama tumeshindwa basi tuachane kwa amani kwenye ndoa,urafiki n.k sio ugomvi
'
Tupendane kiukweli!
mimi naamini kuna level na sababu ya mapungufu naweza kuyavumilia, zaidi ya hapo ni kujiumiza.....
ha haaa, nimekumbuka kitu...... kuna mtu alikuja kunilalamikia kuhusu mwenzie lakini baada ya kuendelea na maongezi yetu mwisho wa habari akajiona yeye ndo ana makosa, lol! nilitumia hiyo hiyo stori aliyoniletea kumwonyesha kuwa yeye hayupo perfect..... alienda kuomba msamaha na maisha yakaendelea.
hili watu wengi tunalo, tunaona katika kila kukwazwa wenzetu ndo wana makosa, kumbe ukiangalia sana wewe mwenyewe ndo unakuwa umelisababisha hilo.... kwa vile wanasema mwamba ngoma ngozi huvutia kwake basi tunapenda kutwisha mzigo wooooteeee wa lawama kwa wenzetu
 
Back
Top Bottom