Baba na Mwana watatoka lini gerezani?

WanaJF,


Hivi ni kweli anayeua kwa upanga naye atakufa kwa upanga? Kama maneno haya ni kweli basi namwomba mwenyezi Mungu yatimie kwa wale wote wanaolihujumu taifa hili kwa kuwakandamiza wanyonge na kutumia mamlaka waliyonayo kupindisha sheria,kusingizia watu na kutengeneza matukio au kesi zisizo za kweli ili wapate kufungwa magerezani!

Wanamuziki ambao ni baba na mwana,Nguza Viking na Papii Kocha mpaka sasa wanatumikia vifungo vya maisha baada ya kusingiziwa kuwalawiti watoto wanafunzi wa shule ya msingi huko Sinza! Katika kesi ambayo kwa sasa inaonekana kusahaulika taratibu kama ilivyo kawaida yetu, mwanasheria maarufu nchini Mabere Marando aliweza kuwatoa katika kifungo cha maisha watoto wawili wa Nguza Viking waliokuwa wamefungwa gerezani pamoja na baba yao!

Mpaka sasa haijulikani ni nani aliyeshinikiza na kuitengeza kesi iliyopelekea familia ya Nguza Viking kupatwa na masaibu haya ya kufungwa maisha gerezani! Ni nani mtu huyu aliyefanya yote haya? Bila shaka atakuwa ni mtu asiye na huruma na hatari sana! Kuna utata mkubwa katika kesi hii kwani mwalimu aliyesemekana kuwa ndiye aliyekuwa akiwapeleka watoto wanafunzi kulawitiwa nyumbani kwa Nguza Viking aliachiwa huru kisha baadaye alihama shule na kwenda kusikojulikana!

YULE MWALIMU YUPO MAENEO YA KIMARA/MBEZI ANAKULA KUKU.

"hii avatar yako mbona inatisha sana"
 
Bado kuna mazingira ya giza kuhusu kesi yake ilivyoendeshwa na ushahidi ulivyotolewa, kwa hivyo bado haiondoi wasiwasi wa wengi tulionao kuwa kuna mkono wa mtu......! Katika mambo ambayo Rais ajaye ataweza kujionesha kuwa ni mtetezi wa haki ni kuondokana na wingu kama hili, ikiwemo kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa

Tena ni giza kuu linalohitaji nuru na busara toka mbinguni kwa atakayewatoa watu hawa na wengine wote waliofungwa kwa kusingiziwa! Nakumbuka kuna kipindi Mchungaji Mtikila alilivalia njuga swala hili lakini baadaye aligeuka ghafla na kuikandamiza familia hii ya Nguza Viking! Tuwaombee uzima ndugu zetu wote waliofungwa kwa kusingiziwa magerezani ili siku moja tujekuwa nao tena uraiani!
 
Mpaka leo najiuliza bila kupata jibu ni kwanini ule wimbo wa SALIMA haupigwi tena redio zote nchini! Na kama hamuamini ombeni huo wimbo upigiwe redioni kama mtapigiwa!
 
  • Thanks
Reactions: PSM
Mpaka aliye juu ya sheria atakapoondoka au kufa! "alisema naweza kuwa nimevaa tabasamu lakini nipo serious?"
 
Mpaka leo najiuliza bila kupata jibu ni kwanini ule wimbo wa SALIMA haupigwi tena redio zote nchini! Na kama hamuamini ombeni huo wimbo upigiwe redioni kama mtapigiwa!
Redio itakayopiga itafungiwa kwa uchochezi na kuhatarisha usalama wa nchi na kuingilia mambo ya ndani ya mkuu wa nchi na mkewe!
 
YULE MWALIMU YUPO MAENEO YA KIMARA/MBEZI ANAKULA KUKU.

"hii avatar yako mbona inatisha sana"
Inatisha nini? Tena uzuri umemsaidia hata kujua mahali alipo shahidi muhimu wa kesi hii. Mimi naomba unielekeze yupo sehemu gani au nisaidie contact zake nataka kufanya mahojiano na yeye bila kuhatarisha usalama wake. Sana sana usalama wangu ndio utakuwa hatarini lakini najitoa mhanga!
 
Nani kawadanganya kuwa akina Nguza walionewa?!Jaribuni kujiridhisha na kauli zenu kabla ya kupost bhana!
 
Kwa hiyo eeh Bwana, tunapokumbuka kifo na mateso ya huyo mwanao tunakutolea kikombe cha wakovu..... ili uweze kuwaokoa waonewao.. tunaomba haya kwa njia ya Kristo mwanao...............!

Eeeh Bwana sema neno moja tu,na roho za waliosingiziwa na kufungwa, waliong'olewa meno na kucha,waliomwagiwa tindikali,waliouawa na waonewao zitapona. Amina.
 
Ningefurahi kupata mchango wa kisheria je hawa jamaa wanaweza kutoka kwa taratibu za kisheria (sheria inasemaje isije tukawa tunaongea kwa huruma kwa kuwa hawa jamaa tunawafahamu) au mpaka msamaha wa rais ndiyo wanaweza kutoka
 
Ningefurahi kupata mchango wa kisheria je hawa jamaa wanaweza kutoka kwa taratibu za kisheria (sheria inasemaje isije tukawa tunaongea kwa huruma kwa kuwa hawa jamaa tunawafahamu) au mpaka msamaha wa rais ndiyo wanaweza kutoka

bdo,Mimi binafsi niliyeanzisha uzi huu simfahamu wala sijapata kumwona Nguza Viking au mwanaye Papii Kocha ana kwa ana zaidi ya kuwaona kwenye TV au CD za muziki! Baba na mwana ni wasanii wa muziki waliokuwa wakiiburudisha jamii na bado wanatuburudisha kupitia TV na CD zao za muziki japo si kama wapenzi wa muziki wao walivyozoea!

Waswahili wanasema,"Zimwi likujualo,halikuli likakwisha." Ikumbukwe kuwa Nguza Viking na wanawe watatu wa kiume walisingiziwa kesi ya kulawiti na kuhukumiwa kifungo cha maisha! Lakini kwa msaada mkubwa wa kisheria toka kwa mwanasheria maarufu nchini Mabere Marando watoto wawili wa Nguza waliachiwa huru!

Lakini wakati wa kesi ushahidi uliotolewa mahakamani uliwakandamiza kuwa walishirikiana na baba yao kuwalawiti wale watoto wa shule ya msingi huko Sinza! Inasemekana kufungwa kwa Nguza Viking na wanawe kuna mkono wa mtu anayelipiza kisasi! Sijui labda kuna siku watatoka kwa msamaha wa rais!!
 
Mwenyezi MUNGU awajalie afya njema, 2015/2016 rais ajae awatoe. hawa watu nilisikitika sana kwa tuhuma walizo bambikizwa, ni sawa sawa na mtu aliye bambikizwa kichwa cha mtu, sema yeye sijui alinusurika vipi. lkn matukio kama haya ni mengi mno, watu hadi wanahukumiwa vifo,maisha gerezani kwa dhuruma kama hizi. unadhani Rwakatare angeweza kupona kwenye kesi yake ya ugaidi?! . hii ndiyo tz ya pinda na polisi wake, ogopa sana! "hakuna taifa la watu waongo kama watu wa tz - Lawrence Masha", wakikwamlia kukupoteza unapotea. MUNGU ataonesha njia ndugu zangu.
 
Nilivyokuwa nafuatilia ile kesi kwenye vyombo vya habari wakati ule nakumbuka maelezo ni kwamba watoto wale walitendewa vitendo hivyo takriban kama mwezi mzima hivi ndio ikaja gundulika, hapa napata taabu kidogo, inawezekanaje mtoto mdogo aingiliwe kimwili na mtu mzima na kisha arudi nyumbani fresh tu, ale, aogeshwe,alale na bila wazazi wake kumgundua!! Watoto wenyewe umri wao kwaujumla ni kama miaka 13 ndie alikuwa mkubwa kabisa wengine walikuwa wadogo sana, sasa ikiwa msichana mkubwa kabisa ambaye ni bikira akigongwa kwa x ya kwanza huwa wanashindwa hata kutembea vizuri iweje kwa watoto wadogo kama wale eti watiwe mdude mwezi mzima bila ya familia zao kushtukia??!! Halafu kwenye kesi inasemwa walitaka kumwingiza mapaka bibi yake na Papii! Binafsi naamini kesi ni ya kupika kabisaa, mwalimu wakaona halimuhusu wakamwachia!! Ok' sawa, waliomuhukumu ndio wenye nchi na sisi mwisho wetu ni kulalamika tu kama hivi!!
 
nafikiri kesi hii anaifahamu vizuri Mkuu MABERE NYAUCHO MARANDO,ADVOCATE!Ni vigumu kupika kesi KISUTU,Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.Pia ni hatari kutafuta huruma mahakama yoyote:kule ni tuhuma-ushahidi-sheria-hukumu,katika mzunguko huo.LAKINI KAMA KUNA ANAYEMJUA FABRICATOR AU MPISHI AU MCHAKACHUAJI,na kweli ana uchungu na BABU SEYA NA FAMILIA,awe wazi abebeb msalaba wake apige kelele mpaka haki ipatikane.VYOVYOTE KWELI ITASHINDA KWA HILI SIKU MOJA.
 
Wapendwa Naupataje Wimbo Wa Salima Binafsi Naupenda Sana Maana Nimejarib Kupitapita Mpaka Waptrick Sijaupata
 
:Ndungu yangu ktk case hii kuna siri nzito ambayo watu wengi hawaijui na kubaki kulaumu viongozi hasa kiongozi mkuu wa nchi, kiukweli hawa jamaa wanahusika katika case kuna ushahidi wa CD inayoonyesha hawa jamaa wakifanya jambo lile na kikubwa hawa jamaa walikua wakiandaa move ya X, sasa kilichomsaidia yule teacher na wale watoto wawili hawakuonekana ktk ile move, nimewapa kwa ufupi tu llkn kuna mlokongo mrefu ktk ile case..mengine nitawaambia next time wacha niendelee na majukumu mengine...
 
Back
Top Bottom