Babu Loliondo awaonya wanaomuiga

Babu Loliondo awaonya wanaomuiga

Hofu ya vifo yatanda kwa Babu


na David Frank, Arusha


amka2.gif
HOFU ya kutokea kwa vifo tena katika kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro imeanza kupanda baada ya ongezeka la idadi ya watu na wagonjwa kwa kile kilichoelezwa hali hiyo imetokana na kituo cha Bunda kulegeza masharti.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wadau wa habari zimeeleza kituo cha Bunda kiliwaachia watu na wagonjwa wengi kupita bila udhibiti wowote tangu Alhamisi iliyopita na kusababisha msongamano mkubwa katika kijiji cha Samunge huku msururu wa magari ukifikia kijiji cha Yandito.
Hazi hizo zimeeleza kutokana na msongamano uliyopo, ni wazi vifo vinaweza kutokea katika eneo hilo kwani hakuna uwezekano wa mgonjwa kupata tiba ndani ya siku mbili huku uhaba wa chakula na uchafuzi wa mazingira ukiendelea kuongezeka.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo huku akiwatahadharisha wagonjwa ambao hawajaanza safari kusitisha mara moja, kwani watakachokipata huko ni mateso ya siku zaidi ya mbili badala ya kusubiri wakiwa katika miji kunakopatikana huduma zote muhimu.
"Hali si shwari, Bunda wanadai wamelegeza masharti eti wamechoka kulaumiwa, sasa hali huku ni mbaya yawezekana kutokea tena kwa maafa na matatizo mengine makubwa …ni vizuri wale ambao hawajaanza safari wasitishe kwanza na sisi tumesimamisha safari kwa vituo vya Arusha na Babati kusubiri hali iwe nzuri," alisema Lali.
Aidha, baadhi ya watu waliozungumzia hali hiyo wameutoa shutuma zao kwa viongozi wanaosimamia kituo cha Bunda na kudai iwapo hali hiyo itaendelea basi vifo visivyotarajiwa vitatokea na tiba hiyo itakuwa katika mashaka.
"Naamini iwapo taratibu zitafuatwa hakuna tena wasiwasi wala mashaka juu ya tiba ya mchungaji huyo…vipi tena watu wa Kanda ya Ziwa wavunje utaratibu uliokuwa na manufaaa kwa jamii yote?" alihoji Jonathan Humbe, mkazi wa Arusha.
Naye Sitta Tumma, anaripoti kutoka Mwanza kuwa tabibu mwingine ameibuka jijini Mwanza ambaye anadai anatibu magonjwa mbalimbali sugu ukiwemo ukimwi, ugonjwa wa akili (vichaa), kisukari na kupooza mwili.
Mganga huyo, Muhangwa Kapeji maarufu kwa jina la Babu wa ‘Glasi' anadai kutibu magonjwa mengine kadhaa na kwamba wagonjwa anaowatibu anawapatia glasi moja ya dawa iliyochemshwa, na baada ya siku 15 mgonjwa anatakiwa anywe tena dawa ya unga atakayopewa na kisha atakuwa amepona.
Akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwake katika Kijiji cha Mwamilolelwa, Kata ya Bugogwa, Kapeji alisema tiba anayoitoa ni sawa na ile ya Babu wa Loliondo, na tayari ameshawatibu maelfu ya wagonjwa wakiwemo wagonjwa watano waliokuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kapeji alisema anatumia miti miwili ambayo ni Ntundwa na Mpandayonzo au kwa jina jingine Mg'holu, ambapo amekuwa akichimba mizizi yake kisha kuichemsha na kuwapa wagonjwa kisha kupona maradhi yao ndani ya muda mfupi, na kati ya miti hiyo, mti wa Mg'holu haupatikani sehemu nyingine mkoani Mwanza, bali unapatikana katika Wilaya ya Sengerema pekee.
"Kazi hii ya kutibu na kuponya wagonjwa nina miaka 20 sasa...watu wengi wanakuja kupata glasi wakiwemo wagonjwa wa ukimwi na wanapona hadi leo wako salama! Wapo wagonjwa wameletwa hapa wamepooza miguu na mwili wote, vichaa, kisukari lakini wakipata glasi moja wanapona.
Awali, mwenyekiti wa taasisi ya utafiti wa dawa za asilia nchini Medicinac-Plant Foundation (TMF), Gonzaga Ndege, alisema utafiti walioufanya unaonyesha tiba inayotolewa na mganga Kapeji imekuwa ikiwaponya wagonjwa, hivyo wanatarajia kuchukua sampuli ya dawa na miti inayotumiwa kwa ajili ya kuipeleka hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
 
Babu wa Loliondo kupumzika siku kuu

Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 18th April 2011 @ 23:35 Imesomwa na watu: 75; Jumla ya maoni: 0








MCHUNGAJI mstaafu wa kijiji cha Samunge, Ambilikile Mwaisapile atasitisha huduma Ijumaa Kuu na Pasaka kutokana na siku hizo kuwa ni muhimu ya kukumbuka mateso ya Bwana Yesu Kristo kwa waumini wa dini ya kikristo nchini.

Aidha, watu wanaotoka Kanda ya Ziwa kwenda kunywa kikombe kwa Mchungaji huyo wametakiwa kufuata utaratibu uliowekwa ili kuondokana na kero zinazowakumba watu hao na magonjwa ya milipuko na vifo kwani hali iliyoko hivi sasa inatisha kutokana na msongamano wa watu na foleni kufikia kilometa 25.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidore Shirima amethibitisha uamuzi huo wa Mchungaji.


Pia aliwasihi watu wa Kanda ya Ziwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa kila njia kutoa watu 500 lakini pamoja na hilo, haikusadia kwa watu wanaotoka Kanda hiyo kamatiiliyoundwa kushughulikia mambo ya foleni kwa Babu inaangalia njia yenye watu pungufu na

kuwaongeza watu wa Kanda hiyo hadi 1,000 pale inapobidi ili waende kunywa dawa.

"Tunajitahidi kupunguza msongamano kule kwa Mchungaji, lakini watu wa Kanda ya Ziwa hawaelewi, tunasisitiza kwenda kule na kukaa foleni si tija na mnakiuka utaratibu uliowekwa; fuateni utaratibu hatutaki watu wafe kule wala msipeleke wagonjwa mahututi kwani kule si Hospitali ya Rufaa, fuateni utaratibu mtahudumiwa".


Aidha, alisema tatizo watu wanalazimisha kwenda kwa Mchungaji lakini kulazimisha kwenda si busara ni ukiukaji wa masharti yaliyotolewa aliwataka na wenye magari kuacha tabia ya kuendesha kwa mwendokasi na kusababisha ajali.


Akizungumzia usalama wakati wa Pasaka, Shirima aliwasihi wananchi kuacha kwenda kwenye matembezi na familia zao bila kuacha waangalizi wa nyumba zao kwani wezi hawana muamana na kuongeza kuwa Polisi wataimarisha ulinzi nyakati za sikukuu na siku nyingine ili Arusha iwe salama.


Aliwasihi wafanyabiashara kuuza sukari kwa bei ya Sh 1,700 na si vinginevyo na kutoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa endapo watauziwa sukari kwa bei zaidi ya Sh 1,700 iliyotangazwa na serikali , na kuwataka wakulima kutumia mvua inayonyesha kwa kupanda mazao ya muda mfupi yanayokwenda na mvua inayonyesha na si kupanda mazao ya muda mrefu yatakayosababisha wakulima hao kutopata mazao kwa wakati.

 
Nimeipenda hii nukuu ya babu hapo juu: “Wananchi wajihadhari na watu wa sehemu nyingine wanaodai wameoteshwa na Mungu na kutoa tiba ya kikombe, ni matapeli tena wauaji.”!!!!!!!!!!!!
 
Mgogoro mpya wa mapato Samunge baina ya wilaya Send to a friend Thursday, 21 April 2011 08:52

Mussa Juma, Samunge
MGOGORO mpya wa mapato ya ushuru wa magari na helkopta zinazokwenda Samunge kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila, umeibuka baada ya kubainika kuwa, baadhi ya vituo vilipangwa kupewa mgao wa Sh3,000, havijawahi kupata mgawo huo.

Sh3,000 zinatakiwa kugawanywa sawa kwa vituo vitatu vinavyoratibu safari za Samunge. Vituo hivyo ni Bunda, Babati na Arusha.

Akizungumza na Mwananchi kijijini Samunge jana, Katibu Tawala Wilaya ya Bunda, Selevine Lalika, alisema tangu waanzishe kutuo cha kuratibu magari hawajawahi kutumiwa mgao wa Sh1,000 wanaostahili kupata.

Kwa sasa Kituo cha Bunda ndicho kinachoongoza kwa idadi kubwa ya magari yanayokwenda Samunge,
"Hali ni ngumu kituoni kwetu, tulikubaliana ushuru wa magari yanayofika Samunge, tupewe mgao ili kusaidia uratibu wa magari, kulipa posho za polisi, kujenga hema na hata kuwa na wauguzi, lakini tunashindwa kutokana na ukata," alisema Lalika.

Lalika alisema hivi sasa kazi ya kudhibiti magari yanayoelekea Samunge, imekuwa shida hasa kutokana na kukosekana fedha za uratibu ambazo zilipangwa kwenye kikao cha wakuu wa mikoa sita inayopakana na Arusha, kikao hicho kilisimamiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
"Bunda tunapokea magari ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na magari toka nchi za Kenya, DRC, Rwanda na Burundi, hivyo tulitarajia fedha hizo zingesaidia lakini hatujapata," alisema Lalika.

Aliomba uongozi wa Halmashauri ya Ngorongoro na wilaya, kutoa fedha katika kituo chao ili waweze kuendelea vizuri na kazi ya uratibu wa magari.

Kuhusu kuongezeka kwa magari yanayopitia lango la Wilaya ya Bunda, Lalika alisema inatokana na kuamua kupitisha watu kati ya 1,000 na 1,500 kwa siku, ili kupunguza msongamano uliokuwapo.
Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Ngorongoro, Dominick Lusasi, alipotakiwa kuelezea malalamiko hayo, alisema yupo jijini Dar es salaam kikazi.

Mgogoro huu wa sasa unaibuka takriban wiki moja tangu kumalizika kwa mgogoro mwingine wa mapato ya magari baina ya Halmashauri ya Ngorongoro na Kijiji cha Samunge, baada ya kijiji kuzuiwa kukusanya ushuru wa Sh2,000 na kazi hiyo kufanywa na halmashauri kwa kukusanya Sh5,000.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, aliingilia kati na kukutana na wajumbe wa serikali ya kijiji na kuamua kuwarejesha wakusanya ushuru wa kijiji ili washirikiane na wale wa halmashauri kukusanya Sh5,000.

Wageni zaidi watua Samunge
Raia zaidi kutoka Kenya jana waliendelea kufika Samunge kupata kikombe cha Mchungaji Mwasapila wakiwamo polisi wa nchi hiyo na familia zao.

Idadi kubwa ya wageni kutoka nje, ni raia wa Kenya ambao wamekuwa wakiingia Samunge na mabasi makubwa na madogo na wengine wakifika kwa kutumia usafiri wa helkopta na ndege.
Maofisa uhamiaji waliopo Samunge, wamekuwa na kazi kubwa ya kuorodhesha raia hao.

Foleni yapungua Samunge
Kutokana na serikali kusitisha kuruhusu magari kufika Samunge hadi baada ya sikukuu ya Pasaka, foleni ya magari imeanza kupungua na sasa ipo takriban kilomita tatu kutoka nyumbani kwa Mchungaji Mwasapila.
Baadhi ya abiria wa magari hayo, jana walikuwa wametimiza siku nne wakiwa kwenye foleni kabla ya kupata kikombe cha tiba.

Joyce Mwakitelima, mkazi wa Mbeya, alisema aliingia kwenye foleni hiyo tangu Jumapili iliyopita na jana alikuwa amekaribia kupata kikombe cha dawa.
 
Babu Loliondo afiwa na mwanaye Send to a friend Monday, 25 April 2011 23:55

afiwa.jpg
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ngorongoro, wakiwa nyumbani kwa mchungaji Ambilikile Mwasapila (kushoto), wakimpa pole kutokana na kifo cha Jackson Mwasapila(43), kilichotokea katika hopitali ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara jana. Picha na mussa juma

Mussa Juma, Samunge
MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge, Loliondo amefiwa na mtoto wake wa kiume jana. Kutokana na msiba huo, Serikali imesitisha tena tiba anayotoa hadi Ijumaa.

Habari zilizopatikana kijijini hapo jana zimeeleza kuwa mtoto huyo, Jackson Mwasapila (43), alifariki dunia jana asubuhi, nyumbani kwake wilayani Babati, Mkoa wa Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali aliliambia gazeti hili jana kuwa kutokana na msiba huo, Mchungaji Mwasapila atasitisha tiba kuanzia leo jioni.Mkuu huyo wa Wilaya alifika Samunge jana hiyo hiyo akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, kumpa pole mchungaji huyo.

"Tunapenda kutangaza rasmi kuwa huduma zitasitishwa hadi Ijumaa na tunaomba watu walio mbali wasije hadi Ijumaa," alisema Lali.Alisema Serikali itashiriki msiba huo na inajiandaa kutoa msaada wa kumpeleka Mchungaji Mwasapila, Babati kushiriki msiba huo.

Mchungaji azungumziakilichomsibu mwanaye
Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo jana, Mchungaji Mwasapila alisema mtoto wake huyo alifariki jana saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Babati baada ya kuugua malaria ghafla.

"Taarifa ambazo nimezipata ni kuwa Jackson alikuwa anasumbuliwa na kichwa na baada ya kufikishwa hospitali, alifariki dunia," alisema Mchungaji Mwasapila.Mchungaji huyo, alisema Jackson ni mtoto wake wa tatu kati ya sita alionao.

Wagonjwa wampa pole
Baadhi ya wagonjwa waliokwenda Samunge jana kupata tiba, walitoa salamu za rambirambi kwa Mchungaji Mwasapila kutokana na msiba huo.Hata hivyo, wakati wagonjwa hao wakimpa pole, mchungaji huyo alikuwa akiendelea kuwapa dawa kama kawaida.

Mchungaji Mwasapila alisema ameamua kuendelea na kutoa tiba kwa wagonjwa hao ili kuwasaidia watu ambao tayari walikuwa wamefika Samunge na wengine watakaofika leo.

"Kesho (leo) jioni nitafunga na kuelekea Babati kwa ajili ya msiba wa mtoto wangu na kama alivyosema mkuu wa wilaya, tutaendelea na tiba Ijumaa," alisema Mchungaji Mwasapila.

Foleni yapungua Samunge
Katika hatua nyingine, msongamano wa magari yaliyoanza kwenda kijijini hapo baada ya Pasaka umeanza kupungua. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mengi ya magari hayo, yalikuwa yamebeba wagonjwa kutoka Kenya.

Serikali ilishafungua vizuizi vya Bunda, Mto wa Mbu, Londigo na Loliondo mjini vilivyokuwa vimefungwa kwa muda wakati wa sherehe za Pasaka.
 
Naibu Spika atua Samunge kupata kikombe cha tiba Send to a friend Monday, 25 April 2011 10:15

Mussa Juma, Samunge
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai juzi alikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliokuwepo Samunge kupata kikombe cha tiba kwa Mchungaji, Ambilikile Mwasapila.

Ndugai alifika Samunge akiwa na Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli pamoja na maofisa wengine wa kadhaa wa Serikali.

Baada ya kufika Ndugai na ujumbe wake, walipokewa na msaidizi wa Nchungaji Mwasapila, Frederick Nisajile na baadaye kupata kikombe cha tiba.

Katika hatua nyingine, juzi kwa mara ya kwanza tangu aanze kutoa tiba hiyo, Mchungaji Mwasapila hakuwa na wagonjwa waliokuwa Samunge kupata tiba. hali hiyo ilimfanya aiombe Serikali kuruhusu magari yaliyo katika vizuizi vya Mto wa Mbu, Arusha na Bunda mkoani Mara yaruhusiwe kwenda leo badala ya kesho kama ilivyokuwa imetangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima.

Nisajile alisema dawa iliyokuwa imetayarishwa ni nyingi hivyo akatoa wito kuwa ni vyema magari mengine yakaruhusiwa ili iweze kutumika yote.

"Kama unavyoona hakuna magari leo (jana) hivyo tunaomba waruhusiwe kuja ili wapate tiba bila kusubiri msongamano," alisema Nisajile.

Hadi jana mchana ni magari sita tu ambayo yaliingia Samunge kwa njia za panya.

Wakati mchungaji Mwasapila akiomba Serikali iruhusu magari, madereva wa magari yanayopeleka wagonjwa huko juzi waliandamana wakilalamikia usumbufu uliopo kwenye vizuizi.

Maandamano hayo, yaliishia katika Ofisi ya Kijiji cha Samunge na kupokewa na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Michael Lengume ambaye alifanya nao mazungumzo.

Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo, Lengume alisema wamekubaliana kuongeza mgambo katika vizuizi ambao watalipwa na madereva hao.

"Madereva wamelalamikia usumbufu kwenye vizuizi na wameomba tutoe mgambo zaidi ambao wao watakuwa wakiwalipa Sh1,000 kila mmoja kama gharama za ulinzi," alisema Lengume.

Kwa upande mwingine, Polisi wilayani Ngorongoro, wameimarisha ulinzi katika maeneo ya Vijiji vya Samunge na Digodigo ili kudhibiti uvunjifu wa amani kutokana na ongezeko la watu.

Gazeti hili lilishuhudia polisi hao wakiwa katika doria Kijiji cha Samunge.
 
Hiv huyo babu ni mtumish wa Mungu aliye hai wa BWANA Yesu kristo, au ni mganga wa kienyeji kama wengine? Ee sianatumia dawa za kienyeji!! Na PM Pinda kasema lazima awe na kibali kama cha akina Mwandulami wa Njombe. Acha awaponye watu kwa mzizi!! Lakini wakifa wote ni motoni kwani hawana ondoleo la dhambi. Marko16:16-- Kwanini mnamsifia wakati hahubiri injili? Maana ndiyo msingi wa uponyaji wa MUNGU aliye hai(Marko16:20) Hiyo inaitwa nguvu ya upotevu (2Wathes2:1-12) Watz weng hawaipend kwl ya maneno tu namtu anapona kwa jina la YESU!! Mpaka wapewe mzizi ama kitu fulani (hilizi) ndiyo wanaamin. Ndiyo maana Mungu ameachia nguvu ya upotevu wapate kupotea kwa kuwa hawakuiamini kweli. Jambo jingine ujue ndizo dalili za mwisho! Huwezi kuzuia dalili isitokee. Unaweza kuzuia mawingu ya mvua yasitande ili mvua isinyeshe (Mathay24:24,32-39. Lakini ktk 2Timoth3:1,8-9. Mwisho wa babu hauko mbali. Na wote wanaomtegemea, wamelaniwa. (Yerem17:5
 
Hiv huyo babu ni mtumish wa Mungu aliye hai wa BWANA Yesu kristo, au ni mganga wa kienyeji kama wengine? Ee sianatumia dawa za kienyeji!! Na PM Pinda kasema lazima awe na kibali kama cha akina Mwandulami wa Njombe. Acha awaponye watu kwa mzizi!! Lakini wakifa wote ni motoni kwani hawana ondoleo la dhambi. Marko16:16-- Kwanini mnamsifia wakati hahubiri injili? Maana ndiyo msingi wa uponyaji wa MUNGU aliye hai(Marko16:20) Hiyo inaitwa nguvu ya upotevu (2Wathes2:1-12) Watz weng hawaipend kwl ya maneno tu namtu anapona kwa jina la YESU!! Mpaka wapewe mzizi ama kitu fulani (hilizi) ndiyo wanaamin. Ndiyo maana Mungu ameachia nguvu ya upotevu wapate kupotea kwa kuwa hawakuiamini kweli. Jambo jingine ujue ndizo dalili za mwisho! Huwezi kuzuia dalili isitokee. Unaweza kuzuia mawingu ya mvua yasitande ili mvua isinyeshe? (Mathay24:24,32-39. Lakini ktk 2Timoth3:1,8-9. Mwisho wa babu hauko mbali. Na wote wanaomtegemea, wamelaniwa. (Yerem17:5
 
Hiv huyo babu ni mtumish wa Mungu aliye hai wa BWANA Yesu kristo, au ni mganga wa kienyeji kama wengine? Ee sianatumia dawa za kienyeji!! Na PM Pinda kasema lazima awe na kibali kama cha akina Mwandulami wa Njombe. Acha awaponye watu kwa mzizi!! Lakini wakifa wote ni motoni kwani hawana ondoleo la dhambi. Marko16:16-- Kwanini mnamsifia wakati hahubiri injili? Maana ndiyo msingi wa uponyaji wa MUNGU aliye hai(Marko16:20) Hiyo inaitwa nguvu ya upotevu (2Wathes2:1-12) Watz weng hawaipend kwl ya maneno tu namtu anapona kwa jina la YESU!! Mpaka wapewe mzizi ama kitu fulani (hilizi) ndiyo wanaamin. Ndiyo maana Mungu ameachia nguvu ya upotevu wapate kupotea kwa kuwa hawakuiamini kweli. Jambo jingine ujue ndizo dalili za mwisho! Huwezi kuzuia dalili isitokee. Unaweza kuzuia mawingu ya mvua yasitande ili mvua isinyeshe? (Mathay24:24,32-39. Lakini ktk 2Timoth3:1,8-9. Mwisho wa babu hauko mbali. Na wote wanaomtegemea, wamelaniwa. (Yerem17:5

Hongera Katabu kwa kuuweka wazi ukweli huu. Babu na wagawa vikombe wengine wote ni kazi za shetani. Mungu wa kweli haponyi kwa mizizi, ila kwa neno lake tu. Miujiza ya Mungu wa kweli ni lazima iambatane ka kuhubiri Injili ya Yesu watu wamgeukie Mungu. Tukumbuke lengo kuu la Mungu ni watu wamjue ili waweze kufika kwake, sio wapone tu miili halafu waendelee na maisha yao ya dhambi na mwishoni watupwe motoni
 
Hongera Katabu kwa kuuweka wazi ukweli huu. Babu na wagawa vikombe wengine wote ni kazi za shetani. Mungu wa kweli haponyi kwa mizizi, ila kwa neno lake tu. Miujiza ya Mungu wa kweli ni lazima iambatane ka kuhubiri Injili ya Yesu watu wamgeukie Mungu. Tukumbuke lengo kuu la Mungu ni watu wamjue ili waweze kufika kwake, sio wapone tu miili halafu waendelee na maisha yao ya dhambi na mwishoni watupwe motoni

Ni kweli Ng'wandu. Wanaoisapot hiyo tiba ya babu walio wengi hata kuokoka bado. Wengi wao ni watu wa dini zao. Hawaamini wokovu wa BWANA Yesu kristo (Luka1:77, Mark16:16) Jaribu kufuatilia maisha ya mtu anayeisapot hiyo tiba, je ameokoka? Utakuta wengi ni wahuni tu wakawaiada na babu wao. Eti ni Mchungaji!! Kwani hakuna wachungaji na maaskofu wanaopinga wokovu hadharani? Kuwa hakuna kuokoka duniani. Wakati huohuo wanamwita Yesu MWOKOZI. Sasa nini kazi ya mwokozi? Jibu ni kuokoa.
 
Nimeipenda hii nukuu ya babu hapo juu: ¡°Wananchi wajihadhari na watu wa sehemu nyingine wanaodai wameoteshwa na Mungu na kutoa tiba ya kikombe, ni matapeli tena wauaji.¡±!!!!!!!!!!!!

nadhani yeye ndio kiongozi wao, ndia alieanza kuleta huu utapeli wa kiimani. So awachie na wenziwe wagange njaa. Hana lolote asibabaishe watu.
 
Back
Top Bottom