Bachelor ya Gesi na Mafuta (Petroleum engineering)

Bachelor ya Gesi na Mafuta (Petroleum engineering)

manem

Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
88
Reaction score
55
Msaada tafadhar wadau, nina rafiki yangu kamaliza six mwaka huu PCM ana CCD anapenda kusomea (Mafuta na Gesi) ananiomba ushauri kuhusu hiyo kozi na changamoto za ajira mtaan. Mim ni mwalimu wa Msingi sina nachojua hapo hivyo nimeshindwa kumshauri nisaidieni ushauri wadau nisije nikampoteza.
 
Nafikiri kama yeye mwanachuo mtarajiwa kapenda hiyo course na anahisi itaimuda, aombe tu vyuo vinavyotoa hii program asome. Changamoto zipo kwa kila course chuoni na baada ya chuo, ila isimkatishe tamaa kutimiza malengo yake.
 
Nimejaribu kufuatilia mwaka mmoja nyuma nigundua ni vyuo vitatu vya udsm, udom na dit ndiyo wanatoa hiyo koz ila mdau umesema wa udsm walipelekwa dit inamaan udsm hawatadahili kwa hiyo koz mwaka huu
 
Mkuu kwanini usiombe telecom/ electronics/mechanical eng? Mafuta na gesi ajira unazungumzia miaka kumi toka sasa, haina ajira kwa sasa, na cha ajabu watanzania wengi wameikimbilia nawaonea huruma sana. Njoo nipm aisee
 
Hapo fanyaa application mapema kijana uje tupige kitabu afu abt kazi ni ujanja wako ackudanganye m2
 
sasa kama nchi haikujipanga kwa nin wanaanzisha koz kwa kas na wanaiweka kwenye kipaumbele kuwapa mkopo ili hali haina uhitaj? hata siielew hii tanzania yangu
 
mdau ejk upo katika hiyo tasnia au unaufahamu wa wale waliowah kuisoma hiyo koz wakamaliza walipo sasa? nisaidien wadau nimshaur huyu dogo kilichobora
 
ejk hakuna jambo jema kama nchi kuwa au kuandaa wataalamu, ina maana ikitaka kuwatumia inakuwa easy, tukirud kwenye reality, kila graduate anataka matunda mapema, ndio maana nashauri ukweli huo hapo juu.
 
Aisee kwa CCD hawezi kuchukuliwa petroleum, mwambie achague lakin sio chaguo la kwanza kama anaweza asome mineral processing ni nzuri ukifaulu vizuri ajira zipo
 
Ni course nzuri sana in terms of payment. Wataalamu kwenye hii fani wanaongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa sehemu yeyote duniani. Ila tatizo kwasasa ulimwengu unabadilika, kutoka kwenye matumizi ya mafuta/gesi kwenda kwenye renewable energy. Ingekuwa ni kumshauri ningemshauri asome renewable energy kwasababu ndipo ulimwengu unapoelekea kwa sasa. Futuatilia mataifa yote ya ulaya na makubwa duniani wameanza kuinvest kwenye hii sector. So mda so mrefu hiyo course itakuwa ni habari tofauti na watabahatika wale waliosoma mapema. Ila nway mwisho wa siku itabaki kuwa ni mapenzi ya mtu ila ndio situation ambayo ulimwengu unaenda kuelekea sahivi. Good lucky. Unaweza uka google pia
 
Back
Top Bottom