Babu Loliondo awaonya wanaomuiga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu Loliondo awaonya wanaomuiga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Apr 16, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Babu Loliondo awaonya wanaomuiga

  Imeandikwa na Na Grace Chilongola, Loliondo;
  Tarehe: 15th April 2011


  [​IMG]


  MCHUNGAJI Ambilikile Masapila wa Kijiji cha Samunge Loliondo maarufu kama Babu, amewataka wananchi wajihadhari na matapeli wanaoibuka na kudai wanatoa tiba ya kikombe kama ya kwake.

  Pia alisema maofisa wanaotumia fursa ya utoaji wa vibali vya kwenda kwake kunywa dawa (kikombe) kwa kujinufaisha na rushwa, ni maadui wa Mungu na kwamba fedha wanazopokea zitaisha bila kufanyia kitu cha maana na wao kubaki hohehahe.


  Aliyasema hayo Alhamisi wakati akizungumza na timu ya waandishi wa habari kutoka mkoani Mwanza waliomtembelea nyumbani kwake Samunge, wilayani Ngorongoro kuona adha mbalimbali wanayoipata abiria wanaokwenda kwa ‘Babu' kupata tiba ya kikombe.


  "Wananchi wajihadhari na watu wa sehemu nyingine wanaodai wameoteshwa na Mungu na kutoa tiba ya kikombe, ni matapeli tena wauaji," alisema na kuwaonya wananchi kujihadhari nao.


  Alidai, wakati Mungu anamuotesha dawa hiyo alikuwa peke yake, watu wanaompinga wakiwemo wachungaji wa madhehebu mengine, wanapingana na Mungu aliyempa dawa ya kuponya watu bila kujali itikadi zao, dini, kabila au vyama vyao vya siasa.


  "Wanaotoa vibali katika njia yoyote waache kutumia nafasi hiyo kujipatia utajiri kwa rushwa, yeyote anayefanya hivyo hela anayoipata haitamsaidia, atafilisika na kuwa na hali ambayo hajawahi kuipata maishani," alieleza Mchungaji Mwasapile.


  Awali msimamizi wa Kituo cha tiba cha babu aliyejitambulisha kwa jinala Fredrick Nsajile aliwaambia waandishi hao kuwa wananchi wafuate utaratibu uliowekwa na serikali bila kutoa rushwa na waratibu wa safari katika vituo mbambali watende haki.


  Nsajile alieleza kwamba, Mchungaji Mwasapile hapendi wagonjwa wasafirishwe kwa malori, wanaumia na kuteseka sana njiani na kudai kuna baadhi ya magari yanayotoa rushwa ambayo yanaonekana kupendelewa kuruhusiwa mara kwa mara kupeleka wagonjwa Samunge.


  Msimamizi huyo alieleza kuwa, idadi ya watu wanaopata tiba (kunywa kikombe) kwa siku wanafikia 8,000 na sio 2,000 kama ambavyo vyombo vya habari vimekuwa vikieleza.


  Wakiwa katika ziara ya kumtembelea babu waandishi hao walishuhudia malori zaidi ya manane wilayani Serengeti mkoani Mara likiwemo maalum kwa ajili ya kubeba samaki yakiwa yamebeba watu na kuwatelekeza kwenye mageti kwa zaidi ya wiki baada ya kukosa kibali cha kuwavusha.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  jana niliona magazeti yanasema watu/wateja wamepungua sana.babu usiwe na wasiwasi,u ar top on the list tunajichangisha nauli
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Mapato Samunge vurugu tupu

  Thursday, 14 April 2011 21:39

  [​IMG]
  Mussa Juma, Samunge

  UONGOZI wa Kijiji cha Samunge, umetoa siku mbili kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuwaondoa maofisa wake wanaokusanya ushuru wa magari na helikopta zinazopeleka wagonjwa kijijini hapo kupata tiba inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila, vinginevyo utasitisha utoaji wa tiba hiyo.

  Uamuzi huo ulifikiwa jana katika Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Samunge, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nanenane na kuhudhuriwa na maofisa kadhaa wa Serikali, akiwamo mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngorongoro, Bakari Gaima.

  Akitangaza uamuzi huo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Michael Lengume alisema mkutano huo unamtaka mkurugenzi kuwaondoa maofisa wanaokusanya ushuru wa magari na helikopta ifikapo leo na kwamba kazi hiyo sasa itaanza kufanywa na wakusanya ushuru wa kijiji kuanzia Jumamosi.

  "Kama halmashauri itakaidi agizo hilo, tutasitisha utoaji wa huduma ya tiba katika kijiji hiki baada ya kukutana na Mchungaji Mwasapila na kuyazuia magari," alisema.


  Wakizungumza kabla ya kufikiwa uamuzi huo, Diwani wa Kata ya Samunge, Jackson Sandea, Kiongozi Mkuu wa mila wa Kabila la Wasonjo (Mwanamiji), Peter Dudui, Solomon Baragiswa, Mary Meano na Njuda Lemindi walisema mapato ya magari na helikopta ni haki ya kijiji hicho na siyo halmashauri wala Serikali Kuu pekee.

  Sandea alisema kamwe hawatakikubali kitendo cha halmashauri kupora mapato hayo kwani Serikali ya Kijiji inatambuliwa kisheria na ina haki ya kukusanya mapato kama vilivyo vijiji vingine nchini.


  "Huu ni uporaji wa mapato yetu, tulianza kukusanya vizuri na kutumia fedha katika kazi za usafi wa mazingira, kuchimba vyoo na kutumia katika miradi mingine lakini sasa wametuvamia na kuanza kukusanya wao," alisema diwani huyo na kuongeza:

  "Katika vituo wanatoza fedha za vibali, wanachukua fedha za ukaguzi wa magari na nyingine nyingi tu ambazo zinalalamikiwa na wananchi. Kwa nini tena tuambiwe na huku kwetu fedha zinakusanywa kwa ajili yao?"

  Dudui alisema viongozi wa mila wanapinga utaratibu wa halmashauri wa kukusanya mapato yote bila kueleza kijiji kitanufaika vipi na ujio wa maelfu ya watu."Sasa vyanzo vya maji vimechafuliwa, mashamba yameharibiwa kutokana na kutupwa taka mbalimbali kama chupa za maji, magari yameegeshwa mashambani, njaa itakuja. Je, nani atawasaidia hawa wananchi?" alihoji Dudui.


  Kiongozi huyo wa kimila pia alieleza kushangazwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuamua kupeleka Samunge watu wa kufanya usafi kutoka nje ya kijiji hicho akisema hatua hiyo inawanyima ajira vijana wa Samunge.

  Kwa upande wake, Baragiswa aliwasihi wananchi wa Samunge kupunguza jazba kutokana na kuporwa mapato yao, akashauri taratibu za kiserikali zifuatwe ili haki ya kijiji kupata mapato irejeshwe.


  "Mimi sipendi kuwafukuza kwa nguvu watu wa halmashauri, dunia nzima sasa inatazama Samunge tusijichafue. Taratibu zifuatwe ili kijiji kikusanye mapato yake," alisema Baragiswa.Lemindi alisema Serikali za vijiji zinatambuliwa kisheria na halmashauri haiwezi kuingilia masuala ya kijiji bila majadiliano hivyo, ni busara suala hilo kumalizwa kisheria.

  Katika mchango wake, Mary Meano alisema alilalamikia uwapo wa kina mama lishe wengi kutoka nje ya wilaya hiyo ambao walifika Samunge kupata tiba na sasa wamefungua migahawa ambayo haina huduma muhimu kama vyoo."Kina mama wa Samunge tunashindwa kufanya biashara. Kuna wageni wengi hapa bila utaratibu, tunaomba kijiji kiratibu ujio wao na kuweka utaratibu mzuri wa huduma za afya na vyoo hapa kijijini," alisema Meano.


  Tangu Mchungaji Ambilikile Mwasapila aanze kutoa tiba ya magonjwa mwanzoni mwa mwaka huu, wastani wa magari 1,000 yanafika Samunge kwa siku, huku helikopta ikifanya safari kati ya nne na sita kwa siku.


  Halmashauri Ngorongoro yajivua lawama


  Gaima aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, alisema haijapora mapato ya kijiji, bali inatekeleza uamuzi wa kikao cha wakuu wa mikoa inayopakana na Ngorongoro na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Gaima alisema kikao hicho kiliamua kuwa halmashauri ikusanye Sh5,000 kwa kila gari na kati ya hizo Sh3,000 zitapelekwa kusaidia vituo vya kuratibu magari yanayokwenda Samunge vya Bunda, Arusha, Longido na Babati na nyingine Sh2,000 zibaki halmashauri.

  "Iliamuliwa mapato kukusanywa na halmashauri ili iwe rahisi kupatikana hizo 3,000 na kuhusu kijiji kuna utaratibu utaandaliwa ili kinufaike na pia ilionekana ni busara halmashauri kusimamia mapato ili kuratibu zoezi zima la usafi na utunzwaji wa mazingira," alisema Gaima. Kaimu Mkurugenzi huyo pia alikanusha uvumi kuwa uamuzi wa kutaka halmashauri ikusanye fedha, ulitokana na mapendekezo ya Mchungaji Mwasapila.


  "Mchungaji alishirikishwa tu baada ya uamuzi kufikiwa hasa baada ya idadi kubwa ya watu kufurika hapa ambapo ilisababisha watu kufariki kutokana na kukosa huduma," alisema Gaima.


  Akizungumzia ajira kwa vijana wa Samunge, Gaima alisema waliamua kutafuta vijana kufanya kazi za usafi kutoka nje ya Samunge baada ya kupata taarifa za vijana wa Samunge kugoma kufanya usafi.

  Wahandisi wa JKT watua Samunge


  Hatimaye wahandisi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), juzi walitua Samunge kuainisha maeneo ya kuchimbwa vyoo ili kuimarisha usafi lakini kabla ya kufanya lolote walipata kikombe cha tiba.

  Wahandisi hao walikuwa wameandamana na Diwani wa Samunge, Sandea na ujio wao ilielezwa kuwa ni wa kuchimba vyoo na kuboresha mazingira ya usafi. Bado huduma za vyoo na usafi ni mbaya katika Kijiji cha Samunge na vijiji vya jirani na pia uchafu umezagaa barabarani kuanzia Kigongoni hadi Samunge na Loliondo.
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hahahahahahahaha! Ameona jero jero zmepungua au? Ndo mana kapatwa na wasi.
   
 5. N

  Nguto JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,649
  Likes Received: 626
  Trophy Points: 280
  No way!!! Hayuko after money!! Angetaka hela angedai hela nyingi kwa tiba sio 500 ambayo nayo tunaambiwa ina mgao.
   
 6. A

  Ayman Anwar New Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni njia moja wapo ya kupata pesa, ama kweli watu wanajua kutafuta
   
 7. A

  Ayman Anwar New Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ile 500 kwa siku anaingiza mamilioni ya pesa
   
 8. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Jana nimecheka sana baada ya jamaa mmoja kujitokeza hadharani Mbagala na kukiri kwamba anamawasiliano ya kindoto na babu. Na kwamba huko wanakokutana yeye ni Senior kwa babu na babu analijua hilo. Hawajawahi kukutana physically, lakini hukutana katika ulimwengu mwingine.
   
 9. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mzushi tu babu hana lolote
   
 10. LivingBody

  LivingBody Senior Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mambo kwelikweli,, bado kidogo tusubili tu.
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  'Mliokunywa ‘kikombe' mkapime

  Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 16th April 2011 @ 16:49 Imesomwa na watu: 226; Jumla ya maoni: 0
  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema, watu waliokunywa kikombe cha Babu Loliondo na maeneo mengine, wakapime hospitali ili kuthibitisha kwamba wamepona au la.

  Pinda pia amewaeleza wabunge mjini Dodoma kuwa, wanaotoa tiba mbadala na tiba asili wanapaswa kujitambulisha kisheria kwa kujaza fomu maalum ya kujisajili na kuthibitisha usalama wa dawa hiyo katika maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa na kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

  "Napenda kuwaomba wananchi wote kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara. Aidha, pale ambapo kuna umuhimu wa kutumia dawa na tiba mbadala ni vizuri kujiridhisha na usalama wa dawa zinazotumika na kurejea kupima maradhi husika katika maabara zinazojulikana kisheria ili kujiridhisha kama maradhi yamekwisha" amesema Pinda.

  Amesema, wanaotoa tiba mbadala wanapaswa kuzingatia sheria za nchi kwa kuhakikisha kuwa wanajisajili wao wenyewe, na wanasajili pia dawa wanazozitumia kutoa tiba na vituo vyao.

  Amewaagiza waratibu wa tiba asili na tiba mbadala wahakikishe kwamba kila mtoa huduma wa tiba hizo katika eneo lake anasajiliwa.

  Kwa mujibu wa Pinda, Tanzania inakabiliwa na maradhi makubwa kama vile Malaria, Kifua Kikuu, Shinikizo la Damu, Kisukari, Saratani na Ukimwi.

  Amesema, Malaria, Kifua Kikuu na Ukimwi yamepata msukumo mkubwa kitaifa na kimataifa katika kupambana nayo.

  "Hata hivyo, magonjwa ya Shinikizo la Damu, Kisukari na Saratani yamekuwa yakiongelewa lakini badi hayajapata msukumo wa kutosha kitaifa. Vile vile watu wengi wamekuwa wakipima Malaria, Kifua Kikuu na Kisukari lakini wamekuwa wazito kupima magonjwa mengine niliyoyataja hapo juu na hasa UKIMWI" amesema.

  Waziri Mkuu amezungumzia kwa kirefu ugonjwa wa saratani kwa kusema kuwa unapoteza nguvu kazi ya taifa na kwamba, gharama za kuutibu ni kubwa sana.
  Kwa mujibu wa Pinda, mchakato wa kumtibu mgonjwa mmoja huchukua miezi sita hadi mwaka mmoja na unaweza kugharimu hadi sh milioni tano.

  Amewaeleza wabunge kuwa, uwezo wa kutambua magonjwa ya saratani nchini umeongezeka lakini takwimu zinaonesha kuwa asilimia 80 hadi 85 ya wagonjwa wanaofika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam huwa katika hatua ya juu ya ugonjwa hivyo mgonjwa huwa ameathirika kwa kiasi kikubwa.

  "Takwimu zinaonesha kwamba, ni kati ya asilimia 15 hadi 20 tu ya wagonjwa wanaokuwa katika hali hiyo hupata nafuu baada ya matibabu. Kwa maana nyingine asilimia 80 hadi 85 ya wagonjwa hao huugua kwa muda mrefu namwisho wake wanapoteza maisha" amesema Pinda.
   
 12. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni uzushi mtupu.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Babu Loliondo abanwa


  na Martin Malera, Dodoma


  [​IMG] SERIKALI imesema kuwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila wa Kijiji cha Samunge pamoja na watu wengi waliojitokeza kudai wanatibu magonjwa sugu kwa kuoteshwa na Mungu, wanapaswa kufuata sheria ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala namba 23 ya mwaka 2002.
  Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akitoa hotuba yake ya kuahirisha mkutano wa tatu wa Bunge. Alisema kumekuwa na kuibuka kwa watabibu hao wanaodai kuoteshwa na Mungu, ambako kumetokana na kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa sugu nchini.
  Alitaja masharti hayo kuwa ni pamoja na kujitambulisha kisheria kwa kujaza fomu maalumu ya kujisajili na kuthibitisha usalama wa dawa hiyo katika Maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa na kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
  Pinda aliwasihi wote wanaotumia dawa hizo kwamba wasiache kujiridhisha kwa kufanya utaratibu wa kupima hospitali ili kuona kama tatizo walilokuwa nalo limekwisha.
  Katika hotuba yake, Pinda alisema kuwa tathimini iliyofanywa na watalaamu wa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini mwanzoni mwa mwaka huu, ilionesha kwamba patakuwepo na upungufu wa wastani wa Megawati (MW) 264 za nishati ya umeme katika Mfumo wa Gridi ya Taifa mwaka 2011.
  Kwa hali hiyo, alisema wananchi watarajie kuwa na upungufu wa umeme wa wastani wa Megawati (MW)60 katika mwaka wa 2011 na hali hiyo inatokana na mahitaji ya umeme kuongezeka kwa kasi kuliko uwekezaji katika miradi mipya ya kuzalisha umeme.
  Pia alizungumzia ajira za walimu ambapo aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri wasiwasumbue Walimu kuwalipa malipo ya Stahili zao mara wanapofika kuripoti katika vituo walivyopangiwa kuanza kazi.
  Akizungumzia mchakato wa madiliko ya Katiba, Pinda alisema baada ya Bunge kuurejesha muswada huo kwa wananchi, sasa ni fursa kwa wananchi kuitazama upya katiba yetu.


  [​IMG]
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  IN PICTURES: Tanzania's 'magic' drink

  [​IMG] Add a comment (2 comments so far)
  You need to login first to submit a comment.

  commentAds


  1. Submitted by starclear
   Posted March 29, 2011 10:47 AM
   "Local media report that about 52 people have died while waiting to see him." In 2009, the government outlawed all witchdoctors and traditional healers. But on Monday, Prime Minister Mizengo Pinda said he would not take any action to stop Mr Mwasapile's activities." Why is that?

  2. Submitted by fourshotz
   Posted March 30, 2011 09:47 PM
   Ngugi's Wizard of the Crow nini?
  Mr Ambikile Mwasapile (left) serves out the the miracle drink. The pilgrimage to Loliondo was stopped on March 28, 2011 as it emerged 52 people had died awaiting treatment. PHOTO | CITIZEN


  • [​IMG]
  • [​IMG]
  • [​IMG]
  • [​IMG]
  • [​IMG]

  « Previous Page Next Page »
  Add a comment (0 comments so far)
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Babu wa Loliondo ageuka dili la madiwani

  Imeandikwa na Ahmed Makongo, Bunda; Tarehe: 18th April 2011 @ 07:35 Imesomwa na watu: 31; Jumla ya maoni: 0
  MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, wameutaka uongozi wa wilaya hiyo kuruhusu Halmashauri yao kuanza kukusanya ushuru kwa magari yote yanayopita wilayani hapo kupeleka wagonjwa Loliondo kwa Mchungaji Ambilikile Mwaisapile.

  Madiwani hao waliazimia kutozwa kwa ushuru huo wakati wa kikao cha bajeti cha Halmashauri hiyo ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wao, Joseph Malimbe.


  Madiwani hao waliazimia kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isaac, ili washirikiane kuandaa utaratibu wa kukusanya ushuru wa magari kutoka katika kituo hicho cha Kanda ya Ziwa.


  Walisema ushuru huo utasaidia kuboresha usafi na kuweka miundombinu mizuri katika kituo hicho ambacho kimekuwa kikipokea magari mengi kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kupeleka wagonjwa katika kijiji cha Samunge kupata kikombe cha Mchungaji huyo maarufu Babu.


  "Tutazungumza na Mkuu wa Wilaya yetu, maana wote ni Serikali, tuzungumze namna ya kukusanya ushuru kwenye kituo hicho...na ushuru huu utasaidia kuboresha usafi na kuboresha miundo mbinu," alisema Malimbe.


  Kwa sasa kila gari inayopita katika kituo hicho, imekuwa ikitozwa Sh 1,000 tu, kwa ajili ya kibali cha kuruhusiwa kwenda huko Loliondo.


  Wakati huo huo, Lucas Raphael anaripoti kutoka Tabora kuwa uongozi wa mkoa huo umeweka utaratibu wa wananchi kwenda kunywa dawa kwa Babu kupitia kituo cha Kanda ya Kati.


  Kwa mujibu wa utaratibu huo, Jumatatu, Jumanne na Jumapili watapita watu wenye magari madogo na Jumatano, Alhamisi na Jumamosi zitakuwa kwa wasafiri wanaotumia mabasi.


  Akitoa utaratibu huo jana, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa alisema uamuzi huo umefikiwa wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.


  Alisema kila mwenye basi atachukua watu wasiozidi 60 kwa siku moja huku akisisitiza wagonjwa mahututi wasipelekwe.


  Mwinyimsa alisema uongozi wa Mkoa umeweka utaratibu wa kila mwenye gari dogo au basi kupata kibali cha muda cha kuwapeleka watu huko kwa kupitia kituo cha Babati ambacho kinachotumiwa na mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora, Manyara pamoja na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.


  Mwinyimsa alisema Ofisi ya Waziri Mkuu imeweka utaratibu wa Kanda tatu kwa ajili uthibiti wa usafirishaji wa abiria kwenda Loliondo ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini pamoja na Kanda ya Kati.


  Alisema kuwa Tabora imepangiwa kupeleka watu wasiozidi 60 kila siku kwenda kunywa dawa ya Babu huko Samunge na kuwataka wote wanaotaka kwenda Loliondo kujiandikisha kwenye ofisi za wakuu wa wilaya wanakotoka badala ya kila mmoja kuondoka apendavyo.


  Alisema ofisi za wakuu wilaya zitawasilisha majina kwa Katibu Tawala wa Mkoa ili waratibu idadi ya watu wa mkoa mzima wanaokwenda Babati kila siku, ili wapate vibali vya magari husika bila kuchelewa.


  Alisema kila gari linalokwenda Loliondo litatozwa Sh 5,000 katika kituo cha Yamimdito na wataokusanya tozo hiyo ni Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Babu wa Loliondo ageuka dili la madiwani

  Imeandikwa na Ahmed Makongo, Bunda; Tarehe: 18th April 2011 @ 07:35 Imesomwa na watu: 31; Jumla ya maoni: 0


  MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, wameutaka uongozi wa wilaya hiyo kuruhusu Halmashauri yao kuanza kukusanya ushuru kwa magari yote yanayopita wilayani hapo kupeleka wagonjwa Loliondo kwa Mchungaji Ambilikile Mwaisapile.

  Madiwani hao waliazimia kutozwa kwa ushuru huo wakati wa kikao cha bajeti cha Halmashauri hiyo ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wao, Joseph Malimbe.


  Madiwani hao waliazimia kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isaac, ili washirikiane kuandaa utaratibu wa kukusanya ushuru wa magari kutoka katika kituo hicho cha Kanda ya Ziwa.


  Walisema ushuru huo utasaidia kuboresha usafi na kuweka miundombinu mizuri katika kituo hicho ambacho kimekuwa kikipokea magari mengi kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kupeleka wagonjwa katika kijiji cha Samunge kupata kikombe cha Mchungaji huyo maarufu Babu.


  “Tutazungumza na Mkuu wa Wilaya yetu, maana wote ni Serikali, tuzungumze namna ya kukusanya ushuru kwenye kituo hicho...na ushuru huu utasaidia kuboresha usafi na kuboresha miundo mbinu,” alisema Malimbe.


  Kwa sasa kila gari inayopita katika kituo hicho, imekuwa ikitozwa Sh 1,000 tu, kwa ajili ya kibali cha kuruhusiwa kwenda huko Loliondo.


  Wakati huo huo, Lucas Raphael anaripoti kutoka Tabora kuwa uongozi wa mkoa huo umeweka utaratibu wa wananchi kwenda kunywa dawa kwa Babu kupitia kituo cha Kanda ya Kati.


  Kwa mujibu wa utaratibu huo, Jumatatu, Jumanne na Jumapili watapita watu wenye magari madogo na Jumatano, Alhamisi na Jumamosi zitakuwa kwa wasafiri wanaotumia mabasi.


  Akitoa utaratibu huo jana, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa alisema uamuzi huo umefikiwa wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.


  Alisema kila mwenye basi atachukua watu wasiozidi 60 kwa siku moja huku akisisitiza wagonjwa mahututi wasipelekwe.


  Mwinyimsa alisema uongozi wa Mkoa umeweka utaratibu wa kila mwenye gari dogo au basi kupata kibali cha muda cha kuwapeleka watu huko kwa kupitia kituo cha Babati ambacho kinachotumiwa na mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora, Manyara pamoja na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.


  Mwinyimsa alisema Ofisi ya Waziri Mkuu imeweka utaratibu wa Kanda tatu kwa ajili uthibiti wa usafirishaji wa abiria kwenda Loliondo ikiwemo Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini pamoja na Kanda ya Kati.


  Alisema kuwa Tabora imepangiwa kupeleka watu wasiozidi 60 kila siku kwenda kunywa dawa ya Babu huko Samunge na kuwataka wote wanaotaka kwenda Loliondo kujiandikisha kwenye ofisi za wakuu wa wilaya wanakotoka badala ya kila mmoja kuondoka apendavyo.


  Alisema ofisi za wakuu wilaya zitawasilisha majina kwa Katibu Tawala wa Mkoa ili waratibu idadi ya watu wa mkoa mzima wanaokwenda Babati kila siku, ili wapate vibali vya magari husika bila kuchelewa.


  Alisema kila gari linalokwenda Loliondo litatozwa Sh 5,000 katika kituo cha Yamimdito na wataokusanya tozo hiyo ni Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Babu aomba wagonjwa wasimshangilie Send to a friend Sunday, 17 April 2011 20:54

  Mussa Juma, Samunge
  MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika Kijiji cha Samunge, Loliondo amewaomba wagonjwa na watu wengine wanaokwenda kupata huduma yake kuacha kumshangilia kila wanapomwona.

  Mchungaji Mwasapila ambaye amekuwa maarufu kwa jina la Babu alisema hayo jana katika mazungumzo yake ya kila siku asubuhi kabla ya kuanza kutoa tiba.Aliwataka wagonjwa na jamaa zao kumshangilia Mungu akisema ndiye anayewatibu na siyo yeye.
  "Nawaona nikitokea kuanza kutoa tiba mnashangilia, pia nikiwaeleza kuhusu dawa hii mnashangilia, anayeponya siyo mimi ni Mungu hivyo mnapaswa kumshangilia Mungu wenu mara kwa mara, "alisema Mwasapila.
  Katika hatua nyingine, mgogoro wa mapato kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Arusha na Serikali ya Kijiji cha Samunge umemalizika baada ya kuamuliwa kwamba kuanzia sasa kijiji hicho kitapata mgawo wa Sh2,000.
  Uamuzi huo ulifikiwa juzi jioni katika kikao cha dharura kati ya wajumbe wa Serikali ya Kijiji cha Samunge na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali.
  Kikao hicho kilifanyika siku ya mwisho ambayo ilitolewa na wakazi wa kijiji hicho kupitia mkutano wao mkuu kwa halmashauri hiyo iwe imewaondoa wakusanya ushuru wake kijijini hapo la sivyo watasitisha huduma ya tiba inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila.
  Akizungumza na Mwananchi jana, Lali, alisema kijiji hicho kitakusanya ushuru huo wa Sh 2,000 kwa ajili ya usafi na uboreshaji wa mazingira ya Samunge.
  "Kulikuwa na kutoelewana tu, lakini uamuzi wa awali ulikuwa ni Sh2,000 kubaki Samunge kusaidia masuala ya mazingira na afya. Sasa baada ya kuelimishana nadhani limekwisha na watu wao wanashirikiana na halmashauri kukusanya ushuru," alisema Lali.
  Alifafanua kwamba, fedha hizo zinazokusanywa ni za Serikali na zitapelekwa benki na baadaye Sh3,000 zitapelekwa kusaidia vituo vya magari na Sh2,000 zitapangiwa utaratibu na kijiji jinsi ya kutumika.
  Vituo vya magari vitakavyonufaika na fedha hizo ni Bunda, Arusha, Babati na Longido.

  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Samunge, Michael Lengume alisema kutokana na uamuzi huo, jana wakusanya ushuru wa kijiji walikuwa wakishirikiana na wenzao wa halmashauri.

  "Tayari tumeteua watu wetu wanakusanya ushuru. Imekubaliwa kuwa tutachukua pesa yetu Sh2,000 na hizo zao 3,000 watapeleka katika vituo vyao," alisema Lengume.

  Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wakusanya ushuru wa kijiji hicho Joel Ezekiel, Gadiel Mearo na Charles Kisida wakikusanya ushuru huo pamoja na ofisa wa halmashauri.
  Tangu Aprili 6, mwaka huu, halmashauri ilianza kukusanya ushuru wa Sh5,000 kwa magari yanayoingia Samunge.
  Awali, kijiji kilikuwa kinakusanya Sh2,000, lakini wakusanya ushuru wake waliondolewa na halmashauri kutokana na uamuzi wa kikao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi na wakuu wa mikoa inayopakana na Ngorongoro, kwa kutaka kuanzisha mpango wa kuratibu na kutoa vibali vya magari yanayokwenda Samunge.

  Vigogo wa Ikulu Kenya
  wazidi kumiminika
  Maofisa wa Ikulu ya Kenya wakiongozwa na Chifu Morijo Loita na familia zao ambao kwa pamoja ni 81, wamewasili jana kwa Mchungaji Mwasapila kupata kikombe.

  Jana, msafara wa maofisa hao ulitua Samunge ukiwa na magari saba na mara baada ya kuwasili walijitambulisha na kuanza kupewa dawa.
  Ujio wa maofisa hao unaelezwa kwamba huenda ukasababisha vigogo wengine kadhaa katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati, kufika Samunge kupata kikombe cha dawa kwa Mchungaji Mwasapila.
  Juzi, baadhi ya wabunge wa Kenya na wagombea wa Useneta, walikwenda na wapigakura wao kwa mchungaji huyo kupata kikombe cha dawa.

  Kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji aliyepo Samunge, Hussein Hamis idadi ya raia wa Kenya waliofika hapo sasa imefikia 2,429 hawa wakiwa ni wale tu waliojitambulisha rasmi.

  Mmoja afariki dunia Samunge
  Mtu mmoja amefariki dunia jana, kabla ya kupata kikombe cha tiba kutokana na kukaa muda mrefu bila ya huduma yoyote ya afya.

  Foleni ya magari jana ilifikia zaidi ya kilometa 10, hali ambayo inatishia tena kutokea kwa vifo hasa kwa wagonjwa ambao hawana dawa za kutosha na chakula.
  Kabla ya kuwekwa utaratibu wa kutoa vibali kwa magari yanayokwenda Samunge, watu 78 walifariki kabla ya kupata tiba kutokana na foleni kubwa na hivyo kuchelewa kupata kikombe na wengine kupata baada ya hali zao kuwa mahututi.
   
 18. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yeye anajuaje kuwa na hao wengine hawajaoteshwa na huyo Mungu wake? Wezi tu wote, hawana lolote
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  PHP:
  [B] [IMG]https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon1.png[/IMG] Re: Babu Loliondo awaonya wanaomuiga [/B]

      
  Yeye anajuaje kuwa na hao wengine hawajaoteshwa na huyo Mungu wakeWezi tu wotehawana lolote
  Anaona wanamkatia dili......kwa hiyo ni lazima ajihami.....................
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Maofisa wa Ikulu Kenya wapata kikombe cha Babu Send to a friend Sunday, 17 April 2011 11:16

  Mussa Juma, Samunge
  MAJAJI wanane wa Mahakama Kuu na Rufani wa Tanzania, Maofisa wa Ikulu wa Serikali ya Kenya, jana walifika Samunge kupata dawa ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapila.
  Maofisa wa Ikulu ya Kenya waliofika Samunge kupata kikombe cha dawa waliongozana na wanasiasa kadhaa mashuhuri wa nchi hiyo waliofika huko pamoja na wapiga kura wao.
  Vigogo hao wa serikali za Kenya na Tanzania, walifika Samunge mchana wakiwa wanasindikizwa na askari polisi ambapo walienda moja kwa moja kwa Mchungaji Mwasapila kujitambulisha na kupata kikombe.
  Kundi la kwanza kufika kijijini hapo lilikuwa la maofisa wa Ikulu ya Kenya na walinzi wa Rais Mwai Kibaki.
  Vigogo hao walikuwa wameongozwa kwenye msafara huo na Chifu John Saitoti aliyekuwa amevalia sare za jeshi akiwa na mke wake na maofisa wengine sita.
  Mmoja wa maofisa hao, alikuwa ni Chifu Daniel Kaka anayetoka Ikulu ya Rais Mwai Kibaki.
  Wakati kundi hilo likipata kikombe, aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Narok Kusini, Steven Ndutu ambaye anagombea useneta wa jimbo hilo, alipata kikombe hicho akiwa na kundi la wapigakura wake.
  Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Ndutu alisema ameamua kufika Samunge na baadhi ya wapiga kura wake, ambao ni wagonjwa.Ofisa wa Ikulu ya Kenya, Chifu Saitoti ambaye alijitambulisha kwa maofisa Usalama wa Tanzania na Polisi waliopo Samunge, alisema amekuja kumleta mke wake, Lenini Saitoti, anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
  "Nimetoka Nairobi, nimemleta mke wangu kunywa dawa baada ya kupata taarifa za mchungaji huyu kupitia vyombo vya habari," alisema Saitoti.

  Majaji wa Tanzania
  Majaji wanane wa Rufani na Mahakama Kuu Tanzania jana walitinga Samunge kupata kikombe cha Mchungaji Mwasapila wakiwa wameongozana na maofisa kadhaa wa Serikali.Baada ya kuwasili Loliondo majaji hao waliripoti Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro na baadaye kuelekea Samunge.Jaji Fredrica Mgaya kabla ya kupata kikombe, alikwenda kujitambulisha kwa Mchungaji Mwasapila na kusalimiana naye.
  Mbali na majaji hao, Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, naye alipata kikombe cha cha dawa ya Babu kwenye majira ya saa saba mchana jana.

  Wageni waongezeka
  Mbali na ujio wa vigogo hao, watu kutoka nje ya nchi wanaofika Samunge wameongezeka maradufu.
  Kwa mujibu wa taarifa za maofisa uhamiaji waliyopo Samunge, hadi jana Wakenya walioandikishwa walikuwa 2,596.
  Ofisa Uhamiaji aliyepo Samunge, Hussein Hamis aliliambia gazeti hili kuwa miongoni mwa wageni waliofika kijijini hapo walikuwapo Waganda wanne, Wanyarwanda wawili na Walebanon watatu.Kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji huyo wageni wengine ni Wamarekani wawili, Wazimbabwe wanne, Mdenmark mmoja na Waingereza wawili.
  "Kuna baadhi hatukupata taarifa zao kutokana na kutojitambulisha, hivyo idadi ya wageni ni kubwa zaidi ya hii tuliyonayo," alisema Hamis.

  Ajali yaua wawili
  Watu wawili walifariki dunia jana na wengine zaidi ya saba kujeruhiwa vibaya, baada ya gari aina ya Land Rover walilokuwa wanasafiria wakati wanatoka kwa Mchungaji Mwasapila kupata dawa kuacha njia na kuanguka.
  Gari hilo lilianguka baada ya kuteleza kwenye changarawe katika eneo la Sale, kilometa chache kutoka Kijiji cha Samunge.
  Dereva wa gari linalobeba watu kutoka Arusha kwenda Samunge, Amani Mshana, alisema wakati wakiwatoa majeruhi wa ajali hiyo ambao walikuwa wamenasa kwenye gari hilo, kuwa chanzo cha ajali ni ubovu wa barabara.
  "Tulikuwa tunafuatana na hili gari ila lilivutwa na changarawe na kuanguka ...hapa tayari kuna miili ya watu wawili waliofariki na wengine ni majeruhi," alisema Mshana.

  Foleni yaongezeka
  Katika hatua nyingine, maelfu ya watu wamefurika Samunge na sasa foleni ya magari imefika zaidi ya kilomita 10 kutoka kijijini hapo.
  Idadi hiyo ya watu haijawahi tokea tangu Serikali iweke utararibu wa kusimamia magari yanayokwenda Samunge.
  Ongezeko hilo sasa limeanza kusababisha watu kukaa zaidi ya siku mbili kusubiri kupata kikombe na kama lisipodhibitiwa, huenda vifo vikaanza kujirudia.
  Baadhi ya wenye magari wamefunga barabara ya kutoka Samunge na hivyo kuzuia gari la kubeba wagonjwa kwenda kusaidia wagonjwa mahututi.

  Shirika la PSI latinga Samunge
  Maofisa wa Shirika la Kimataifa la PSI, wamejitokeza Samunge na kuanza kuhamasisha jamii kujikinga na magonjwa ya mlipuko na Malaria na Ukimwi.
  Ofisa wa Uhamasishaji wa PSI maeneo ya vijijini mikoa ya Arusha na Manyara, Erasmus Majura, alisema wameamua kuweka kambi Samunge kutokana na ongezeko la watu katika eneo hilo ili kulinda afya.
  "Tunatoa elimu ya matumizi ya maji safi na kutoa dawa, tunatoa elimu ya Ukimwi na Malaria na pia tunaonyesha sinema usiku" alisema Majura.
   
Loading...