Baba na mwanaye waoa mabinti mapacha

Baba na mwanaye waoa mabinti mapacha

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,834
Reaction score
7,724
Wahenga walisema dunia ina mengi na wengine walisema dunia imevaa koti.

Watu wawili ambao ni baba na mwanaye wameoa mabinti mapacha wilayani Kisarawe Pwani. Inadaiwa baba alilazimishwa kuoa akiwa kijana mdogo sana na baadae kumzaa mtoto wa kiume ambapo aliamua kumtelekeza mama kutokana na ugumu wa maisha.

Inadaiwa jamaa alihama kwao Kwenda kisarawe kutafuta maisha na baada ya mtoto wa kiume kukua aliamua kumsaka baba ambaye aliunganaye huko kisarawe na wakawa marafiki wakubwa na kuwa kama washikaji kiasi kwamba hata salamu hawaamkiani kiheshima bali kishikaji.

Inadaiwa waliishi wote geto na huongozana kila sehemu huku wakidanganya watu kuwa wao ni marafiki ilihali ni mtu na babake. Walifanikiwa kupata wapenzi ambao ni mapacha na kila mtu kuishi geto lake rasmi na kila mtu humuita mke wa mwenzie shemeji au shemela.

Baadae walioa rasmi na mke wa kijana hajapata ujauzito hadi leo na inadaiwa ni tasa ila baba kapata mtoto.

Kufichuka kwa siri kuwa wale ni baba na mwanaye kulifichuliwa na mtu aliyetoka huko kwao kuja kutafuta maisha wilayani kisarawe. Ufichuzi huu uliwaacha watu mdomo wazi.

Source: Radio One.
 
Ndio maana kuna zero nyingi sana huko.

Labda ndio sababu
 
Hii habari ni ya kutunga ili kurudisha nyuma juhudi za mkuu wa wilaya Kisarawe. Kamwe hawa wafuasi wa Bashite hawata fanikiwa kwani jamii imeshaona Kisarawe siyo mahala penye mambo ya hovyo ki hivyo. Big up DC wa Kisarawe tunaona mabadiliko ya maendeleo katika mwendo kasi ndio maana kuna wanaokupiga vita. Daima mbele Kisarawe juu juu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom