Babu wa Loliondo sasa yuko hatarini...

Wanaompigia kelele babu ni wezi kwa kutumia Biblia, janja yao kutokea nigeria na india, wanaombea matatizo miaka nenda rudi, sadaka mamiliöni. Lakini hakuna kitu. Babu ukimuona mara moja hutamuona tena. Wameambiwa usihukumu, wao wamepata wapi uwezo wa kuhukumu? PUMBA TUPU.
 
Nenda kwanza shule ya uandishi wa habari ndio utaweza kuchambua post zangu na vichwa vyake.

Wewe kwenye post hii umeandika Ndiyo Siyo Ndiyo Siyo - ongea pointi !

Kumbe ukiguswa kwenye ukweli unajua kukasirika. Hakuna mahali nimeandika ndiyo siyo. Kwa taarifa yako nimesomea uandishi wa kitaalamu. Hii ni pamoja na layout. Sina haja ya kuthibitisha hilo kwani mtu akisoma na kuangalia post yangu atathibitisha hayo. Na kama huoni pointi kwenye post yangu; basi unawathibitishia watu wote watakaosoma thread hii nani kati yetu hana point.

Umeshikilia ubatizo wa maji mengi, maji mengi! Kwa taarifa yako nimebatizwa kwa maji mengi. Ubatizo wa maji mengi siyo hoja ya msingi kwa suala la babu na huduma yake.
 
Unasubiri Revelation ndio ujue kuwa shetani yupo. Pole sana


Bado hapa umepoteza zaidi.....I think you are now beyond heaven

Kumbe kujua shetani yupo huhitaji revelation?

Basi kazi ipo maana naona pengo kubwa kati ya wahubiri injili wa aina yako na injili yenyewe
 
Bado hapa umepoteza zaidi.....I think you are now beyond heaven

Kumbe kujua shetani yupo huhitaji revelation?

Basi kazi ipo maana naona pengo kubwa kati ya wahubiri injili wa aina yako na injili yenyewe

What is revelation? It's a disclosing, discovering or making known of what was before secret, private or unknown.

The Bible has already disclosed Satan. Unataka revelation kutoka wapi tena?
 

Kwanini tuandikie mate na wino upo? Subiri baada ya siku chache zijazo utajua mkweli na mwongo ni nani.
 

Ukinywa au ukiwa na imani na kikombe cha babu huwezi kuona siri wala hatari. Giza la shetani linakufunika.
 
Kwanini tuandikie mate na wino upo? Subiri baada ya siku chache zijazo utajua mkweli na mwongo ni nani.

Nashukuru umeanza kuona hoja. Hatuna haja ya kuhukumu na kuwa wakali kama unavyofanya. Time will tell. There are so many things we do not know.

Ukinywa au ukiwa na imani na kikombe cha babu huwezi kuona siri wala hatari. Giza la shetani linakufunika.

Kwa taarifa yako sijaenda kwa babu. Hata hivyo siwabezi walioenda huko. I hava a very strong biblical background.
 
Hata Kakobe asilalamike, aliwahi kusema huwezi kuhoji nguvu za Kimungu. Kwa hiyo kama babu anatibu kwa nguvu za Kimungu hakuna kuhoji, au mapato yamepungua kanisani kwenu ndo maana mnamuonea gere babu aliyebarikiwa kweli na Mungu?
 
Unabii hupimwa na neno la Mungu kama yardstick/kioo. Hivyo kama unabii unapingana na neno la Mungu, unabii huo huwa wa uongo. Biblia inasema MTAWEKA MIKONO JUU YA WAGONJWA, NAO WATAPATA AFYA, sasa hii staili mpya ya kikombe imetoka wapi? Ama kwa kuwa kina Askofu Laizer wamekwenda, na kina Sumaye na Lowasa ndio iwe sababu ya kuamini ndoto zake? Kila jambo litawekwa wazi, punde mtagundua kuwa babu alipata ndoto ya kishetani...
 
Ukinywa au ukiwa na imani na kikombe cha babu huwezi kuona siri wala hatari. Giza la shetani linakufunika.

Nimekufuatilia sana kwa kuwa naamini una mafundisho ambayo siyo sahihi. Narudia kusema sijaenda kwa babu na hata hivyo siwabezi walioenda kwa sababu sina biblical basis ya kufanya hivyo.

Maandiko yote uliyokuwa unayachomoa kutoka kwa Yeremia yana historia yake kwa wakati ule. Ni vema ukaacha kupeleka maana kwenye maandiko. Acha andiko lijisemee lenyewe. Manabii wa wakati ule walizungumza na watu wale kwa wakati ule kwa mazingira na tatizo la wakati huo. Tunaposoma ni vizuri tukajua Mungu alikuwa anasema nao nini wakati ule huko. Na baada ya hapo, ndipo tuseme na sisi tunajifunza nini (au andiko hilo lina maana gani kwetu sisi sasa).

Sasa hivi tuko na hoja ya babu na tiba yake. Je maandiko yanakataza tiba ya miti shamba?

Nimesoma post zako na kuona umemtumia sana Yeremia. Naomba ufahamu Yeremia anataja habari ya dawa ya miti shamba (healing balm) walau mara tatu katika kitabu chake (Soma Yer 8:22; 46:11; 51:8). Gilead ilijulikana kwa kuwa na miti mingi ya tiba. Tunawaambiaje watu hao? Kuwa wayahudi wote hawakumjua Mungu? Tunasemaje pale Mungu anapowatuma wamisri waende Gilead kupata dawa?
Mwanzo 43:11 inasema: Hapo Israeli, baba yao, akawaambia, "Haya kwa kuwa ni lazima iwe hivyo basi, fanyeni hivi: chukueni katika mifuko yenu baadhi ya mazao bora ya nchi yetu, mkampelekee zawadi huyo mkuu. Mchukulieni mafuta kidogo ya mkwaju [healing balm], asali kidogo, ubani, manemane, kungu na lozi. Yakobo anawaambia watoto wake wampelekee Yusufu dawa ya miti shamba. Je, tumsemeje Yakobo hapa? Unahitaji kusoma maandiko zaidi.

Kwa taarifa yako vyakula vyote vya aina ya mbegu (matunda na mazao mengine) ni miti shamba. Kwa vile umeyazoea mahindi hayafanyi kuwa siyo mti shamba.
 
Kwa aliyeanzisha hii thread mimi nasema hivi......believe what you want to believe and let other people decide for themselves. Kila mtu atapima imani yake towards huyu Babu na ataamua kulingana na utashi wake! Going on and on about sijui mstari wa Bible unasema x, y and z isnt going to help much. If you think he is fake, ur point of view is noted and personally i respect ur views...but at the end of the day i will trust and believe what i want! Do i hear an AMEN?
 

Wagonjwa wote makanisani na kwenye mikutano ya injili huwa wanawekewa mikono? Je, staili ya kuombea handkerchief imetoka wapi? Vipi staili ya kupiga power watu imetoka wapi?
 
Nawachia wadau ama kwa upande nilko mimi kwanza manabii wameshakwisha,pili dawa za mitishamba si miujiza bali ni dawa za kawaida na suwala la ndoto ni ndoto tu Mungu hana haja ya kumjia mtu hivi sasa kwani alishakamilisha maamrisho yake na hata hapo alipokuwa akileta basi alitumia malaika.
 
kama babu ni nabii wa uongo na anafuatwa na watu wengi namna hii wenye kuhitaji uponyaji wa magonjwa ya miili yao, basi ujue kwamba taifa hili halina nabii wa kweli hata mmoja kwa sasa. Kama wangilikuwepo na kupewa uwezo wa kuwaponya watu maradhi yao kwa neno la Yesu, hawa wanaomwendea babu wangetoka wapi?
Kwa habari ya babu kutoza 500, sijui kama hilo ni tatizo. Litakuwa tatizo ikiwa atajitokeza mtumishi mmoja tuu katika taifa letu mwenye kanisa na kwa uaminifu akanushe kwamba gherama za maisha yake hazina hata senti moja ya pesa zilizotoka kwa wafuasi wa kanisa.
Hapo babu atakuwa na hatia kumsemea mungu ambaye wale wanaompinga hawanae.
.
 

Kumbe hivi ndivyo mnavyoelezwa huko kanisani kwenu. 'Ole wenu maana ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa mbinguni''
 


  • Manabii wa uwongo ni hawa wanaoanzisha makanisa yao katika hii karne ya 21. Babu hajaanzisha kanisa
  • Ninachoweza kuwashauri wamiliki wa makanisa ya maombezi/kiroho ni kuweka mkakati wa kuwavutia watu wasio na shida waje makanisani. Muache kupita mahospitalini na kuwarubuni wagonjwa, hamuwatendei haki. Wafateni watu wenye afya zao wajiunge na makanisa yenu, hapo hamtapata mtikisiko hata akitokea nani. Hii ndio sababu ya uimara au ukubwa wa makanisa kama ya KKKT, RC, Anglikana, Sabato nk.
 

Kuna better life in christ kuliko huko kuponywa na dawa ya Babu na kesho unaugua mafua, malaria, typhoid etc kweli ikiingia ndani yako basi ugonjwa ukigusa mwili wako wenyewe una surrender na kupiga magoti nimekoma sinta rudi tena. Kwanini ukapange foleni na wengine kufa kabla ya kupata kikombe cha Babu huku unaweza tu ukajiwekea mwenyewe maji free kutoka kwa Yesu just from the atmosphere? Its possible to live such kind of life thats the whole mission of why Christ came and died for us.

Pata shule hapa;

|| Pastor Chris Online - Channel ||


|| Pastor Chris Online - Channel ||

Do you want to live in the night of your life of day of your life?

I choosed to live in the day of my life and am preaching so that others may discover themselves and come out of their dark life to the greater life where they would enjoy life in sunshine.
 
Mada hii ni nzuri. Wewe ni jasiri najua hutaumia wala kukata tamaa kwa matusi yanayofuata. Umesema kweli unayoiamini bila kuogopa kwa sababu unajua unachokifanya.

Ninachoona mimi, watu hawana sababu ya kutetea kwamba Loliondo kuna Mungu. Hilo jambo ni gumu kulisema kwa kuimba kama kibwagizo kama kweli mtu unamaanisha. Ninaomba wapenzi wa babu wasitoe matusi. Mbona yeye hatukani? Ninachokijua mimi wengi wanakwenda kule kutafuta uponyaji wa mwili na wala siyo kumtafuta Mungu. Na hata babu mwenyewe sijasikia anahusisha dawa zake na msamaha wa dhambi wala utakatifu. Hivyo watu wanaenda kunywa dawa sawa kama wangeambiwa imegunduliwa katika kitengo cha tiba za asili muhimbili, au ni ya nchi fulani, ama dawa za wachina. Bahati mbaya sana tukienda huko tulikokuzoea kutibiwa hatuulizagi hayo madawa asili zake nini. Mimi binafsi sitaki kuoanisha madawa na uwepo wa Mungu.

ILA KWA HABARI YA IMANI, NAWAAMBIA BINADAMU WAACHE DHAMBI NA WALA WASIMTUMAINIE BABU WA LOLIONDO WALA MTU YEYOTE MAANA NI WANADAMU WAKUPITA NA WOTE WAKO CHINI YA SHERIA YA MUNGU.

HAIJALISHI WANAUMWA AMA NI WAZIMA. WAMETIBIWA LOLIONDO, HOSPITALINI AMA KWA WAGANGA WAKIENYEJI WANAPASWA KUMUISHIA MUNGU. KUFA KUPO TU NA NI MARA MOJA. BAADA YA KIFO NI HUKUMU. SASA HAITASAIDIA KAMA MTU UNAKUFA KATIKA DHAMBI KWA SABABU YA MAISHA HAYA MAFUPI HALAFU UNAPOTEZA UMILELE WAKO. NAOMBA WATU WOTE WAMPOKEE BWANA YESU KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAO MAANA YEYE NDIYE NJIA KWELI NA UZIMA. NA MTU HAFIKI KWA MUNGU ILA KWA NJIA YA YESU KRISTO PEKE YAKE.
NAWASILISHA.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…