Baba na mama nani mwenye uchungu zaidi wa mtotoi? Soma kisa hiki...

Tall

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
1,425
165
Majuzi majira ya saa 1 jioni hivi katika moja ya vitongoji vya jiji la Dar,jamaa mmoja alipata mkong'oto wa nguvu.Mambo yalikuwa hivi: Jamaa huyo alikuwa amezaa na binti mmoja,kutokana na ukali wa maisha binti aliekuwa na mtoto mdogo akaamua kuanza biashara ya kuuza maandazi,mwanae akamkabidhi kwa majirani,Jamaa alipokuja alimkuta bibie hayupo, alipouliza aliambiwa kaenda barabarani kuuza maandazi.Kwa kasi ya ajabu na hasira nyingi huku akiwa tayari kakunja ngumi, akaondoka kumfuata mpenzi wake,alipofika akaanza kumpiga vibao na mateke mbele ya watu,akachukua beseni kubwa lililokuwa na maandazi akalikanyaga na kulivunja,maandazi yote akayamwaga chini huku akiyakanyaga.Watu wakauliza kulikoni?yule binti akajibu'' kwa vile nimezaa nae imekuwa nongwa'', Jamaa nae alijibu kuwa ''mwanangu anapata shida sana yeye yupo huku kamwacha mtoto peke yake''.Kuna waliosema yule dada aende polisi,wapo pia waliosema,alipe maandazi yote palepale, na wengine wakasema mnamchelewesha,apigwe.Japo yule jamaa alijitetea kuwa pesa za mtaji katoa yeye,lakini tayari alishachelewa,kwani jamaa walishaanza kumshushia kipigo,kuona hivyo alitoka spidi hadi kwenye ATM zilizokuwa jirani na tukio ambapo maaskari waliokuwepo lindoni walimwokoa.
1.Mwana JF ungekuwepo pale ungekuwa upande gani?.APIGWE,APELEKWE POLISI,AU ALIPE?
2.Huyu jamaa alikuwa na uchungu sana na mwanae alieachwa peke yake,lakini je bila upendeleo na ukisema toka moyoni unadhani nani mwenye uchungu zaidi wa mtoto kati ya baba na mama?......usijali jinsia yako just be fair
 
mama anauchungu sana na mwanae kwa sababu kaona kuliko akamweke kwenye upepo huku anauza mandazi bora amwachie jirani na yy akatafute
 
Kwanza Mwanaume inaonyesha hatoi hata hela ya matumizi harafu anaenda kumpiga dada wa watu.
Mwenye uchungu ni Mama wa mtoto hakupenda kumtesa mtoto kwa jua ,vumbi wakati akitafuta riziki.
 
Mama siku zote ana uchungu na mtoto... au umesahau ule usemi "Uchungu wa Mwana..."

Saa 1 jioni kutoka na mtoto kwenda naye kwenye biashara ni risk kubwa, kwanza upepo ule wa jioni, baridi, vumbi na hata mazingira ya biashara yenyewe... huyu dada anamjali sana mtoto wake ndio maana akaomba hifadhi ili angalau apate pesa za kumnunulia maziwa na chakula

Hebu muelekeze M-J huyo jamaa alipo... maana hata mimi hajanifurahisha
 
Jamaa ni mjinga na auseme ukweli wake wala sio mtoto; hapo ni mijiwivu yake ya kizamani hana lolote! kwanini yeye asifike na kumfuata mtoto aliko na akaendelea na kumbembeleza! hana uchungu wala nini huyo jamaa!

Ningewajua waliomchapa jamaa ningewanunulia soda! Sehemu nyingine watu wangekaa kimya eti wasiingilie ndoa! safi sana alivyoshikishwa adabu! Na jifunze!
 
Back
Top Bottom