Baba Nakupenda

Baba Nakupenda

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,430
Umetoka shule kwa likizo. Umefika nyumbani unamkuta mama, unamuuliza mama, baba yuko wapi anakujibu yuko kazini.

Muda mwingi uko na mama ako tu. Ni siku ya Jumapili, baba anaingia chumbani kwako anakukuta ukipanga mabegi kwani kesho unarudi shuleni (likizo imeisha) anakupatia laki 8 za ada.

Ile anataka kuondoka, unamuomba laki moja ya matumizi. Anakwambia "hali ni ngumu mwanangu" ila anakupatia elfu 80, kisha anaondoka.

Unatoka chumbani kwako ukiwa umenuna, unaenda sitting room, unamkuta mama. Mama anakuuliza "mbona umenuna", unamjibu, "baba
amenipa elfu 80 badala laki kwa matumizi". Mama anafungua hand bag, anakupa elfu 30.

Wewe kwa akili yako mbovu, unakimbilia simu, unaingia FB unapost "HAKUNA KAMA MAMA". Umesahau kwamba baba yako leo ameenda kazini kwa mguu kwa sababu hana nauli? Umesahau kwamba jasho lake ndilo linalokuweka shule? Umesahau kwamba, hela aliyokupa mama kapewa na baba?

ACHA UBAGUZI WA WAZAZI!

Wazazi wote ni sawa ndugu. Kama umezoea kupost 'hakuna kama Mama", leo comment hapa chini "BABA NAKUPENDA SANA" Niwatakie siku njema ndugu zangu.

Mulanga Michael mwakibete
 
Na ambao baba zetu walitukataa na hawakujali hata tulikua tukilala njaa na kuvaa chupi zenye matobo na wao wanakula bata mjini tunacoment neno gani
Sijawahi kumpenda na sitompenda japo simchukii ila sitaki ukaribu nae maana alinambia kwa kinywa chake nisitumie hata ubini wake ila leo ananitafuta eti nimpe matumizi
Nampa kama navoweza kuwapa ombaomba ila si kwa heahima ya ubaba
Nakupenda mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Sasa Kali!.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetoka shule kwa likizo. Umefika nyumbani
unamkuta mama, unamuuliza mama, baba yuko
wapi anakujibu yuko kazini.
Mda mwingi uko na mama ako tu. Ni siku ya
juma pili, baba anaingia chumbani kwako
anakukuta ukipanga mabegi kwani kesho unarudi
shuleni (likizo imeisha) Anakupatia laki 8 za ada.
Ile anataka kuondoka, unamuomba laki moja ya
matumizi.
Anakwambia "hali ni ngumu mwanangu" ila
anakupatia elfu 80, kisha anaondoka.
Unatoka chumbani kwako ukiwa umenuna,
unaenda sitting room, unamkuta mama. Mama
anakuuliza "mbona umenuna", unamjibu, "baba
amenipa elfu 80 badala laki kwa matumizi".
Mama anafungua hand bag, anakupa elfu 30.
Wewe kwa akiri yako mbovu, unakimbilia simu,
unaingia FB unapost "HAKUNA KAMA MAMA".
Umesahau kwamba baba yako leo ameenda
Kazini kwa mguu kwa sababu hana nauli?
Umesahau kwamba jasho lake ndilo linalokuweka
shule?
Umesahau kwamba, hela aliyokupa mama
kapewa na baba? ACHA UBAGUZI WA WAZAZI
Wazazi wote ni sawa ndugu.
Kama umezoea kupost 'hakuna kama Mama", leo
comment hapa chini
"BABA NAKUPENDA SANA"
Niwatakie siku njema ndugu zangu.

Mulanga Michael mwakibete
Alikuwa ananipenda sana hakuna ninachokosa ila RIP

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ambao baba zetu walitukataa na hawakujali hata tulikua tukilala njaa na kuvaa chupi zenye matobo na wao wanakula bata mjini tunacoment neno gani
Sijawahi kumpenda na sitompenda japo simchukii ila sitaki ukaribu nae maana alinambia kwa kinywa chake nisitumie hata ubini wake ila leo ananitafuta eti nimpe matumizi
Nampa kama navoweza kuwapa ombaomba ila si kwa heahima ya ubaba
Nakupenda mama

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakushauri kaa vizuri na mama yako kwa nini mshua alikuwa anakukutaa muuliZe,
Samahani lakini kwa kuwa umeshakuwa mkubwa mkonvice dingi mkacheki DNA inawezekana unamlaum bure mzee wa watu.
 
Pole mzee, msamehe tu
Na ambao baba zetu walitukataa na hawakujali hata tulikua tukilala njaa na kuvaa chupi zenye matobo na wao wanakula bata mjini tunacoment neno gani
Sijawahi kumpenda na sitompenda japo simchukii ila sitaki ukaribu nae maana alinambia kwa kinywa chake nisitumie hata ubini wake ila leo ananitafuta eti nimpe matumizi
Nampa kama navoweza kuwapa ombaomba ila si kwa heahima ya ubaba
Nakupenda mama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh, samahani kwa kuuliza, baba yako alisema hivyo kweli?
Yaani alikosa kabisa sababu nyingine ya kujitetea?
Ndio alichosema na alipata watoto wengine kwa mwanamke alieishi nae lakini wamekufa wote nimebaki mimi tu na ndio alipokuja kuniomba msamaha
Nikamuuliza kosa langu au alilokosa mama kwake akadai hajawahi kumkosea kwani alipompa mimba tu alikataa na kukimbia kijijini hapo hivyo hawezi ongopa na nakumbuka tumeishi kwa shida sana sana na nilikua natembea kwa miguu siku nzima kwenda mjini kuomba msaada kwake ila alinifukuza kama mara nne hivyo nikachoka
Baada ya kufiwa na watoto na mke wake akabaki mwenyewe na alipata matatizo ya kutokuona vizuri ndio akaanz kunitafuta na kuja kumuangukia mama na mm
Ila nikikumbuka naumia sana niishie hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom