Baba Jonii, Bangi na Hasira

Baba Jonii, Bangi na Hasira

Gini

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2018
Posts
398
Reaction score
385
BANGI NA HASIRA ZA BABA JONII (Mchomvu).
Na Mwl George Sylvester Wambura.
+255716109169/+255755057229.

Eyooo Mchomvuuuuu wape mashavu wana wape mashavu. Moja ya jingle nimekuwa wakati huo nikisizikia kupitia Clouds Fm kwenye kipindi cha mchana cha XXL, wakiwa watangazaji watatu ndani ya mjengo (B12, Mchomvu na Dj Fetty). Ni wazi show ilikuwa kali sana kos kwenye 1&2 yuko Dj Steve B, hakika ilikuwa ni show kali sana baada ya revolution ya kipindi kilichoitwa Doctor Beat wakati huo.

Jana Jumamosi, Agosti 15, 2020 pale uwanja wa Uhuru kulikuwa na jambo kubwa sana ambalo limeacha historia ndefu. Na kipekee kabisa nichukue fursa hii kukipongeza chama changu, Chama Cha Mapinduzi (Ccm), Katibu wa Nec -Itikadi na Uenezi ndugu Humphrey Polepole kwa kuandaa tamasha la aina yake, Tamasha la Uzinduzi wa Nyimbo za CCM. Watu waliohudhuria walikuwa ni wengi haijawahi kutokea na wasanii waliojitokeza walikuwa wengi pia, hii inaonesha namna Ccm inakwenda kushinda kwa kishindo uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2020. Usalama ulikuwa wa kutosha sana na nikiwa miongoni mwa waliohakikisha wageni wamekaa sehemu walizoandaliwa na usalama mahali hapo upo wa kutosha.

Kila mwananchi aliyehudhuria alifanikiwa kukata kiu ya kupata radha ya burudani kutoka kwa wasanii wao wawapendao. Rais wa JMT Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kwa upendo mkubwa alionao kwa Watanzania na mahaba ya dhati alipiga simu na kuwasalimia watanzania na kuwaambia kuwa yuko nao mwanzo mwisho, ni upendo uliopitiliza, tunakuombea Rais wetu na Oktoba kura zote kwako #Kaziiendelee, #Mitanotena.

Washereheshaji kutoka vituo tofauti vya radio & Tv walishika mic kuwaita stejini wasanii, alianza Jimy Jamal, Baba Jonii (Adam Mchomvu), na kufuatiwa na wengine kama Lil Ommy, JoniJoo, Bdozen n.k.

Yes yes yes, Baba Jonii alimuita Emmanuel Mbaya kwa stage, akafanya yake na katika utani utani kama ambavyo utani upo mtaani tu akamwambia Adam Mchomvu kuwa “Sema Adam we mibangi sana ujue”, na kumkumbatia ishara ya ile vijana wanasema one lobe mwanangu. Binafsi ili sound kiutani sana kama ambavyo tumezoea kutaniana.

Mbasha akiwa anaondoka Adam Mchomvu akageuka na kumpiga mtama, Mbasha aliyumba na kuanguka, naamini aliumia lakini hakurudishia. Hapo ndipo inakuja tafsiri ya ukweli wa jambo lililosemwa. Waswahili wanasemaga kuwa “Ukweli unauma sana”, kwamba mtu akikutania kiukweli ukweli huwa inauma sana kiasi ambacho inapandisha hasira japo unatakiwa ujue kuidhibiti hasira maana hasira ikizidi matokeo yake ni kukushushia thamani kama ambavyo Adam Mchomvu thamani na heshima yake imeshuka.

Show ilikuwa ikiangaliwa na dunia nzima, tv stations, online platforms zilikuwa zinarusha mubashara (Live), mtu anakutania kiutani cha kawaida una react kiasi kile. Hiyo tu inaonesha alichosema Mbasha kuwa ni kweli Mchomvu ni mtu wa bangi na ilimuuma kuambiwa ukweli huo mbele ya kadamnasi.

Kutoidhibiti hasira ni udhaifu mkubwa na inaweza kupelekea kukosa hata kile kidogo ulichotakiwa kukipata, matokeo ya alichokifanya Mchomvu jana ni kutopewa tena fursa ya kusimama jukwaani na watakaokuwa na shughuli yao kwa kuhofia kuidharilisha aidha shughuli yao au brand yao (taasisi), Ccm ikiwa ni taasisi yenye heshima kubwa Duniani, yenye kuthamini na kutobagua mchango wa kila mwananchi, iliwapa nafasi watangazaji wote kupanda jukwaani lakini siamini kama wakati mwingine watakuwa na utayari wa kumualika Adam Mchomvu ku host shughuli nyingine kubwa, kilichokea jana kwa watu waelewa ni mwisho wa kumshirikisha tena.

Utani umekuwa sehemu ya maisha ya mwanadamu hasa Tanzania ambapo makabila kwa makabila hutaniana, ni kawaida kukuta Mkurya anamtania Mhaya au Muha n.k.
Wakati fulani nikiishi jeshini nilishuhudia utani uliohusisha familia ya marehemu na kabila walilokuwa wanataniana. Aliyefariki alikuwa ni mwanajeshi na ilikuwa baada ya kuaga taratibu za kijeshi juu ya kusafirisha mwili wa marehemu zifuate na kimsingi ndiyo walikuwa wanasimamia zoezi zima. Baada ya kuaga, mtani (kabila ambalo lina utani na kabila) la marehemu lilizuia jeneza kupandishwa kwenye gari mpaka alichodai kutoka katika lile kabila la marehemu kufanyika ndiyo mambo mengine yakaendelea. Sikuona wale wananjeshi wanawapiga wale watani, ni kwa sababu wanatambua kuwa jamii zetu zinaishi katika maisha ya utani ambao kimsingi sio wenye lengo ovu.

Ukimwangalia Mbasha usoni utaona alikuwa akitabasamu kabisa kiashilio cha maneno yake kuwa ni utani, Mchomvu ni kijana na Mbasha ni kijana pia, hawa wapo katika rika ya utani, ilimpasa Mchomvu achukulie kuwa ni utani na ajue muktadha wa utani ule, reaction yoyote mbaya itamuondolea au kumbomolea taswira yake nzima.

Swali ni je, nani ameonekana mvuta bangi kati ya Adam Mchomvu na Mbasha?

Kwa watu wenye uelewa mzuri watamuona Mchomvu kuwa mvuta bangi kweli maana matendo aliyoyaonesha hayana tofauti kabisa na mvuta bangi, hata uvaaji wake unaonesha kuwa ni mvuta bangi kweli. Sisemi Adam Mchomvu ni mvuta bangi NO NO, tafsiri ya matendo yake ndiyo inaleta picha kuwa atakuwa kweli anavuta, huwezi kuaminiwa na Chama kikubwa kama Ccm, show inatazamwa na watu dunia nzima halafu umevaa suruali inaning'inia makalioni. Mbona Jimmy Jamal hakuvaa hivo. Uvaaji wa suruali chini ya makalio ndiyo unatafsiri kuwa yawezekana Adam Mchomvu anavuta bangi. Reaction ya kumpiga mtama Mbasha inaonesha Adam Mchomvu ni mvuta bangi, kama unashindwa kudhibiti unachosema baadae kuwa kilikukera.

Mbasha ameilinda hadhi yake, kitendo cha Mbasha kutorudishia imeonesha ni mstaatabu kiasi gani. Ametambua kuwa mazingira yale sio ya kuleta fujo na kwamba kwa kufanya vile atakuwa ameidharilisha Ccm iliyompa nafasi ya kuwa katika jukwaa lile. Mbasha amekiheshimisha sana Chama na ameilinda taswira yake na ni imani yangu kuwa ataendelea kuuishi uungwana wake na kuungwa mkono na watu wengi.

Mbasha ameonesha ya kuwa anayaishi maisha na mafundisho ya Mungu ambayo yanatusihi kutolipiza hata kwa baya lolote, Mathayo 5:39 inasema “Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.” na huu mdiyo uungwana. Katika medani za siasa tungesema amekomaa kisiasa, na katika medani za kijeshi tungemtunuku u-field Marshall.

Kwa upande mwingine Adam Mchomvu amezidi kuonesha tabia za jamii ya watu wanaovuta bingi, sisemi anavuta bangi (tuelewane hapo), tabia za wavuta bangi ndiyo kama alizozifanya, hajui yuko wapi, anafanya nini, watu gani wanamtazama, kwa kuwa bangi ndiyo inamuongoza anajiona yuko sahihi. Ndiyo maana bangi kwa mujibu wa sheria za Tanzania inahesabika kuwa haramu na imepigwa marufuku. Mtu anayevuta bangi anaweza fanya lolote linalomtuma pasipokujua kwa kufanya vile ni kosa.

Mwisho: Adam Mchomvu, omba msamaha kwa Rais, Ccm, Mbasha, na Clouds Media na watanzania wote kwa kuwa tukio ulilolifanya ni la fedheha na umedharilisha kituo chako cha kazi na haikutakiwa kufanyika na mtu kama wewe, wewe ni role model wa vijana wengi wanaotamani kuwa watangazaji wa Radio, unawa inspire vijana wengi, pengine wazazi watawaona tasnia ya habari kama haiko sawa kwa sababu ya ulichokifanya.
It's me, your brother from another mother,
Mwl George Sylvester Wambura.
Chukulia yote niliyoandika in a very positive way dingilai, don't panic. Tchao!.
 
Ukiwa unapenda utani ujue na kusoma mazingira. We unaona mtu kamaindi halafu unaendelea kutania hapo kinachofata ni vifuti vya pua au mtama kama aliopigwa Country Boy watu wakadhani sarakasi.
 
We dada Umeolewa? Kama bado nikutafute unaweza sana tetea mumeo akifanya jambo la hovyo. Wote wawili wana makosa. Swali je huwa wanautani? Siku akutanie mtu we Gini ni kahaba huku anakuchekea....uone.
 
Kaomba radhi na mambo kama hayo kwa vijana ni yakawaida sana
Tusiwajengee chuki sana wasameeane maisha yaendelee
 
Clouds media wajitafakari
CEO watu kama hawa simamisha kazi tu
Hajui heshima ya Ofisi
 
Hakuna utani kama ule mbele ya kadamnasi kama ile... Na kama ni utani basi na Adam nae alimtania kwa Tama ndiyo mana alisema vinega kama wale huwa wanaishi nao .. Bangi pale mbele ya uongozi wa serikali ulikuwa inahusiana nini,,, Acheni kuleta utu wa kinafki sehemu za kazi kama zile muache ajifunze ili aweze ku ballance shobo hata kwa watu wengine
 
Mbasha kaharibu shughuli Kwa kumtania mvuta bangi. Mabangi kashindwa kuhimili kamkata mtama. Wote wakosaji.
 
Unaniambia mambo ya bangi mbele ya hadhara ya viongozi wa cham, serikali na live Tv waTanzania afu nikuchekee? Kwanza ule mtama alimstahi sana, ni ningemuongezea na makonde ya kutosha
 
Muhimu Kusoma Nyakati,Mahala, aina ya utani na kubwa zaiidi kumsoma vyema Yule umtaniaye..!


Utani si wa kila Mtu.



Linex Anavuta Bangi...?? Yes Yes Havuti Bangi.

Mchomvu Anavuta Bangii...?? NO NO Havuti Bangi.
 
Mkuu kama na wewe unatabia kama za Mbasha acha mara moja, iko siku utapigwa mitama nested kama ile ya DONNIE YEN unachotwa miguu kabla hujaanguka unachotwa kichwa.
 
Back
Top Bottom