Bachelor mimi nimedakwa na mke wa mtu

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
885
Wakuu za majukumu.

Awali ya yote niseme tu kuwa nilishaapa kutotongoza mke wa mtu cozi najua mke wa mtu sumu.

Basi ni kama mwezi umepita, kuna siku mwanamke mmoja ameolewa, nimemzoea kama shemeji. Nilikutana nae meneo ya baa, alikuwa amejibust kidogo, aliponiona alinifuata na kunikumbatia huku akichezesha kiuno. Masikini mcroun Mimi, masai alisimama nikabaki nafikiria namna ya kujinasua pale. Ilikuwa kigiza ndo kinaingia lakini niliogopa mno licha ya midadi kunipanda.

Nilichomoka na baadae tukio hilo sikuliwaza sana maana mhusika alikuwa amelewa.

Siku zilipita. Siku moja nikakitana na huyu mke wa mtu akiwa hajalewa. Nilimkumbusha tukio hilo alilonifanyia akiwa amelewa na nikamweleza sikupenda. Yeye alicheka na yakaisha.

Baadae kama siku tatu kupita, nikiwa kwenye majukumu yangu jioni moja, mara niliona simu ikiita namba ngeni. Kupokea sauti ya mwanamke. Alijitambulisha sikumfahamu mara moja mpaka baada ya maelezo marefu.

Nilimhoji namba yangu aliipata wapi, hakunambia, ila tu alichosisitiza ni kuwa kwa nini naringa. Nilimweleza hofu yangu kuhusu kutembea na wake za watu, hakunielewa. Alisisitiza kuwa sisi siyo watoto kuja kujulikana.

Ukweli ni kuwa sikuwahi kumpigia simu ila yeye ilikuwa hadi kelo. Kama binadam, nilianguka kwenye dhambi ya zinaa mara moja lakini nikamweleza kuwa siko tayari kukosana na mmewe, hivyo iwe mwisho.

Nilipoona haelewi nikamblock. Alipogundua kuna siku jioni alikuwa amelewa alinitafuta Sana maana hakuwa ananipata kwenye simu. Hakuwa na aibu hata chembe sababu ya pombe. Alinisaka vijiwe vyote ambavyo aliamini angenikuta.

Nilionana nae ila hapo ndo nilijilaumu kwanini nilitembea nae. Yeye alisisitiza kuwa tuendelee na mahisiano ila nilimkatalia. Nilimtoa block ila tulikubaliana apunguze kunipigia cm.

Hiyo ilikuwa juzi. Leo jioni kanipigia nikapokea, akaanza kulalamika kwanini akinipigia naongea kwa kujivuta. Simu ilikatika ghafla, nami sikuifatilia maana ni kama naiona kelo.

Saa mbili usiku nikiwa natoka misele naenda kwangu, ile nafika getini nakutana na mme wa huyu mwanamke. Alikuwa amepaniki akiwa na simu mbili mkononi. Sure I understood what was going on. Mwanaume alikuwa amefura hasira.

Off course alikuwa mstaarabu kiasi. Aliongea kwa utulivu Sana. Hakunipa nafasi ya kujitetea. Alinielekeza tu mwanzo mpaka alivyoondoka. It was a shit! Nilichemka ghafla, mdomo ulijaa maji na hata nilipojiandaa kukataa mashitaka hayo tayari alikuwa ameondoka.

Alinambia kuwa anafahamu kuwa nina mahisiano na mke wake toka siku nyingi. Akasema anajua nimetembea nae mara nyingi tu. Na akahitimisha kwa kusema kuwa ananiachia mke. Hapohapo akaondoka. Aliniacha nimeganda Kama nimechomwa sindano za barafu. Hapa npo nimechanganyikiwa. Naanzaje kulitatua.
 
Unajua tulioa tunahangaika sana, tunarisk na kusacrifice Mambo mengi sana ili kutunza familia then anatokea mtu anakugongea mkeo kwa kisingizio mkeo kajilengesha! Aisee ibaki hivi hivi tu sijui kinachoendelea upande wa pili ila siku nikijua sijui itakuaje! Tungekua tunakaa mtaa mmoja ningekufanya kitu hamna Aisee!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom