Baba Fed amemuoa mkwe wake chap baada ya Fed kumuacha

Baba Fed amemuoa mkwe wake chap baada ya Fed kumuacha

View attachment 3631819
Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Klarensi Usakazi (86), mkazi wa Kitongoji cha Mbisi, Tarafa ya Chipanga, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, aliyeamua mtalaka wa mtoto wake ‘mkamwana’ aitwaye Mary (20) baada ya wazazi wake kudai kutokuwa na uwezo wa kurudisha mahari.

Hata hivyo, Mary anakuwa mke wa nane kwa Usakazi, wakiwamo wengine watatu wa familia moja ‘pacha’, ambao anadai kufurahishwa na tabia ya ukoo wao hadi kufikia uamuzi wa kuwaoa.

Usakazi mwenye ukwasi wa mifugo karibu kila eneo la Tarafa ya Chipanga alimuoa Mary Chaina (20) kupitia ndoa halali ya kimila iliyofanyika Januari 25, 2024, baada ya kuolewa na Fredrick ambaye ni mtoto wake.

“Ni kweli alikuwa mke wa mtoto wangu Fed (Fredrick), lakini waliishi mwaka mmoja na wakaanza kusumbuana. Mimi nikaona bora nimuoe ili kijana akatafute mke mwingine anayempenda na alifanya hivyo. Nikalipa mahari,” amesema.
Huo ni ukosefu wa maadili,mipaka ya uhusiano wa damu,kutojitambua,kutumia akili za kihayawani na kuvaa uso/moyo baridi usio na soni.
 
Ndiyo Kilichomfanya Ajifumbie Macho Baada Ya Kuona Utajiri Wa Chapa Ng'ombe
 
Waislamu ni watu wa ajabu sana, mtume Muddy pia aliyafanya haya,

Surah Al-Ahzab (33:37). Humo Allah anasema wazi kwamba Mtume Muhammad aliozeshwa Zaynab bint Jahsh baada ya talaka yake na Zayd ibn Harithah.

Muddy anadai kuwa "Na kumbuka ulipomwambia yule ambaye Allah amemfanyia wema na wewe pia ukamfanyia wema: ‘Shikilia mke wako na mche Allah,’ na huku ukificha ndani ya nafsi yako jambo ambalo Allah atakalifichua. Na ulikuwa unawaogopa watu, lakini Allah ndiye anayestahiki zaidi kuogopwa. Basi Zayd alipoacha haja yake kwake, tulikuoza kwake, ili wasiwe na tabu Waumini kwa wake wa watoto wao .”

Hivyo Quran pamoja na Muddy kwao ni rukusa kuoa mabinti wa vijana au watoto wao.
Hatutachoka kuwapa elimu ili muelimike na kutoa ujinga vichwani mwenu

Zayd hakuwa mtoto wa damu wa Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake,alikuwa ni mtoto wa kufikia tu,kwahiyo Allah alitaka hilo lijulikane mapema kwamba hakika mtoto wa kufikia sio mtoto wa damu,hivyo jambo hili liliwekwa ili watu wapate somo toka kwa Mtume

Ni kweli swala hili lilikuwa gumu sana kwa Mtume kama mwanadamu,hasa akifikiria je jamii yake itamuonaje,lakini maadamu ni Amri ya Allah basi lazima itekelezwe
 
Kichwa changu kinakuwa kigumu kuelewa kila nikikumbuka kuwa mtalaka hatongozwi na mtalaka yupo nyumba hyo
 
Back
Top Bottom