Baba Mkwe wangu ananitishia NISHAURINI


Kwa hiyo unaona ndoa ni nzuri kwa sababu ya kibano cha maisha? Na kama hakuna kibano cha maisha?
 
Mimi naona kama ulifanya kosa kumrudisha kwao kabla hujawaeleza wazazi wake tatizo ni nini. wao hawana taarifa za upande wako wana za mtoto wao tu. Isitoshe suala hili si la wazazi wake peke yao. Nadhani ungemshirikisha mshenga wako pamoja na wazee wa busara wakusaidie. Wazazi wake pia hawana busara walitakiwa wakuulize kulikoni, kabla hawaanza kukurushia maneno ya kipuuzi. Hii inaonyesha hukufanya homework yako vizuri kabla hukuoa. Uliangalia uzuri nini? Uzuri wa mtu si sura ila watu wengi hubabaika na jinsi mtu anavyoonekana. Ilibidi usome tabia ya mwenzio kabla hamjaoana. Tafuta wazee wa busara mkae wewe,wazee wako na wake muangalie jisi ya kulitatua. Pole.
 

Pole sana ndugu.
Kwenye ndoa huwa wanaume tunafanya makosa sana ndoa inapoanza, hatuweki misingi ya ndoa na kuisimamia pale ndoa inapoanza na kuchukua hatua sitahili misingi inapokiukwa. Moja ya makosa ni kuonesha ustaarabu pale misingi ya ndoa inapokiukwa. Uzoefu nilionao kwenye ndoa (7years) ni kwamba ninapochukua hatua ambayo inaonekana ni harsh kwa misingi ya ndoa yangu iliyokiukwa na wife kosa hilo halirudiwi tena. Nimeshafanya hivyo hadi ndugu wa wife wakanitishia kunitenga nikawaambia poa tu, nitabaki na ndoa yangu na lazima afuate misingi ya ndoa yangu na kama hataki atimue na sihitaji msaada wowote kutoka kwenu. Waliweka mgomo kutokuja kwangu for 6 months lakini sasa wanakuja na nina wasaidia! Weka msimamo bwana, wewe ni mwanaume!
 
Kwa hiyo unaona ndoa ni nzuri kwa sababu ya kibano cha maisha? Na kama hakuna kibano cha maisha?
Kiranga,
Ndoa ni nzuri kwa mambo mengi, mungu aliyemuumba mwanaume aliona ni vyema akawa na msaidizi kwa kuwa Alijua kuwa hatoweza kuface challenge za maisha akiwa peke yake,kwa hiyo sio kibano peke yake, mwanamke ni mwenza katika maisha, ni mwenza katika kila kitu na ni msaidizi wa kweli.Nilitoa mfano wa kibano angalau kukuonyesha ni namna gani unahitaji kuwa na mwenza.Maisha yana nyakati nyingi unahitaji mtu ambaye atakuwa na wewe katika steji zote za maisha wakati wa furaha mnafuraia mafanikio pamoja, wakati wa huzuni mnahuzunika pamoja, mnatofautiana kwa jambo moja au jingine lakini bado mnakuwa pamoja.
 
kama wazazi wa binti hawataki kukusikiliza kujua tatizo ni nini na wanalazimisha kumrudisha binti kwako basi acha wamrudishe lakini wewe ondoka mwachie binti yao nyumba wewe angalia utaratibu mwingine wa maisha
 
mkuu pole dah inaelekea hao wakwe zako wote walikuaga maaskari..utiii amri bila shurutii
 
Wazazi wengi uwasikiliza wakwe zao zaidi ya mabinti zao...unajua kwa nini?

Wewe utakuwa ulikuwa hupeleki misaada ukweni. Lol

Ila kwangu mimi kama mwanamke napenda sana wazazi wangu wa stand by me...ingawa si kwa staili hiyo...ila it feels good ndugu na jamaa zako wakikuamini
 
Watz wengi huwa tunakosea kutoa ushsuri mahali amabpo una mgogo baina ya pande mbili kwa kusikiliza madai ya upande mmoja,ni imani yangu kwamba huyo mkeo amewaambia maneno mazito na mabaya kuhusu wewe ndio maana wamereaact,kuna njia za kufuatwa kumaliza taizo hili sijui ndoa yako uliifinga kimisingi gani yaani serikalini,kanisani,msikitini aua wapi???
 
kama wazazi wa binti hawataki kukusikiliza kujua tatizo ni nini na wanalazimisha kumrudisha binti kwako basi acha wamrudishe lakini wewe ondoka mwachie binti yao nyumba wewe angalia utaratibu mwingine wa maisha
duh mgogoro hauwi solved hivyo naamini lengo la kumrudisha kwa wazazi wake sio kumkimbia ni ili apaeleke tarifa nini kinaendelea na wazazi wajue kwa busara zao nini wanaweza wakafanya kunusuru ndoa ajabu wazazi wenyewe hovyo wamekuruouka kwenye kufanya maamuzi
 
ww pia huna busara kwanini unarudisha mkeo nyumbani mara kwa mara?Miaka 10 adi leo hamjajuana tabia zenu?
Suluhisho la ndoa hufanya na wanandoa wenyewe na si wazazi wala majirani,Marafiki.

Mkishindwa kuelewana na mkeo hama chumba kwa mda adi hasira zikuishe na sio kumfukuza mwenzio na kwenda kujiongezea maneno na chuki kwa watu wa nje.Hayo mambo ya kufukuza wanafanya mwenye ndoa changa ikifika miaka 4 kuendelea mnakuwa mmeshajuana tabia.sio kwamba watu hawagombani wengi tunakwaruzana kwenye ndoa zetu lakini tunayamaliza mwenyewe kimya kimya na si kufukuza wala kwenda kushitakiana.
 
mwaga mboga kama hawajakuita wakawaulizeni tatizo ni nini?mwambie baba mkwe mwanawe analazimisha anipe tigo!!kwishney
 
Duh! kweli dunia hii ina mengi, Mkuu kelele za chura hazimzuii mtu kulala, na ukiona chura anakufanya ushindwe kulala ujue huna usingizi! Mi nadhani wanaelewa lililotokea ila wanafanya kusudi!

Muhimu ni kusolve hilo tatizo mojakwamoja, So jikaze na usubiri mpaka muyamalize ndio umrejeshe!
 
Nakushauri mtafutie bi mdogo kuongeza ushindani,mimi sasa hivi nimeamini kuwa ukitaka kujua tabia ya binti fuatilia tabia ya mama mzazi ama mlezi!

kaka umesema kweli,,, tabia huanzia nyumbani..... victim wa mianajike kama hiyo ni wengi mno........ afikirie maisha mengine hapo hamna kitu,,,,
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…