Baba wa Mtoto Aliyefufuka Apigwa Mkwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba wa Mtoto Aliyefufuka Apigwa Mkwara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Feb 15, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,989
  Likes Received: 37,283
  Trophy Points: 280
  WAFANYABISHARA wanne wa mbao wilayani Mufindi, mkoani Iringa, wanadaiwa kutaka kumpa Sh4 milioni , baba mzazi wa Nikson Kabonge, aliyeibuka akiwa hai wiki mbili zilizopita, baada ya kudaiwa alikuwa amekufa, ili amkatae mtoto wake.

  Akizungumza na Mwananchi, mzee Boniface Kabonge, alisema wafanyabiashara hao walifika nyumbani kwake wiki iliyopita na kumbembeleza amkane mtoto huyo, jambo ambalo hakulikubali.

  Alisema hawezi kumkana mtoto huyo kwa sababu ana uhakika kuwa Nikson ni mwanaye japo kaburi lake bado halijafukuliwa, ili kubaini nani aliyezikwa ikiwa inadaiwa kuwa alichanganya maiti.

  "Walikuja wanataka nipokee fedha zao ili nimkatae mwanangu kuwa simjui. Siwezi kukubali hela zao wala kumkataa mwanangu hata kama wangenihonga milioni kumi, hii ni damu yangu,"alisema.

  Alisema tangu kijana huyo arudi nyumbani kwake, amekuwa akisumbuliwa na wafanyabisara hao wa mbao wakitaka akanushe kuwepo kwa kijana wake kwa madai ya kuhatarisha biashara zao jambo ambalo linampa wasi wasi.

  "Siwezi kuwataja majina yao lakini nawatambua, ila kama wataendelea kunisumbua nitawataja kwani huenda wanahusika kwa njia moja au nyingine katika tukio hili, kwanini watake nimkane mwanangu. Msimamo wangu kwa mwanangu upo pale pale," alisema.

  Alisema jeshi la polisi linataarifa hiyo na kuomba jeshi hilo kutoa taarifa za wapi na nani alikuwa akiishi na Niksona kwa kipindi cha miezi minne iliyopita na ambayo watu walijua kuwa alikuwa amekufa na kuzikwa.

  Mzee huyo alisema madai kuwa majirani, ndugu na jamaa walikosea kuutambua mwili, hayana msingi.

  Kwa upande wake, Nikson Kabonge alisema anajisikia vibaya kuona wafanyabishara wa mbao wakitaka baba yake amkane na kuwa huenda wanataka kumrejesha kwenye msitu wa Kihanga, alikokuwa akifanyishwa kazi za mbao bila kupumzika.

  Alisema kutokana na hali hiyo, ameamua kuokoka na kuwa karibu na Mchungaji wa Kanisa la Pentekosti, ili kunusuru uhai wake.

  "Kwa sasa haniwezi mtu kwa sababu nimeokoka na muda mwingi nakuwa na mchungaji niyanusuru maisha yangu, wanataka baba anikatae kwani inawahusu nini,?" alisema.
  Bado kaburi la kijana huyo halijafukuliwa licha ya wananchi kuomba lifukuliwe, ili wajue nani alizikwa na Nikson ambaye ameibuka hai alikuwa wapi.

  source: mwananchi
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hivi Watanzania hatuwezi kufanikiwa kwenye biashara zetu bila kutumia uchawi?
  Zamani hii ilikuwa maarufuku sana mikoa ya Mbeya,lringa na kanda ya kusini magharibi.
  Lakini leo hii ili ufanikiwe kibiashara ni lazima uchawi uhusishwe, hii sasa imekuwa ni Tanzania nzima.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Ndo maana maendeleo kwetu kupatikana ni issue kubwa sana
  kwa hali hii!!
   
 4. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 974
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Lakini Serikali inasema nini juu ya utata huu? kwanini hawataki kuchunguza na kulitolea maelezo?
   
 5. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  mmmh uncle mbn inatisha?mil 4?inasaidia nn,so amkane zen?hata sielewi mm
   
 6. N

  Nanu JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Swali langu ni hili kwanini serikali wanakaa kimya kuhusu hili? Mpaka leo hii kwanini kaburi halijafukuliwa na DNA kufanyika kubaini ni mtu gani huyo aliyezikwa? nadhani hili jambo ni zito sana na linatakiwa lifanyiwe uchunguzi kwa uzito unaotakubalika. Aliyezikwa ni mtu na aliyedhaniwa ndiyo amezikwa yuko hai maana yake aliyezikwa ni mtu mwingine ambaye wazazi au ndugu zake wanajua bado yupo hai. Maisha ya mtu yeyote awaye yote ni "priority for any government which cares for her people" Tunataka tupate tamko au ripoti ya serikali kuhusu hili!
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,989
  Likes Received: 37,283
  Trophy Points: 280
  hamna adui mkubwa kama umasikini wa fikra.
  Bora uwe masikini wa kipato kuliko kuwa masikini wa fikra.
  Thkukuu ilikuwaje?
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  lakini jambo moja sielewi...hivi ni kweli watu hawa hufufuka, baada ya kufa ama ni confussion za wahudumu wa mochwari ?
   
 9. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Ww mwenyewe ulisema utakuwa my valentine nakutumia msg hujibu na cm ukafunga!
   
 10. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145

  Uko nje ya mada..........Wagumu kuelewa wepesi wa kusahau...
   
 11. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Inaelekea asipomkana,utajiri wao wote tapotea!!
   
 12. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  ah ah ah it can be
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mmh makubwa haya.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...