Kilimo kwanza hakihusishi power tiller pekee, kilimo kwanza ni kila kitu kihusucho kilimo, pasipo faa power tiller patapelekwa kinachofaa. Hivi ukanunue power tiller mahali pakulima na trekta la horse power 200 utakuwa una akili sawasawa?<br />
<br />
Nakuona kuwa u mbumbumbu wa kutupwa, hujui kuwa maua ni zao moja lenye faida sana duniani? kweli umbumbumbu umekukithiri. Leo Mbeya kiwanja cha ndege cha Kimataifa kina pigiwa debe haraka haraka ili waweze kulima maua kwa wingi, kama hujui umuhimu wa mazao ya maua tafadhali nenda Arusha na Moshi ukawaeleze hayo, magwanda wenzako watakucheka kwa hilo, wengi wako huko na wanafaidika sana na maua.<br />
<br />
Ukumbuke kuhusu Kilimo kwanza, dhanna yake sio kutoa matrekta ya bure,kama unaona ya Suma ni ghali wala hujalazimishwa lazima ukanunue hayo, unaweza hata wewe kuleta matrekta ya rahisi, mbona wengi sana wanaleta hata ya mitumba na yote hayana ushuru kabisa, au hayo huyajui. Kama wewe unangoja ya bure, utangoja sana. Hata huyo Slaa na Mbowe hawawezi kukupa cha bure, kama unabisha nenda pale Bilicanas ukaone kama kuna bure pale! au nenda CCBRT. Usintie kichefu chefu kwa kuongea utumbo.