obedia musa
Member
- Nov 19, 2014
- 57
- 41
BABA MWENYE NYUMBA TUMAINI LA WANAKAYA.
Mara baada ya kuingia hapa nyumbani ameweza kufunga mianya ya matumizi yasiyo ya lazima na kuziba mianya mikubwa ya ukwepaji kodi.
Baba mwenye nyumba ameunda baraza dogo la mawaziri lenye mawaziri 19 na manaibu 15. Ikilinganishwa na awamu iliyopita baba mwenye nyumba amepunguza mawaziri 12 na manaibu 9 pungufu ya awamu iliyopita iliyokua na Mawaziri 31 na manaibu 24 ambao kila mmoja alipewa mshahara kati ya Mil 3.8 hadi Mil 5, kodi ya nyumba, gari lenye thamani ya Mil 250 na mafuta lita 1,000 kila mwezi.
Baba mwenye nyumba ameahidi kumfukuza kazi Waziri yeyote atakayebainika kuwahi kutumia hovyo madaraka yake, kula rushwa au kuisababishia hasara kaya yetu, hivyo uteuzi wao siyo jambo la kufurahia
Baba mwenye nyumba yupo mbioni kufungua mahakama maalum itakayowashughulikia wezi wakubwa wa jasho la wanakaya haraka iwezekanavyo bila kujali vyeo vyao. Wabobezi wa sheria wapo ukingoni kuikamilisha mahakama hiyo.
Tayari wanafunzi wote wa elimu ya juu wameshatangaziwa kupewa mikopo, huku akiwasihi wazidishe jitihada zao kwenye masomo.
Tangu ahamie hapa nyumbani umahiri wake katika fani ya utabibu umedhihirika kwa kuyatumbua majipu makubwa tu, katu hajashughulika na vijipu vidogo
Wanakaya tulikata tamaa, lakini sasa matumaini yamerejea na tunashuhudia mabadiliko makubwa waziwazi. Sifa zake zimeenea kwa majirani wote na vijiji vya mbali pia, wengine wanatamani awe baba yao japo kwa siku tatu tu.
Hongera Baba mwenye nyumba, Mungu akulinde.