Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,627
- 154,983
WAFANYABISHARA wanne wa mbao wilayani Mufindi, mkoani Iringa, wanadaiwa kutaka kumpa Sh4 milioni , baba mzazi wa Nikson Kabonge, aliyeibuka akiwa hai wiki mbili zilizopita, baada ya kudaiwa alikuwa amekufa, ili amkatae mtoto wake.
Akizungumza na Mwananchi, mzee Boniface Kabonge, alisema wafanyabiashara hao walifika nyumbani kwake wiki iliyopita na kumbembeleza amkane mtoto huyo, jambo ambalo hakulikubali.
Alisema hawezi kumkana mtoto huyo kwa sababu ana uhakika kuwa Nikson ni mwanaye japo kaburi lake bado halijafukuliwa, ili kubaini nani aliyezikwa ikiwa inadaiwa kuwa alichanganya maiti.
"Walikuja wanataka nipokee fedha zao ili nimkatae mwanangu kuwa simjui. Siwezi kukubali hela zao wala kumkataa mwanangu hata kama wangenihonga milioni kumi, hii ni damu yangu,"alisema.
Alisema tangu kijana huyo arudi nyumbani kwake, amekuwa akisumbuliwa na wafanyabisara hao wa mbao wakitaka akanushe kuwepo kwa kijana wake kwa madai ya kuhatarisha biashara zao jambo ambalo linampa wasi wasi.
"Siwezi kuwataja majina yao lakini nawatambua, ila kama wataendelea kunisumbua nitawataja kwani huenda wanahusika kwa njia moja au nyingine katika tukio hili, kwanini watake nimkane mwanangu. Msimamo wangu kwa mwanangu upo pale pale," alisema.
Alisema jeshi la polisi linataarifa hiyo na kuomba jeshi hilo kutoa taarifa za wapi na nani alikuwa akiishi na Niksona kwa kipindi cha miezi minne iliyopita na ambayo watu walijua kuwa alikuwa amekufa na kuzikwa.
Mzee huyo alisema madai kuwa majirani, ndugu na jamaa walikosea kuutambua mwili, hayana msingi.
Kwa upande wake, Nikson Kabonge alisema anajisikia vibaya kuona wafanyabishara wa mbao wakitaka baba yake amkane na kuwa huenda wanataka kumrejesha kwenye msitu wa Kihanga, alikokuwa akifanyishwa kazi za mbao bila kupumzika.
Alisema kutokana na hali hiyo, ameamua kuokoka na kuwa karibu na Mchungaji wa Kanisa la Pentekosti, ili kunusuru uhai wake.
"Kwa sasa haniwezi mtu kwa sababu nimeokoka na muda mwingi nakuwa na mchungaji niyanusuru maisha yangu, wanataka baba anikatae kwani inawahusu nini,?" alisema.
Bado kaburi la kijana huyo halijafukuliwa licha ya wananchi kuomba lifukuliwe, ili wajue nani alizikwa na Nikson ambaye ameibuka hai alikuwa wapi.
source: mwananchi