Babu wa Loliondo apata mawasiliano! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa Loliondo apata mawasiliano!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ngongo, Apr 9, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu wanajamvi.

  Jana nilipata ujumbe wa sms from AIRTEL kwamba wamezindua huduma yao kijiji Samunge Loliondo kwa Mchungaji Babu.Ndugu jamaa na marafiki sasa mtaweza kuwasiliana na jamaa zenu wanaokwenda kwa Babu kupata kikombe.

  Hongera AIRTEL mko juu sana>Hongera Babu kama si wewe wanakijiji wa Samunge wangeisubiri huduma kwa karne nyingine mbili.

  Babu ohoyeeeee.
   
 2. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Yap! Hongera kwa wanasamunge kupitia babu, hongera Airtel!
   
 3. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Bw Elias Wawa Lali (katikati), Diwani wa Kata ya Samunge, Bw Jackson Sandea (kulia), Meneja Biashara wa Airtel mkoa wa Arusha, Paschal Bikomagu

  [​IMG]

  Mchungaji Mstaafu Mwaisapile akipokea zawadi ya simu ya Mkononi kutoka airtel. anayemkabidhi ni meneja wa biashara wa Airtel Mkoa wa Arusha, Paschal Bikomagu. Kulia DC, Ngorongoro

  airtel yazidi kusheheneza mawasiliano vijijini – Samunge sasa yapata mawasiliano
  • Yazindua mnara wa mawasiliano kwa ajili ya maeneo ya Samunge, Mgongo, Mageri, Yasimdito na Digodigo huko Loliondo
  • Yawa kampuni ya kwanza na pekee kuwezesha mawasiliano maeneo hayo
  April 07, 2011

  Ikiwa ni muendelezo wa kutimiza ahadi yake ya kuleta mawasiliano nafuu na yenye kuwafikia watanzania wengi zaidi, hasa walioko maeneo ya vijijini hapa nchini, kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel, leo imetangaza kuzidi kupanua mtandao wake kwa kuzindiua huduma ya mawasiliano katika eneo la Samunge na maeneo jirani, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

  Kwa mujibu wa Airtel Tanzania, kuzinduliwa kwa mtandao imara na wenye nguvu umegharimu zaidi ya dola za kimarekani laki moja na nusu hadi ulipomalizika. Uwekezaji huu utawezesha kuleta mawasiliano thabiti kwa watu wa vijiji vya Samunge, Mgongo, Mageri, Yasimdito and Digodigo.

  Akitoa maoni yake juu ya uzinduzi huu wa huduma ya mawasiliano, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sam Elangalloor amesema kwamba Airtel imejidhatiti vilivyo katika kutoa huduma bora na nafuu kwa watu wa Samunge, huduma inayoambatana na uwepo wa mtandao madhubuti pamoja na huduma nyingine lukuki ambazo zimekuwa zikipatikana na kufurahiwa na wateja wengine wa Airtel Tanzania nzima.

  “Uwepo wetu wetu Samunge na maeneo mengine ya jirani, kwa hakika kutaleta chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi na wageni wa maeneo haya. Kuwaunganisha watu wa Loliondo wakati huu ambapo mahitaji ya mawasiliano ni makubwa, kunadhihirisha dhamira yetu ya kuwa mbele zaidi kwa kila tunalofanya”, alieleza zaidi.

  Kwa kipindi cha karibuni, eneo la Samunge limeonyesha kuwepo ongezeko kubwa la wageni wanaotembelea, kutoka Afrika ya Mashariki na Kati, wengi wao wakiwa wanaelekea kupata tiba maarufu ya kikombe cha Mchungaji Mstaafu Ambikile Mwaisapile.

  Inakadiriwa ya kwamba idadi ya wageni wanaoingia na kutoka siku inafikia hadi watu 25,000, huku eneo hilo likiwa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa kutokuwa na mawasiliano ya simu za mkononi. Kwa kuwepo kwa Airtel sasa hivi, kutawawezesha watu kuweza kupiga na kupokea simu na sms, jutumia huduma nafuu ya internet na pia kuweza kutuma na kupokea fedha kupitia Airtel Money.

  Vilevile, kuwepo kwa mtandao wa airtel eneo hilo kutawawezesha wageni mbalimbali ambao wengine hutoka nje ya mipaka ya Tanzania kuweza kunufaika na huduma ya One Network, ambayo inawawezesha kuwasiliana kwa kutumia viwango vya gharama vya nchi wanazotoka.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidore Shirima amesema “Sisi, kama serikali, tumefarijika sana kuona juhudi hizi za uongozi na wafanyakazi wa airtel katika kuhakikisha wanafikisha huduma ya mawasilano ya simu za mkononi kwa wana jumuia ya samunge na maeneo jirani. Kuwepo kwa mtandao wa Airtel hapa sit u ya kwamba utaleta manufaa ya kiuchumi, bali pia kutachochea maendeleo ya huduma za kijamii kwa wageni na wenyeji”.
   
 4. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mission accomplished.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Leo nimewasiliana na ndugu yangu kijijini Samunge kaniambia foleni si kubwa sana anaweza kurejea kesho.Hongera Airtel mawasiano ni jambo zuri wapo jamaa waliokwenda kupata kikombe kwa Babu Loliondo walikutana shida mbali mbali hadi wengine mauti lakini ndugu wa wakuwasaidia hakuwa na habari kwakuwa eneo lenyewe halikuwa na network ya mtandao wowote.
   
Loading...