Back from Honeymoon

asante sana rafiki kwa hii clip pia, naipenda saaanaaa, itabidi nijifunze kucheza hivyo, huwezi kujua next honeymoon, lol!
kwa kweli BAK mapenzi ni matamu mno, na nimeshikwa barabara, kwa hiyo na mimi bila hiana nimeamua kushikamana haswaaaaaaaaaaaa, na ukweli nina furaha mno.
huyu teja sidhani kama atakubali hiyo mizizi ya rafiki, maana hataki kabisa kusikia kuna kuponyeshwa huo ugonjwa, eti anasema yupo comfortable zaidi na kuumwa kuliko akipona, lol! chezeya uteja wa mapenzi weye.
Na mimi nakuombea rafiki, kama bado hujapata wa kupendana naye basi umpate kama huyu wangu ili muelee pamoja kwenye hilo dimbwi zito la mahaba.....usikubali kuwa peke yako, lol!
Nashukuru rafiki, nawe nakutakia weekend njema
 
Last edited by a moderator:
ha haaaaaaaaa, binamu nani anataka talaka? inabidi kumsikiliza mwenzio anasemaje....... kwa vile ameshaniomba nibaki hivi, nitajitahidi kwa ajili yake
eheehheheeh asikukazanie wewe tu na yeye ajitahidi asije kuwa na kimimba cha kudumu(Kitambi) manake tubia na tushwain vinatutoa vitambi na hivi hatuna muda wa mazoezi basi ni umbo la biringanya kwa kwenda mbele
 
eheehheheeh asikukazanie wewe tu na yeye ajitahidi asije kuwa na kimimba cha kudumu(Kitambi) manake tubia na tushwain vinatutoa vitambi na hivi hatuna muda wa mazoezi basi ni umbo la biringanya kwa kwenda mbele
ha haaaaaaaaa, umenichekesha na hilo umbo la biringanya, lol! noted
 
Hahahahaha lol! Unataka kujua kucheza eeh! kucheza mchezo gani rafiki? :behindsofa: hahahahah lol! Kama unataka kujua kudance BAK ana shule yake ya kufundisha kucheza ila anacharge $ kwa saa. Mapenzi matamu sana rafiki FP acha tu...sasa wasioyafahamu wanayafanya kuwa kama mafungu ya nyanya kule sokoni. Nilishasoma kule MMU baadhi ya "Wataalam wa Mapenzi" wakidai huyu nampenda 30% na yule 30% na nanihii 40% halafu wakishaharibikiwa hawakawii kuja kuomba ushauri kwa kupigwa chini. Sasa ukishaweka mapenzi sawa na mafungu ya nyanya kweli utaijua ladha ya kweli ya mapenzi? Ukisikia mtu aliyependwa na kupenda kama rafiki yangu FP hukawii kusema kishalishwa limbwata yule!!! au kisha nyunyiziwa vya kunyunyuziwa!! haiwezekani ukampenda mpenzi kiasi hicho!!!! Kisha pia nikawasoma eti mpenzi usiwe naye karibu sana. Siku nyingine akitaka kuwa nawe ili mkajirushe sehemu sehemu basi unampotezea tu eti anapokuwa hayuko mara nyingi nawe ndio anakumiss sana na mapenzi yanazidi kupamba moto!!!!!:target:

Mie nina hamu ya mupenzi twende sehemu tukajirushe kwa raha zetu halafu ananiambia eti "Rafiki zangu akina nanihii wanakuja hapa leo tutajipikilisha pikilisha biriyani na chapati kisha tutaangalia movie." nasepa zangu kimya kimya na donge langu. Siku nyingine tena unamfuata mupenzi kwa kufuata ushauri aliusoma MMU anakupotezea tena eti ndio mapenzi yanapamba moto!!! "Mie leo sijisikii kutoka." atanisikia kwenye redio mbao.

Sasa akiona kimya anaanza kukutafuta yeye, "We BAK mbona umekuwa kimya sana?" "kitu gani nilichokuudhi" BAK kimya tu. "BAK nakuja kukupikia chapati na vitumbua weekend hii tutapata breakfast pamoja." anajua huyu kwamba BAK ni mpenzi sana wa vitumbua na chapati. BAK anamjibu kisha nunua mkate wake wa Boflo akishaupaka mawese basi unatosha kabisa kwa chai ya asubuhi. Ushauri mwingine kule MMU badala ya kujenga unabomoa kabisa rafiki....ogopa sana baadhi ya ushauri kule MMU.

Teja mfuatilie kwa karibu ukiona dalili zinazidi kuwa mbaya kama za kuongea akiwa pekee yake, kucheka kwa sauti kubwa akiwa pekee yake, au kulialia basi hapo hakuna mahojiano tena inabidi akokotwe haraka sana ili akatibiwe vinginevyo anaweza kupata uchizi hivi hivi.

Nataka nimuige yule jamaa aliyetemwa miaka 13 iliyopita ila bado anasubiri hadi kesho lol! Mwambie aangali asije kufa kibudu (kufa kibudu ni kufa kwa mtu mzima ambaye alikuwa anasubiri mke wa mtu aachike ili yeye amuoe, muhusika huwa hajawahi kuoa maishani mwake) ila mie nitasubiri kwa Mwaka tu nikiona hakuna dalili basi nasepa zangu lol!

:fencing:
Furahia kupendwa na kupenda rafiki wengine raha hizo hawajawahi kuzipata maishani mwao.



 
Last edited by a moderator:
welkam bak FP mzima wewe??? we missed u dearly, lazma honey moon itakuwa imezaa matunda! lol, nilikuwa jela kwa ushirikiano wa viranja wa hili jamvi, but at last nipo mtaani kama kawa, tutajuzana zaidi, karibu tena!

...afu wewe mtoto cacico nimekumisije... Mzima bibie?
 
Last edited by a moderator:
ha haaaaaa, rafiki yangu BAK ndo maana nilikumiss sana ulipokuwa huko unashangilia ushindi wa BO, usiwe unapotea bwana, maushauri kama haya ndo huwa tunayahitaji hapa mara kwa mara. nimekupendaje sasa, lol! Asante sana.
Ngoja nimwite mlongo wangu snowhite aje apate haya mautamu hapa. maana najua tupo wote kwenye haya mambo ya uteja, hakuna kupenda nusu nusu hapa, lol!
Rafiki nitafurahi sana kujiunga kwenye hicho chuo chako..... huyu teja atalipa kiwango chochote utakachotaka..... hilo halitakuwa na shida kabisa, cha muhimu mwanafunzi afaulu.... na nakuhakikishia mimi ni mwanafunzi mzuri sana, sitachukua muda mrefu kama una wakufunzi wazuri..... nipo serious ujue BAK
Huyu teja, Eish, sijui hata nimfanyaje...... naendelea kumpeleka taratibu ili siende kwenye uchizi, sitaki afike huko kabisa.
huyo jamaa wa kufa kibudu simlaumu rafiki, hata wewe ukipenda hivyo unaweza kusubiri maisha yako yote, lol!
asante sana rafiki kwa clip, naomba nisiongee zaidi kuhusu hili, jua tu nimeipenda sana.
Barikiwa sana rafiki yangu kwa michango yako....
 
Last edited by a moderator:
ahahahhahahhahha dada mkubwa huwa anajua vizuri uteja wa mdogo wake !lol sijui tumelogwa!kha!
 
shikamoo BAK! sikamoo tena!
lol!hata sijui nisemeje!ila ngoja tu niendelee kukuamkia!yani ujue nimepiga na lile goti la kingoni kabisa hapa! watu8 nafikir u need to read this my dear!mi staki haya maujuzi ya BAK yakupite Ciello please come zis way mamduchu Boflo hii inakuhusu pia incase hujaisoma !
 
Last edited by a moderator:
Asante mlongo wangu kwa kunisaidia kumwamkia huyu rafiki, sasa sijui na mimi ana-deserve shikamoo yangu? naogopa kuamkia mabwana wadogo, lol! BAK njoo uthibitishe hapa kama unastahili shikamoo toka kwa dada mkubwa
 
Last edited by a moderator:
Asante mlongo wangu kwa kunisaidia kumwamkia huyu rafiki, sasa sijui na mimi ana-deserve shikamoo yangu? naogopa kuamkia mabwana wadogo, lol! BAK njoo uthibitishe hapa kama unastahili shikamoo toka kwa dada mkubwa

hii ya BAK ni ya kukubali alichopost!sasa kwa minajili hiyo we mpe tu japo najua lazima we ni dada mkubwa pia kwake!
 
Last edited by a moderator:
hii ya BAK ni ya kukubali alichopost!sasa kwa minajili hiyo we mpe tu japo najua lazima we ni dada mkubwa pia kwake!
sawa mlongo wangu, angalau umetoa ufafanuzi kwa hiyo akija kuona namwamkia ajue kabisa ni ya post siyo yake. ni kweli huyu rafiki huwa ananifurahishaga sana na msimamo wake wa kupenda 100% na kukubali kuwa teja. inatia moyo kujua bado kuna vijana wanapenda hivi.........lol! (ndo awe mzee mzima, atanitoaje mbio! ha haaaa, mlongo wangu usicheze mbali, akija kunitoa mbio unisaidie, sawa?)
Shikamoo rafiki yangu BAK
 
Last edited by a moderator:
ahahhahhahhhahhahah mie tena si ndio bodigadi wako!wala usijali!ila BAK hana tatizo dada mkubwa ,ako poa sana ila tu siku hizi kabanwa na nini sijui au ndo uteja wenyewe!manake tatizo uteja huu huwa hauna rehab bana!lol
 
Last edited by a moderator:
ahahhahhahhhahhahah mie tena si ndio bodigadi wako!wala usijali!ila BAK hana tatizo dada mkubwa ,ako poa sana ila tu siku hizi kabanwa na nini sijui au ndo uteja wenyewe!manake tatizo uteja huu huwa hauna rehab bana!lol
ha haaaaaaaaa, hapa sisemi neno mlongo wangu, na wala sikuulizi kwa nini unamwamini BAK kiasi hicho, lol! dada mkubwa nakaa kimya tuuuuuuu.
ila mara ya mwisho nakumbuka alisema yuko busy na kampeni then kusherekea ushindi wa BO. sasa inawezekana kaamua kuunganisha kwenye uteja, hiyo ni kawaida kabisa hasa kama kapata teja mwenzake, lol! rehab hata zingekuwepo unafikiri mateja wa hivi wanataka hata kuzisikia? wanaona ni bora waendelee kuugua tu
 
Last edited by a moderator:
LoL! Haya rafiki nitajitahid nisipotee sana. Sasa mbona mdogo wako snowhiteameninong'oneza kwamba dada yake kwa kudance ndiye mwenyewe? Au ulikuwa unanisanifu rafiki yangu Mpekele Teja kwenye matibabu rafiki kabla hajachizika maana akishafikia hali hiyo basi matibabu huwa yanachukua muda mrefu sana na kunaweza kusiwe na mafanikio ya kuridhisha baada ya matibabu

[video]http://www.youtube.com/watch?NR=1&feature=endscreen&v =7KhxmAD74Ck[/video]


 
Shosti uteja huu hata mie nakuombea kwa mola kamwe usiishe. Next week naenda kusherehekea miaka 50 ya ndoa ya wazee wangu, nawaangalia nawatamania yaani. Bibi ukimuambia kitu anajibu ngoja niongee kwanza na babu nitakujibu. Usismsikilize BAK. Muambie aongezee dozi hata ukienda rehab kwa bahati mbaya usipone mwayego.
umeona eeh rafiki..... hakuna anayetaka uteja uishe....
na kwa vile tupo kwenye same boat basi tumekubaliana tuendelee tu kuugua, no rehab
 
Last edited by a moderator:
Marahaba mdogo wake FP lol! dada yako kashikwa akashikamana. Yumo ndani ya mahaba mazito kupita kiasi. anasema maraharaha ni kupita kiasi. Anaamka na tabasamu la nguvu siku nzima anashinda na tabasamu lake la nguvu na kupanda kitandani na hilo tabasamu lake. Amebahatika sana kupenda na kupendwa kiasi hicho. Chezeya mweziasali mara mbili kwa mwaka weye!!!


 
Last edited by a moderator:
ha haaaaaaaa, rafiki "don't get it twisted love is a beautiful thing", lol!
asante sana kwa huu wimbo, kuna verse nyingi sana zinanifurahisha.....
teja bwana, anavizia hadi mazoezini! kaazi kweli kweli
huyo mlongo wangu <b><a href="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=96061" target="_blank">snowhite</a></b> ameshaanza kutoa siri zetu? kakuambia pia huwa ni mwimbaji mzuri?
 
Hehehe rafiki FP mie sitaki shikamoo banaaaa nisije kuzeeka siku zangu lol!

:fencing::fencing::fencing::fencing:



Ntaachaje kujua mdogo wangu wakati tumetokea shina moja? acha kabisa.
na tunavyojua kuchizika tukipata tunapopaamini, full kuachia mwili na moyo, lol!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…