Babu Wa Loliondo Janga La Kitaifa 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu Wa Loliondo Janga La Kitaifa 2011

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Dec 31, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  "Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote",ni wimbo unaovutia ni wimbo unaelezea wasifu wetu wasifu wa nchi yetu Tanzania kweli jina lako ni tamu tulalapo tunakuota wewe, Ndoto wakati mwingine uashiria kitu kijacho !

  Naam ndugu zangu Watanzania,
  tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka nchi yetu imekumbwa na majanga kadhaa likiwepo hili la mafuriko napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote waliofikwa na mafuriko najua Mungu atasimama upande wao, janga hili ni muendelezo wa majanga mengi yaliyoikuta Tanzania yetu tunayoiota tutalalapo,,Ambikile Mwaisapile maarufu kama babu wa loliondo ni moja ya majanga hayo .

  Inayodaiwa kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeonyesha madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu ilikuwa ni mradi, na kwa kweli kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa.

  Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi mabaya, na ni sugu. Ndio, miongoni mwetu kuna wenye kusumbuliwa na maradhi ya unafiki. Nitatoa mfano nilipata kukaa na wasomi wawili, tena wana digrii zao. Tukazungumzia ya Babu wa Loliondo.

  Mimi na wasomi wale tulikuwa na misimamo ya kufanana, tulipinga upotoshaji unaoendelea katika jamii kuwa Babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapile , anatibu ukimwi, kansa, kisukari na mengineyo. Na kwa vile wote tumekwenda shule, hoja kuu ilikuwa hii; kuwa hadi sasa hakuna hata wagonjwa watatu wa ukimwi waliothibitishwa kitaalamu kuwa wamepona ukimwi kwa dawa ya Babu. Badala yake, kuna wengi wamekufa baada ya kuacha kutumia madawa waliyoelekezwa na madaktari watalaamu waliosomea tiba.

  Wakati tukiendelea kuzungumza, mara akatokea mheshimiwa fulani, naye akaingia moja kwa moja kwenye mjadala. Alimtetea Babu na kusisitiza kuwa Babu ni lulu ya taifa, lazima aenziwe. Wasomi wale afadhali wangekaa kimya, hapana, walianza kumuunga mkono mheshimiwa kwa hoja nyepesi.

  Hawakuwa wapumbavu, walijifanya tu wapumbavu wakiniacha mimi nikipambana peke yangu kuziponda hoja za mheshimiwa yule. Kwa kiasi fulani, niliogopa kuona hulka hii ya wasomi wetu. Wasomi ambao, kwa unafiki, wanashindwa kutetea na kusimamia katika hoja zao za msingi. Na hii, bila shaka, ni moja ya majibu ya swali la kwa nini Tanzania ni masikini?


  Hakika, ya Babu wa Loliondo ni aibu yetu kitaifa. Katika karne hii ya 21 nchi yetu inatumia raslimali zake kufanya promosheni ya ndoto ya Mtanzania mmoja kati ya Watanzania milioni 42! Ndio, tunafanya promosheni ya jambo lisilo na uthibitisho wa kisayansi. Si tuliona, haikupita siku bila kusikia habari za Babu wa Loliondo?

  Kwa sasa, tunaweza kabisa kusema, kuwa habari za huduma za Babu wa Loliondo zilitangazwa na kuufikia umma kuliko habari za Wizara yeyote ile katika Serikali ya Awamu ya Nne. Babu wa Loliondo si mchezo bwana, alikuwa na ‘maafisa habari wake' wanaowafunika hata maafisa habari wa Wizara za Serikali.

  Na katika mzaha huu wa mambo ya msingi kitaifa, tuna maelfu kwa maelfu ya Watanzania wanaotaabika na hata baadhi kufa kwa kuamini kuwa Loliondo kuna tiba, na iko Loliondo tu! , kuna Watanzania walioweka rehani mavuno yao ya mwaka mzima ili wapate nauli ya kwenda kwa Babu. Si wameambiwa, kuwa hata mawaziri wanapanga foleni ya kwenda kupata kikombe cha Babu!

  Na wakishapata kikombe wanapiga picha ya ukumbusho, au labda ya kisiasa. Asubuhi yake 'maafisa habari' wa Babu wameshatundika picha ya waziri ukurasa wa kwanza gazetini! Jimboni kwa mheshimiwa wapiga kura wake watamwona au kusikia kuwa Mheshimiwa naye anaumwa kama sisi, na amepata kikombe cha Babu!

  Kikombe cha Babu ni abrakadabra, nilipata kuandika hilo. Na Watanzania, baadhi, kwa hiyari yetu, tumekubali kujifanya, wajinga na hivyo kuwapumbaza wengi wengine. Kwanini? Tulitafute jibu kwa kufikiri kwa bidii.

  Hebu jiulize; wakati Shirika la Afya Duniani (WHO), Juni mwaka huu, liliadhimisha miaka 30 ya mapambano dhidi ya ukimwi, je, Tanzania, kama nchi, tulikuwa na banda la maonyesho likielezea ugunduzi wa tiba ya ukimwi iliyotokana na ndoto ya Babu?!

  Labda ndio maana, magazeti yetu ya lugha ya Kiingereza hayakufanya sana promosheni ya tiba ya Babu. Maana, kama habari za Babu zingepewa uzito kama ilivyo kwenye magazeti yetu ya lugha ya Kiswahili, basi, wana jumuiya ya Kimataifa, wakiwamo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, huenda wangeshindwa kuamini wanachokisoma.

  Maana, wawakilishi wa mashirika kama PSI na FHI yenye miradi ya kupambana na ukimwi nchini na mengineyo wangejiuliza; nini hasa wanachokifanya katika nchi yetu. Na pengine wameshatafsiriwa tunachooandika juu ya Babu kwa Kiswahili chetu!

  Si ajabu basi, Ubalozi wa Marekani ulikuja na tamko lake Mei 5 mwaka huu. Wamarekani hawa, kwa kuwaonea huruma Watanzania, wameshauri watu wanaotumia tiba mbadala wasiache kutumia dawa walizopewa na madakatri na vile vile waendelee kujikinga na maambukizi.

  Na wakaweka msisitizo kuwa, kuacha kutumia dawa hizo za madaktari watalaamu kunafanya dawa hizo zinapotumiwa tena kushindwa kufanya kazi ipasavyo (drug resistance). Na ajabu ya habari ya tamko lile la Wamarekani ilichapishwa katika gazeti moja tu kwa lugha ya Kiingereza - The Citizen, jina la gazeti hilo lina maana ya Mwananchi; ingawa wananchi wengi hawakupata habari hiyo kwa lugha yao!

  Kwa hakika, hatuhitaji kuambiwa na Wamarekani juu ya ukweli huu na wajibu wetu. Huu ni wakati kwa wizara inayohusika kufanya jitihada za dhati kutoa tamko litakaloweka bayana kuwa tiba inayodaiwa kutolewa na Babu bado haijathibitika kitalaamu kama inaponya maradhi sugu kama vile ukimwi, kansa na kisukari.

  Wakati utafiti huo ukiendelea, umma ukumbushwe kuwa, dawa zinazotambulika kitalaamu kwa sasa ni zile zinazotolewa na madaktari wetu watalaamu. Kwamba wanaokwenda kwa Babu wana ruhusa ya kufanya hivyo, lakini, kikombe cha Babu kinaweza kunywewa pamoja na dawa za hospitalini.

  Tufanye hivyo sasa, na ujumbe huo usambazwe kwa nguvu zote na maafisa wa habari wa wizara husika. Ndio, maofisa habari wa Wizara ya Afya nao washindane na ‘maafisa habari' wa kujitolea wa Babu wa Loliondo!

  Watanzania tunapita kwenye kipindi kigumu sana. Na huu ni wakati wa kutafakari kwa kina. Na nimepata kumwuliza jamaa yangu swali hili; mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Naye akanijibu; " Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!" Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani angetamka kuwa, angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

  Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri?

  Haya ya kwa ‘Babu wa Loliondo' ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, unahitaji mwanga.

  Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu wakaoteshwa na Mungu juu ya dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndio, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa kiserikali.

  Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo; maana, watakuwa wameufanyia utafiti. Nahitimisha.


  Niwatakieni Heri ya Mwaka Mpya.
  Maggid Mjengwa.
   
 2. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Maggid mbona hutaki kumlaumu ' mungu' wa babu? Tulionya hapa kuwa mungu wa DECI amerudi tena kwa njia ya matibabu ya Loliondo, wenye mungu wao hawakuacha kumtetea!
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mpk na leo nasikia kuna watu wanaendaga kupata kikombe!

  Na juzi nasikitika kusikia toka kwa mteja wake aliyetoka huko wiki iliyopita akisema Babu kaoteshwa na MUNGU ya kwamba mafuriko ya watu ya atakuja zaidi ya awali.

  Hakika nimesikitika sana!
   
 4. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,428
  Likes Received: 12,694
  Trophy Points: 280
  hawa wakina jey key pamoja na wizara
  ya afya ndo walimpromote


  so wao ndo janga la kitaifa
   
 5. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mh! Mi naenda vyangu atii! Baadae saana ntarudi! Nawahi bar!
   
 6. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,650
  Likes Received: 3,299
  Trophy Points: 280
  Umenifanya nivute pumzi nyingi kuliko kawaida. Ndugu Mh Maggid huna haja ya kujitambulisha ili niweze kujua kuwa wewe u msomi, kati ya wale waliopata elimu bora kabisa, mh. Ila baada ya kumaliza kusoma post yako hii nimehisi kama jicho lile nililo kuwa nikikutazamia limeanza kuingia ukungu, nadhani hii ni dalili dhahiri ya upofu! Sita weza kulaumu kwani jicho hili la ndani kama lilivyo la nje nalo lina independent movement,ni dhahiri kuwa unaelewa maana halisi ya majanga na ni dhahiri kuwa majanga mengi yaliyoikumba nchi yetu ndiyo yale.tu uliyoyaona,je unafikiri si zaidi ya hapo? Je unafikiri hayo yaliyotufika ni yale yaliyoweza tu kuzuilika?je umejaribu ku categorize majanga hayo ili angalau uweze kuainisha kati ya yale tunayoweza kuyazuia na yale yaliyo nje ya uwezo wetu?na kama ndivyo mloliondo huyu alikuwa kwenye kundi gani?sidhani kama kweli kabisa ulipaswa kuja na hasira ulizokuja nazo kwa issue tambarare kama hii! Maggid unanilazimisha kufikiri muda ninaopoteza kwenye nyumba za ibada mimi na familia yangu vilevile nifikirie athari ninayo weza kuwa nimeipata tangu niigizwe/niingie kwenye mambo hayo ya kiimani,nifikiri kuhusu vita zinazopiganwa kwa sababu ya imani,jinsi serikali za dunia zikigongana vichwa kwa jambo hili japo nyingi zinasema hazina dini ila zinaapisha pia, ndiyo imani hii hii kama yako kama yangu,ambayo imepandwa kwenye msingi wa kuamini tu,baada ya hapo endelea kuamini huku ukisubiria kwenda mahali panapoitwa Mbinguni!huku ukisubiria kupoNYWA magonjwa yote yanayo kusibu ndiyo imani hii inayotupeleka mecca na nazareth kwa kutumia fedha ambazo ni sehemu ya uchumi wa nchi usinilazimishe kuamini kuwa falsafa ya Babu wa loliondo ni ngumu ya kukufanya un`gate meno,hujaishiwa maarifa Maggid no, staki kuamini hivyo hata siku moja ,siamini kuwa hili ndiyo janga kubwa uliloliona mkuu kiasi cha kulipa attention ya kiasi hicho. Sina haja ya kujiuliza kwa nini malaria inaendelea kumaliza watu huku viwanda vya ALU,Fansidar na vinginevyo vikiendelea kufanya kazi. Tena usiku na mchana hakika ntajitia kichaa kama hicho unachoki tafuta kwa kwenye mlango wa kanisa kusubiri walio ndani wakupe ushuhuda ili nawe uamue kuingia ama hapana, huu udini Maggid huu Udini huu!
   
 7. M

  Makupa JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mimi nitalaumu maaskofu hasa wa KKKT na bila kusahau baadhi ya Viongozi waandamizi wa serikali kwa kushabikia miti shamba kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia
   
 8. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  lakini nafikiri hii dawa ni ya kiimani zaidi. Imani ya mtu ndiyo imponyayo. Mimi kuna ndugu yangu alikuwa na bp na sukari amepona kabisa.
   
 9. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  ..Janga kubwa zaidi ni viongozi wetu ktk kila ngazi, walikuwa na nafasi nzuri sana ya kubadilisha maisha ya wananchi, lakini wao wakaamua kubadilisha maisha yao kwa kuongeza posho maradufu ili wawe waheshimiwa na sie tubakie wadharauliwa. Aaah! Where is TZ's Kagame when we need him the most?
   
 10. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,650
  Likes Received: 3,299
  Trophy Points: 280
  Dawa ni dawa inamponya yule anayepona na haimponyi yule asiyepona pia ni sumu kwa yule atakayekufa.
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280

  Swadakta!
  Viongozi wa serikali ndo janga zaidi, kwa sababu wengi wao (mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, watendaji n.k.) walijazana kwa Babu kupata tiba ya kikombe badala ya kuboresha huduma za afya katika vituo vya afya na zahanati zetu zenye wahudumu wachache na dawa haba. Kumlaumu Babu wa Loliondo ni kukosa busara na kukwepa tatizo sugu linalokabili sekta ya afya. Wingi wa watu kukimbilia Loliondo mwaka jana kunamaanisha kwamba kuna shida kubwa katika huduma na sekta ya afya katika nchi yetu, suala ambalo inatakiwa tulishikie bango ili litatutuliwe. Babu si janga, janga ni wale wanaompa nafasi ya kujitangaza na kumtangaza kama mtoa mada hii na viongozi wa serikali wanaokwendsa kupata kikombe
   
 12. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Babu wa loliondo aliwaambia watu kuwa kupona kwao itatokana na imani yake na kuna watu waliamini hivyo wakapona.Sioni sababu ya kusema kwamba ni janga la kitaifa,kwa nini MFUMUKO wa BEI isiwe janga la kitaifa?

  Hakuna mtu alielazimishwa kwenda kwa Babu,na hata wagonjwa wanaokwenda mahosptitalini wako wanaopona na wanaofariki na wala hatusemi hosptitali zimekuwa janga la kitaifa.Labda tatizo ni jinsi serikali na vyombo vya habari zilivyotangaza.

  Hivyo mi binafsi sioni sababu ya kumlaumu Babu.
   
 13. kasingo

  kasingo Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mmmmh!wa tz tumechoka kabisa tunaamini vitu vya kufikirika muda si mrefu tutaitwa nchi ya kufikirika
   
 14. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  cha ajabu babu ambae mpaka muda huu alitakiwa awe mahabusu kusubiri hukumu kwa kosa lake la wizi wa kuaminiwa bado anapeta.lazima apete ktk nchi ya chukua chako mapema,siri kali ilishindwa kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa taratibu ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti ikawa ndio chambo.leo wanaona aibu hawajui hata pa kuanzia wako kimya.imani haiko hivyo imani inaendana na vitu halisi.lazima tuwe makini na watu wanaofanya utapeli wa aina mbalimbali kwa jina la mungu.tuamke wadanganyika hatuna kiranja tena,baba mwizi mama tapeli watoto wadokozi nani atamkemea nani?
   
 15. V

  VAMPA Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we mkali
   
 16. S

  Snitch Senior Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani hapa tujitahidi kuwa makini kwa Tanzania ya sasa yenye dalili za Udini na tumekua Wapofu and tend to keep a blind eyes on the Reality...cha msingi hapa ni kua katika dunia hii ya Utandawazi hivi hii ya Samunge iwe dawa kweli Wazungu na wawakilishi wa WHO na wengine wasilione hili.... Sasa hapa kuna vitu viwili
  Moja
  Ni kua wale linawagusa kiimani kwa maana ya kufanywa na viongozi wa kiroho wanaowaamini ni wajibu wao kutetea tu hata Kama hakuna uthibitisho wa kitaalamu ingawaje walishatoa tamko .

  Pili
  Ni kwa wale waliojitambulisha kwa jina la Magid wengine kudhani tathmini hii ni muendelezo wa kuponda dini Au kiongozi wa dini nyingine na kuamsha hisia ambazo hazija hoja Bali ni kutetea sasa hii ni hatari sana ktk taifa.

  Sasa hapa hebu tuangalie logic is it scientifically proven... Je tulishawahi kuenda nje kwa Imani?

  Tukumbuke wale MASALIA waliosambaratika kwa kipindupindu.....

  Tuone LOGIC jamani
   
Loading...