Baba mdogo awadhulumu watoto wa Marehemu

je parle

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,882
3,620
Yatima tuwapende na sio kuwadhulumu na kwa kuwa nguzo zao zimeondoka au nguzo Moja Imeondoka !

Kuna watu wanadhuluma Hadi shetani anakaa pembeni kushangaaa.

Jamaa mmoja huyu alikuwa anaumwa sana takriban mwaka na zaidi, Amehangaika mno sijui ni hospital gani ambayo haijui.

Huyu jamaa alikuwa na wake wawili maneno TOFAUTI na vibanda vyake kama vitatu mjini hapa.

Nyumba mbili kazijenga sehemu Moja ila Kuna kama mpaka Fulani hivi.

Nyumba moja ndogo anakaa na bi mkubwa na nyumba kubwa kapangisha

Nyumba nyingine ipo wilaya nyingine anakaa mkewe mdogo na watoto

Wakati anaumwa alitaka kuuza hii kubwa ya wapangaji ila kaka yake mkubwa kamkataza na kumwambia usijali maradhi ni kawaida utopona tu kuwa na subira

Jamaa akaachana na mteja Ambae alikuwa anataka kununua kwa Milion 14.

Siku zimeenda jamaa kazidiwa akafariki

Watu wamezika fresh Kila mtu karudi kwao

Mwezi mmoja mbele kaka WA MAREHEMU anataka kuuza nyumba kubwa Milion 10 !!!!

Mke mdogo akakataa
What the hell Milion 10? Si mume wetu alitaka kuuza Milion 14 ukamkataza sasa iweje ukubali Milion 10 au unalako jambo.?

Kaka akaona huyu mke mdogo kihere here lakin hanijui kama Mimi ndio kaka na maamuzi yote ninayo Mimi.!!!

Siku zinakatika jamaa anakomalia sana kuuza nyumba Kila siku anahitisha vikao na wake WA MAREHEMU

Ila mke mkubwa alishatonywa kama hapo usidai hata kitu kimoja Cha marehemu hata wakikufukuza kwenye hiyo nyumba pia ondoka kapange wasije wakakuroga

Mke mdogo na yeye kasikia habar na anajua kuhusu ushirikina kwamba jamaaa wanapuliza sana

Kuna cenario ilitokea katika ukoo huo .Kuna ndugu alifariki aliacha vimali flani sasa mkewe katika kudai Hadi mahakami ikawa tafran kubwa siku anapewa haki na mahakama ya kumiliki hizo Mali za mume ndio siku ambayo alipata upofu Hadi leo haoni

Kaka mkubwa katafuta mteja kapata WA kununua nyumba milioni 20 na akawaitw wakeze marehemu kuwa nyumba ikapatikana mtu WA Milion 12 ila dalali anakula Milion 2

Wake wamekubali ili yaishe mana wanajua jamaa ni mtata

Basi hizo Milion 10 zikagaiwa kwa wakeze wawili na watoto.

Mambo yakaishia hapo

Huyu kaka mkubwa anajiona mwerevu kwa kula Hela za yatima na wajane .wananchi tunamtabiria mabaya sana kwa kitendo hiki Cha kifedhuli.

Dua ya mtu aliedhulumiwa Haina pazia hata kidogo ni dakika tu Allah kujibu Dua za namna hiii.......

Na kibaya zaidi hata kijijin kwao habar zimeshavuja kama kaka mkubwa katenda vitendo vya hovyo.

Watu wanamuangalia hizo Hela atatumia miaka mingapi.
 
Iyo kama sio Tanga, basi maeneo ya pwani, au ikizid sana lindi au mtwara ndo kuna jamii za aina hiyo. Hapo huyo kaka nae ana mke zaid ya mmoja utakuta! Kuoa wake wengi ni kuongeza umaskini kwenye jamii! Ndo maana maeneo hayo 90% ni maskini!
 
Nyumba iliuzwa Ili kugawana pesa au kulikuwa na tatizo la familia za wajane lilohitaji pesa kutatuliwa?
 
Iyo kama sio Tanga, basi maeneo ya pwani, au ikizid sana lindi au mtwara ndo kuna jamii za aina hiyo. Hapo huyo kaka nae ana mke zaid ya mmoja utakuta! Kuoa wake wengi ni kuongeza umaskini kwenye jamii! Ndo maana maeneo hayo 90% ni maskini!
Ni hapa hapa dar
 
Back
Top Bottom