Nimeshabikia sana CHADEMA lakini kwa ninayoyaona sasa, yanadhihirisha something is seriously wrong. Imani inashuka. Mambo madogomadogo mnayakuza sana. Kulikuwa na sababu gani kumfanyia kikao huyu mzee kwa sababu tu ya matamshi yake ambayo kama haungwi mkono ni wazi hayana athari? Na kwa hilo tu amestahili kufukuzwa? Mtafukuza wangapi?
Mnatuacha katika sintofahamu, kama katika mstari huu kutoka kwa mshairi Mrisho Mpoto:
"Waliopo hatuwataki, na wanaotaka tuwape hatuwaamini"
Sijui mnataka tufanye nini sasa? Tuanzishe vyama vingine viwe vingi kama vile vya enzi ya Mobutu na Zaire yake? Mnatukatisha tamaa.