Baba wa taifa kutangazwa mwenye heri, wakatoliki hili limekaaje?

Kuhusu Paulo nishajibu jibu lake linamhusu hata Petro pia pitia uzi mzima kabla hujajibu.
Lakini nikijibu hoja ya kwenda mbinguni ni sawa kwa kila mkombolewa lakini je kila anayekwenda mbinguni tunamtangaza mwenye heri na kumuomba atuombee? na je wasiotangazwa wenye heri hawajafika mbinguni kwa mujibu wa maelezo yako?
una jina zuri laini hujui matumizi yake!
 
Swadaktaaa!Enhee...alimuua nani hebu tutanabaishie ndugu shuhuda ili basi tupate ufahamu!?
Kuna bwana mmoja alikuwa anaghasiwa na mkuu wa mkoa katika harakati za siasa za ujamaa kwa maana huyo bwana alikuwa na mashamba makubwa ambayo kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa alikuwa anaonekana bwana yule ni bepari, basi jumapili moja akumfuata shambani kwake na kumfanyia kama mkuu mmoja aliyevamia kituo cha tv hapa Dar, basi bwana yule akamtwanga gobole ndugu mkuu akaaga ulimwengu, kisha bwana yule akafikishwa kunako koti na kuhukumiwa kifo, basi baba akatia saini bwana yule akanyongwa.
Nadhani kwakuwa umekaa na shangazi kwa miaka 25 utakumbuka vizuri sasa.
 
Alisign death sentence kibao. Japo alikuwa abauwwzo wa kuwaacha wakatumikia kifungo cha maisha.
Sheria inazungumzaje juu ya mtu aliyeua kwa makusudi na kukiri au ushahidi kumuweka hatiani?Unaweza ukajidai unahisi machungu mengi juu ya mzee Mwamindi,je upande wa akina Klerruu umewahi kuhisi hisia zao?Mwana wa mwenzio si mbwa "ndaa" ni mtu vilevile!
 
Kuhusu shangazi yako sijabisha.Kwani mtu akikutusi adhabu yake ni kumuua palepale?Hakuna vyombo vya kisheria kukupa haki?
 
Walihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia. Mwlimu alikuwa mkotoliki safi na mcha Mungu, kwa mamlaka aliyokuwa nayo alikuwa na uwezo wa kutosign jamaa kunyongwa na akawaacha wakafia gerezani.

Kumbuka haki ya kwanza ya mtu ni kuishi. Unapotoa mtu uhai ni kumyanganya haki yake ya kuishi. Kuna taarifa enzi zake Mwalomu alisign vifo zaidi ya 125.
 
Sasa unataka kumuhukumu mwalimu kwa kusaini kwake hati ya kifo badala ya ninyi kina gitogito mngemnasihi mwamuhehe Mwamwindi kuepuka hasira za e-kihehe?Binadamu tusiwe na visingizio kkwa makosa yetu kwa kusingizia matokeo hasi ya.mnachofanya.Kila kazi ina ujira wake.
 
Dini is for Stupids....

Yaani grupu la watu wazinzi ,waasherati na wazandiki kama mimi wanakaa kwenye meza wanapiga kura eti fulani awe "mtakatifu"..

Mbwa kasoro mikia kabisa...
Umetumia maneno makali ili uoneshe fikra zako.Jambo moja ni kuwa umewakusanya woootee kwa kadiri ya fikra zako.Unataka kuwaaminisha wanaokuunga mkono kuwa wote hao ni wadhambi?Tafakari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…