Badala kulipa deni yeye kaenda polisi, naombeni ushauri nimfanye nini?

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,184
3,517
Amani iwe nanyi.

Mnamo tarehe 30 July 2020 nilimkopesha L.S. pesa kiasi cha 1.5M kwa riba ya 25% kwa mwezi mmoja hadi tarehe 30 Agosti 2020.

Wakati wa kupeana pesa tuliandikishana mbele ya balozi na ndugu yake mmoja kama shahidi wake. Dhamana ya mkopo wake ilikuwa hati ya serikali ya mtaa ya nyumba yake ambayo haijakamilika iliyopo Tegeta Skanska.

Sharti lililokuwepo kwenye mkataba ni kwamba akishindwa kulipa ndani ya muda kutakuwa na penalty ya 25% kwa kila mwezi utakao ongezeka hivyo hadi kufika 30 December 2020 inakuwa miezi mitano hivyo kufanya penalty kuwa 75% hivyo ukijumlisha na ile riba inakuja kuwa 100%.

Wakati wa kuandikishana sikushikilia dhamana kwa kuwa anayeishi pale ni ndugu yake hivyo nikaondoka na hati na mkataba.

Mpaka naandika hapa Jamaa hajalipa hata senti tano na nilipoanza kumbana alinizungusha sana yaani mnoo na baadae nilipomwambia naenda kumtoa ndugu yake kwenye nyumba (nakumbuka ilikuwa 02 December 2020) jamaa aliongea na polisi ambao ni rafiki zake wanitumie barua ya kuitwa kituo za polisi Kunduchi Mtongani.

Wakati hayo yote yanatokea nilikuwa nimepata udhuru wa kikazi hivyo nilisafiri kwenda Simiyu kikazi. Hivyo nikawaambia ndugu zangu wasitishe kwenda kumtoa ndugu yake kwenye nyumba badala yake wakachukue ile barua.

Sasa sikwenda polisi na nilipokuwa Simiyu balozi alinipigia simu kuna barua yangu nyingine, nikamwambia aniambie niende kureport kituo chochote cha polisi mkoani Simiyu kusema hivyo mpaka sasa hivi kimyaa nami bado sijarudi Dar es Salaam.

Ninavyojua mimi polisi hawaruhusiwi kuingilia kesi za madai(sasa sijui jamaa alimwambia nini polisi hadi kutuma barua ya kuniita kituoni).

DAWA YA DENI NI KULIPA VYOVYOTE ITAKAVYOKUWA.

Ndugu zangu jamaa nilimsaidia akiwa ana shida mnoo tena sanaaa leo hii amefanya nijute sana kumsaidia. Swala la kwenda polisi kuzuia nisishikilie dhamana amenipa hasira zaidi.

KABLA SIJAFANYA MAAMUZI YANGU YA HASIRA NIMEONA NIJE KWENU MNISHAURI KWA LOLOTE HASA KISHERIA ZAIDI.

AHSANTE SANA.
 
Mkuu kwanza hukumsaidia, ulifanya biashara kwa kumkopesha kwa riba. Pili msaidie mjadiliane hiyo Riba na penalty, kuzalisha faida ya asilimia 100 ndani ya miezi 4 kutoka kwa mtu mwenye matatizo si afya na kuweka dhamana isiyofanana kwa namna yeyote na deni. Aidha matatizo yalimsukuma au hakuelewa makubaliano. Mwisho ni haki yako kupewa chako.
 
Sheria za kibeberu zinaanza kuyeyusha uhalisia na utamu wa Maisha ya Kiafrika. Yaaani uje kwangu Kijana wako kafaulu kwenda Chuo Kikuu hajapata Boom unataka nikukopeshe Milioni 1 utatue suala la mwanao kujiunga chuo, NAKUPA PESA KIROHO SAFI.

Halafu nijje kukudai ulete Sheria za BOT???? Happo ndio mtajua kwanini wengine wanatahiri bila ganzi na wengine wanatahiri Hospital maaana Polisi sitakwenda na Pesa utaitoa tuuu!
 
Acha kumtisha, nyie ndo wadaiwa sugu

Tabia njema ni kulipa mlichokubaliana
Siyo kumtisha ndiyo ukweli halisi. Mimi kuna mke wa bro wangu alihama hadi mkoa wa Dar kwa muda kisa alikuwa anafanya biashara ya kukopesha wafanyabiashara wadogo wakina mama, akaja mpatia pesa maza flani milion kadhaa maza, akaweka nyumba na hela kashindwa irudisha. Mke wa bro akataka kuichukua maza akaenda mfungulia kesi, ilikuwa ni balaa alikimbia mpaka mkoa, hadi kesi kuisha alihonga na pesa hakuwahi kulipwa.

Hizi biashara za kukopesha watu mtu akitaka fanya awe na vibali vyote, lah sivyo unakula hasara na mdeni anapita mtaani akiringa.
 
Mkuu kwanza hukumsaidia, ulifanya biashara kwa kumkopesha kwa riba. Pili msaidie mjadiliane hiyo Riba na penalty, kuzalisha faida ya asilimia 100 ndani ya miezi 4 kutoka kwa mtu mwenye matatizo si afya na kuweka dhamana isiyofanana kwa namna yeyote na deni. Aidha matatizo yalimsukuma au hakuelewa makubaliano. Mwisho ni haki yako kupewa chako.
Mkuu nilishamsamehe penalty yote 75% mpaka sasa na hili wala sitobadilisha.
 
Pole Sana. Kwanza kabisa hujaonyesha popote barua imeandikwa nini Kwa sababu hujaipokea. Pili. Tii wito wa Polisi bila shuruti yawezakana si la mdeni wako. Kwa kuwa alikuwa na shida na ukaamua kuibeba shida yake kama yako kwa uungwana alipaswa alipe kama si hivyo jua nini kimemsibu mpaka akashindwa kukuletea pesa. Usifunge mlango kama atakuja kwenye meza ya mazungumzo. Lakini kama atashindwa kukupa pesa nenda kamtoe Kwa kutumia yuleyule balozi aliyesimamia awali.
 
Back
Top Bottom