Basi tukarudi Karibu na baiskeli na mbao tukakita wale simba wamesimama tu wakituangalia! Kumbe wale simba walikua wanaogopa kusonga mbele wakiogopa vyuma vya baiskeli vinavyong'aa ya Ile sterling!
Basi tukaamua kuacha baiskeli Na mbao Hapo tukaanza Kukimbia kinyumenyume huku tukiwaangalia hao simba Maana ukiwapa mgongo ni Hatari sn!
Wale simba wakaanza kutufata, na walipokaribia baiskeli wakaikwepa wakapita pembeni then wakarudi njiani kutufukuza!
Tulikimbia sn Siku Hiyo Karibu Dakika 20 ivi huku tunawarushia zile fimbo!