WanaJF
Salaam kwenu!
Haya ni maoni ya Mlei wa Kanisa Katoliki DSM kufuatia kutofautiana hadharani kwa Mwadhama Policarp Pengo na Makamu wa RAIS wa TEC Askofu Severine Niwemugizi....Endelea...
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC lina Kurugenzi na idara nyingi. Kiutawala Muadhama Polycarp Kardinali Pengo sio Mkuu wa Kanisa Katoliki wala si msemaji wake.
Mkuu na msemaji wa Kanisa Katoliki ni Rais wake Bishop Tarcisius Ngalalekumtwa na ndie Msemaji wake. Kuna Maaskofu na mapadre ambao ni wakurugenzi wa idara mbalimbali katika kanisa kama:-
Idara ya kichungaji.
Idara ya liturjia.
Idara ya haki na amani.
Idara ya katekesi.
Idara ya miito
Na nyinginezo wanayo dhamana ya kusemea idara zao.
Mhashamu Severini Niwemugizi hawezi kufungwa na msimamo wa Pengo anayeliingiza kanisa kwa nguvu katika siasa zinazo mfanya apoteze heshima yake.
Askofu wa kanisa katoliki ana mamlaka ya kiutawala na kichungaji katikak jimbo lake. Ndiyo maana hata ibada za kikatoliki askofu au padre hawezi kufanya ibada ktk jimbo lisilo lake hadi ruhusa ya askofu mahalia. Muadhama Pengo ni Askofu wa DSM wakati Niwemugizi ni wa Rulenge- Ngara.
Hivyo kila mmoja anayo mamlaka kamili na dhamira yake na hafungwi na mtazamo wa mwenzake. Ikumbukwe pia Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), ni Askofu Severine Niwemugizi
Kuhusu mambo yanayohusu imani kikanda yanasimamiwa na maaskofu wakuu na hapa kuna Mwanza, Dodoma, Arusha, DSM, Songea na Tabora na hapa ni kama kuna rufaa mbalimbali kutoka kwa waumini, watawa na au mapadre na kitaifa ndipo Muadhama anapohusika ikiwa ni pamoja na usharika wa makardinali wote duniani ambao pia huhusika na uchaguzi wa Papa.
Sasa ni vema huyu Muadhana Kardinali pengo atuambie Baba Niwemugizi amevunja kanuni ipi ya kanisa au na canon law. Niwemugizi kama Muadhama Pengo anafikiri Msimamo wake binafsi unawakilisha kanisa katoliki la Tanzania anapotosha kusudi kwa malengo maovu ya kisiasa.
Mahaba yake kwa CCM yanamfumba hata kusahau kosa kubwa Magufuli analofanya kama Mkristu na Mseminari kwa kukiuka mafundisho ya msingi ya Yesu mwenyewe, " Mpende Bwana Mungu wako kwa akili yako yote na mpende jirani yako kama nafsi yako.
Ndimi Mkatoliki wa DSM