mi babu yangu ni mzee sana maana alizaliwa kipindi kile ule uwanja wa man u unaitwa Old traphod enzi hizo ulikuwa unaitwa NEW TRAPHOD
Du Samito, mbona unatulisha matango pori aisee!???
Lakana na Isembo.....
Babu yangu alikuwa anaitwa Tondoloveta(nadhani ni tusi la kijerumani).tafuta Yeye alikuwa anatuhimiza kutafuta mademu
Siku nyingine tumetoka kumchukua dukani kwake (alikuwa mshonaji mzuri sana wa nguo)..na amelewa si kichezo,
sasa tukawa tunashuka kilima cha kuelekea nyumbani (kichumi). Akatuambia, "wajukuu zangue, nyie tangulieni mbele, ili mkiteleza nije nikiwaokota"lol
Kumbe huku nyuma yeye ndo alikuwa akiteleza na kuanguka kila saa. Yani trick yake ni ili tusimuone anavyoanguka...
Mzee Nyella huyo!
Babu yangu alikuwa na vitu sana, mtaani walikuwa wanamwita pilipili jinsi alivyokuwa mkali, katika vitu alivyokuwa anachukia ni akukute unaonea....awe mtu ...mnyama au mdudu, siku moja siafu wakaingia jikoni kwake, akaja akatukuta tunazichoma akatuletea noma kinoma yaani na kusema acheni wadudu wa Mungu, kuna siafu alipandia akamng'ata nyuma ya goti.... aliruka na bakora ikarushwa pembeni.....alipomtoa alisema "lazima nikushome...."akamtupia kwenye moto....na akaturuhusu kuchoma wote....
Siku nyingine tukawa tunaua panya buku, tukaziba njia zake zote za kutokea shimoni na kubakiza shimo moja tulilolitumia kuingiza maji ya mfereji.... kadri tulivyokuwa tunajaza maji na panya buku kuonyesha dalili zote za kutoka ndivyo babu yangu alivyokuwa anatutaka kuwa wajasiri...kila mtu alisimama kwenye shimo lake... panya buku akatoka speed shimo alilokuwa kasimama babu...Babu alishtuka badala ya kumpiga akabaki akisema huyu hapa huyu hapa huku anasogea pembeni....
RIP babu Asprin ila nna hakika utakuwa umemsingzia..,lol.Babu yangu Meku Serya...
Siku mvua inanyesha sie tunaota moto huku tukichoma maindi, akaachia ushuzi kwa bahati mbaya....nilisikia nikauchuna naye akauchuna. Ushuzi ulipotoa harufu mbaya, kaka yangu akala makwenzi na kupigwa mkwala "wanaume huwa hawajambi hovyo"........Kaka akitaka kujitetea babu akamkatiza "Nyamaza, malabuku" Akala kwenzi jingine.
dah! Ushuzi aachie babu, kwenzi atiwe bradha.............nlitoka nje nikacheka sana.....ningechekea pale nami ningekula kwenzi.......!
RIP my dear Babu.... I miss you vibaya sana!