Baba Muhadhama Kadinali Pengo usitupeleke huko unakotaka kutupeleka

Baba Muhadhama Kadinali Pengo usitupeleke huko unakotaka kutupeleka

Kardinali Pengo hana tofauti na lile tawi dogo la CCM linaloiitwa Bakwata. Kazi yao ni kutetea unafiki wa CCM, hawa viongozi wadini hawana maadili yoyote, wamekuwa waongo na wanafiki wa wanasiasa. Wameacha kabisa kusimamia ukweli, wamekuwa makuadi ya CCM.
 
Hivi kwanini huyu Kardinari asinyamaze tu.
Nasubiri jumapili ya leo kama hajaamshiwa dude!
 
Mimi ni Mroma . Ila Viongozi wa dhehebu langu naomba Mungu awangoze waone yanayoendelea ambayo hawayaoni.
 
Mkuu hata mimi najiuliza. Kwani Muadhama Pengo kakosea wapi? (Full disclosure: mimi ni RC na naamini kwenye umuhimu wa katiba mpya). Lakini mimi sioni kosa. Mhashamu Askofu Niwemugizi alitoa maoni yake. Na alichofanya Muadhama ni kusema kwamba msimamo wa Niwemugizi siyo msimamo rasmi wa Kanisa. Sasa kosa li wapi?

Anyway labda tutajuzwa kosa la Mhashamu Niwemugizi vinginevyo sioni kosa lake (labda kwa sababu Niwemugizi kaongea lile wengi tunalopenda kulisikia na Muadhama hakuongea lile wengi tunalotaka au tungependa kulisikia kutoka kwake.
Naungana na wewe kwa asilimia mia moja, hakuna kosa ambalo Kardinali Pengo amelifanya. Mhashamu Askofu Niwemugizi aliongea kama msimamo wake yeye na si wa kanisa la katoliki. Kwa kuwa hakuna kikao chochote kilichofanyika na kutoa msimamo kama huo, hivyo waache kumnyooshea kidole Kardinali Pengo kwani yupo sahihi.
 
Pengo anaharibu sana. PERIOD.
 
Pengo alipokuwa anatoa kauli za kuikejeli na kuikebehi Serikal ya Kikwete mlitambua Kama ni Msimamo wa Kanisa Katoliki sasa hivi kaamua kumuunga Mkono Mkatoliki Mwenzie Rais John Joseph Povu linawatoka!
Kipindi cha 2015 nilipowaona wale masister pale Mikumi wakimpigia kampeni nikaanza kumuulizia mmiliki wa kobe aliye mpandisha Darini... Mchzo wa Kanisa ulianzia Mikumi na unaendelea kwenye awamu
 
Amekula maharage ya ikulu huyu
Wewe ndo mchochez, vita ya imani unayoichochea ni kubwa kuliko unavyofikiri, kosa kubwa ni lipi hapo hadi povu linakutoka..? Siasa imekushinda....., unakuja kwenye imani, mkatoliki gani ww...!??
 
Kosa lake ni kusema maneno ya askofu niwemugizi si msimamo wa kanisa? Ni ilo tu au kuna lingine?
Niwemugizi alisema mwenyewe siku ile kuwa ni msimamo binafsi na sikuona maana ya Pengo kurudia.
Hivi huwa hatusikilizi?
 
Kuhubiri Haki na Amani Ni Muhimu sana Kwa Ustawi wa Jamii
Kweli kabisa. Sote ni mashahidi wa namna haki na amani ilivyo msamiati mgumu leo ukilinganisha na awamu zilizopita. Je tumeisikia hii idara kama tulivyoshuhudia matamko yao huko nyuma! Dunia bila unafiki haiendi!
 
Kweli kabisa. Sote ni mashahidi wa namna haki na amani ilivyo msamiati mgumu leo ukilinganisha na awamu zilizopita. Je tumeisikia hii idara kama tulivyoshuhudia matamko yao huko nyuma! Dunia bila unafiki haiendi!
Haki na Amani Hebu Tujadili Kidogo Nadhani Bila Amani Muumini Hawezi Kwenda Kanisani pia Anaweza akawa Amenyimwa Haki akakosa Amani
 
Swali kwako mkatoliki wa Dar .... nini maana ya KARDINALI na ni yapi MAJUKUMU yake na MIPAKA YAKE YA KAZI?

Pili, Kauli ya MWAKILISHI WA VATICAN NCHINI juu ya kauli askofu wa Ngara .... ni kwamba amemuunga mkono KARDINALI PENGO na kusema kauli ya askofu was Ngara si MTAZAMO wala MSIMAMO wa KANISA KATOLIKI .....

Ni nini kauli yako? .... mbona MASHAMBULIZI yaelekezwa kwa Mhashamu KARDINALI PENGO pekee?
Jamani labda mngeweka clip ya video ndo mjadala uendelee nakumbuka Niwemugizi alisema categorically siku ile kwamba ni maoni yake binafsi na akasema kwa msimamo huo kama ataitwa mchochezi yuko tayari.mwenye video clip aweke
 
Kosa lake ni kusema maneno ya askofu niwemugizi si msimamo wa kanisa? Ni ilo tu au kuna lingine?
Yeye Pengo anasimama kama nani kulisemea kanisa? Pengo wenu huyu ni useless kuanzia kanisani hadi kwa jamii/ndugu zake huku Rukwa
 
Hakumsikiliza niwemugizi vizuri kwasababu niwemugizi aliweka wazi kuwa sio msimamo wa kanisa bali wake peke yake
Kumbuka pengo hana cheo chochote zaidi ya uaskofu wa jimbo la dar
Anamsemeaje mwenzake wakati ni askofu kama yeye
Tatizo anazeeka vibaya
Tunajua yeye ni ccm
Na amesahau kabisa kuonya maovu yanayotokea katika jamii
Ngalalekumtwa huyu ndio kila kitu ndani ya kanisa la tanzania
Ungejua tofauti kati ya Muhadhama na Muashamu usingeropoka huu ujinga wako
 
Pengo alipokuwa anatoa kauli za kuikejeli na kuikebehi Serikal ya Kikwete mlitambua Kama ni Msimamo wa Kanisa Katoliki sasa hivi kaamua kumuunga Mkono Mkatoliki Mwenzie Rais John Joseph Povu linawatoka!
Pengo kumuunga mkono Magufuli hajakatazwa , lakini asijifiche kwenye kichaka cha kanisa , SI MSEMAJI WA KANISA .
 
WanaJF
Salaam kwenu!

Haya ni maoni ya Mlei wa Kanisa Katoliki DSM kufuatia kutofautiana hadharani kwa Mwadhama Policarp Pengo na Makamu wa RAIS wa TEC Askofu Severine Niwemugizi....Endelea...

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC lina Kurugenzi na idara nyingi. Kiutawala Muadhama Polycarp Kardinali Pengo sio Mkuu wa Kanisa Katoliki wala si msemaji wake.

Mkuu na msemaji wa Kanisa Katoliki ni Rais wake Bishop Tarcisius Ngalalekumtwa na ndie Msemaji wake. Kuna Maaskofu na mapadre ambao ni wakurugenzi wa idara mbalimbali katika kanisa kama:-

Idara ya kichungaji.
Idara ya liturjia.
Idara ya haki na amani.
Idara ya katekesi.
Idara ya miito
Na nyinginezo wanayo dhamana ya kusemea idara zao.

Mhashamu Severini Niwemugizi hawezi kufungwa na msimamo wa Pengo anayeliingiza kanisa kwa nguvu katika siasa zinazo mfanya apoteze heshima yake.

Askofu wa kanisa katoliki ana mamlaka ya kiutawala na kichungaji katikak jimbo lake. Ndiyo maana hata ibada za kikatoliki askofu au padre hawezi kufanya ibada ktk jimbo lisilo lake hadi ruhusa ya askofu mahalia. Muadhama Pengo ni Askofu wa DSM wakati Niwemugizi ni wa Rulenge- Ngara.

Hivyo kila mmoja anayo mamlaka kamili na dhamira yake na hafungwi na mtazamo wa mwenzake. Ikumbukwe pia Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), ni Askofu Severine Niwemugizi
Kuhusu mambo yanayohusu imani kikanda yanasimamiwa na maaskofu wakuu na hapa kuna Mwanza, Dodoma, Arusha, DSM, Songea na Tabora na hapa ni kama kuna rufaa mbalimbali kutoka kwa waumini, watawa na au mapadre na kitaifa ndipo Muadhama anapohusika ikiwa ni pamoja na usharika wa makardinali wote duniani ambao pia huhusika na uchaguzi wa Papa.

Sasa ni vema huyu Muadhana Kardinali pengo atuambie Baba Niwemugizi amevunja kanuni ipi ya kanisa au na canon law. Niwemugizi kama Muadhama Pengo anafikiri Msimamo wake binafsi unawakilisha kanisa katoliki la Tanzania anapotosha kusudi kwa malengo maovu ya kisiasa.

Mahaba yake kwa CCM yanamfumba hata kusahau kosa kubwa Magufuli analofanya kama Mkristu na Mseminari kwa kukiuka mafundisho ya msingi ya Yesu mwenyewe, " Mpende Bwana Mungu wako kwa akili yako yote na mpende jirani yako kama nafsi yako.

Ndimi Mkatoliki wa DSM
Yeye Alilsha Toka Kimaisha Nadhani Hana Stresss Za Maisha Lakini Kwenye Hili Ataanza Kujifunza Maana Ya Stress
 
Back
Top Bottom