Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,553
- 52,288
BADALA YA KUBARIKI WATOTO NA KIZAZI CHAKO UNABARIKI ISRAEL USIYOIJUA WALA ISIYOKUJUA; ACHENI UCHIZI.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli
Yesu kama Watibeli wengine alishawahi kuwatolea maneno mbaya mbovu Wafuasi wake akiwaambia;
Lk 23:28
Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.
Kitabu cha biblia hasa vitabu alivyoandika Musa vimeandikwa kwa namna Mbili. Mosi, vimeandikwa kwa maelekezo ya Mungu mwenyewe, lakini pili, vimeandikwa kisiasa na Musa mwenyewe ambaye ndiye Legend namba moja wa Uyahudi.
Jua kuwa Musa alikuwa Msomi wa kiyahudi aliyekulia katika jumba la kifalme la Farao. Hivyo elimu za wakati huo za kisiasa alikuwa nazo mbali na elimu ya dini kutoka kwa Mama yake.
Maneno ya kuwa ukiibariki Israel unabarikiwa na ukiilani Israel unalaaniwa yameasisiwa na yeye mwenyewe Musa ikiwa kama Propaganda za kisiasa katika kutetea maslahi ya Waisrael kwa wakati huo. Zingatia kwa zama walizokuwa kina Musa ilikuwa Zama za Vita ya miungu. Na kila jamii ilikuwa inapambana kugombea maeneo nyeti ya huu ulimwengu.
Hivyo katika namna ya kukabiliana na maadui zao hasa wale maadui waoga walitumia zaidi propaganda za Imani kuwadhibiti adui zao. Moja ya maneno na misemo waliyoitumia ilikuwa huo msemo wa "kuibariki Israel ni kutafuta baraka, na kuilaani ni kujitafutia Laana"
Kauli hiyo kwa mara ya kwanza aliiandika Musa Kwa mhusika Ibrahim akipewa maneno hayo na Yahweh.
Propaganda hizo za kidini hazikuishia kutumika katika zama hizo za vita ya miungu. Bali zimetumika mpaka kipindi cha juzi cha Ukoloni ambapo Ukristo ulitumika kusambaza propaganda za kulainisha nyoyo za Waafrika ili wakoloniwe( watawaliwe).
Sio hivyo tuu, hata hivi leo tumeona viongozi wengi wa dini wakitumia maneno na misemo ya kiiimani kama propaganda ya kutawala na kuwaburuza Watu vile wanavyotaka. Mfano, msemo wa kutomnyooshea Mtumishi wa Mungu kidole au kutomkosoa ni msemo wa propaganda wa kijinga mno ambao hutumika kudhibiti Watu walioamua kutotumia akili zao.
Yaani ni wanadamu fulani waliojitia cheo au hadhi fulani ambao wanatumia kisingizio cha imani kuwatumia wanadamu wenzao vibaya.
Israel ni moja ya mataifa yaliyoburuzwa na kupigwa sana katika Historia ya dunia. Kama yalivyo mataifa mengine, Israel imeshatawaliwa mara kibao na kupelekwa utumwani mara kibao.
Israel ni Watu kama Watu wengine ndio maana wanapitia mambo yote wanadamu wengine wanayopitia.
Kuiombea Israel badala ya kuombea nchi yako na familia yako ni uleule ujinga wa kumchangia mchungaji gari wakati wewe huna hata baiskeli. Au kumjengea nyumba mchungaji wakati waumini mnaishi maisha ya kindezi. Ni upumbavu tuu.
Propaganda ni upepo ambao hubeba Watu wenye upeo mdogo na kuwaburuza vile watakavyo.
Leo sina mengi ya kusema. Acha nipumzike tuu.
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam