- umekaa na familia yako mnapanga budget ya familia, mnatenga fedha kwa ajili ya kulipia ada za watoto. Kesho Unaona jilani kanunua gari mpya ya kifahari na WEWE anachukua pesa mliyotenga kulipa ada tena bila kuitisha kikao cha familia, anaenda na kununua gari mpyaa kama ya jirani.
- Unamarafiki zako wanne wawili wana miaka 40 na zaidi, ni wakubwa na wa rika lako, wameoa na wanafamilia, wawili ni vijana under 18, cha kushangaza unajitoa katika urafiki na hao wa rika lako na kuwa best friend ya mmoja wapo wa under 18, alafu unajisifia eti kuna vitu unajifunza sana kutoka kwa kijana huyu, tena vya maendeleo vinavyojenga ndoa yako
- una nyumba imezungushiwa ukuta, ndani ya nyumba unalima mbaazi, unasisitiza eti nyumba yako itaendeshwa na kilimo cha mbaazi. Huko nje ya ukuta wako watu wamegundua mbegu bora ya mbaazi inayokua ndani ya muda mfupi. Lakini hujawahi kutoka nje ya ukuta wa nyumba yako, na huna mpango wa kutoka, pia watoto unaowatuma huko nje ya ukuta wanakuogopa kiasi cha kushindwa hata kukwambia kuwa kilimo cha mbaazi mnacholima ndani kwenu kimepitwa na wakati, nje ya ukuta kuna mbegu bora
- Una familia yako na wanoa wakubwa ambao umewaweka kuwa washauri wako, lakini kila siku unawatukana na kuwatisha kuwafukuza kwako, alafu unaitisha kikao cha familia ili wakushauri.
- Umeoa hujawahi kumtoa mkeo out hata siku moja wala hata kumnunulia zawadi, lakini kila siku unatamba kwenye magenge kuhusu outing na zawadi alizonunuliwa mkeo na boyfriend wake wa zamani kabla yako. Huku ukisisitiza eti mpaka leo unammiliki zipo kwaiyo zinakuhusu
- Umempa mwanao mkubwa kazi ya kukagua duka lako, anagundua kuwa umekuwa ukichukua pipi na kuwagawia madem. Anapoleta taarifa anakwambia upungufu wa pipi na hasara zake, alafu unakasirika na kuwashawishi wanao waliobaki wakamseme kwa majirani na vijiweni
- umepewa uongozi kanisani, alafu hutaki wanajumuiya kusali jumuiya ndogondogo katika mitaa yao kila jumamosi, eti sala ni moja tu siku ya misa jumapili
Familia hii, kila siku wanajisifia eti wanafamilia bora, ndoa itadumu, watoto wanafuraha, na mbwembwe myiingi. Yajayo Yanasikitisha