Baba awapa sumu watoto wake wa kambo, mmoja afariki

Baba awapa sumu watoto wake wa kambo, mmoja afariki

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Mkazi wa Majengo wilayani Urambo Mkoa wa Tabora, Seleman Mashaka (31) anatuhumiwa kuwapa sumu watoto wake wa kambo na mmoja kufariki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema amesema leo Jumanne Aprili 30, 2019 kuwa walipata taarifa jana Jumatatu saa 8:00 mchana za mtoto kufariki na mwingine mahututi kutokana na kunywa soda na juisi zinazodhaniwa kuwa na sumu.

Amedai kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa ndiye aliyewanunulia watoto soda na juisi na kuziwekea sumu kwa lengo la kuwaua.

Amedai mtuhumiwa anaishi na mwanamke ambaye ni mama mzazi wa watoto hao wanaodaiwa kuwekewa sumu.

Amemtaja mtoto aliyefariki kuwa ni Nyamizi Ally Ramadhani (7) na aliyelazwa Hospitali ya Wilaya ya Urambo ni Kalunde Ally Ramadhan (4), akibainisha kuwa hali yake ni mbaya.

Akielezea zaidi tukio hilo, Nley amesema mtuhumiwa hakuwa akipenda kuishi na watoto hao na alipenda zaidi kuishi na mama yao, huku akitaka watoto hao wakaishi na baba yao mzazi.

Amesema jana muda usiojulikana Mashaka anadaiwa kuwanunulia watoto hao soda na juisi na kuziwekea sumu ambayo haijajulikana.

Amesema Polisi inamshikilia mtuhumiwa na kwamba, uchunguzi unaendelea.

Naye mganga mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dk Paul Swakala amesema mtoto aliyebaki anaendelea na matibabu.
 
Sasa jitu kama hilo eti linasubir uchunguzi!!
Alitakiwa mpka sasa awe hana macho mikono na miguu huku akisubiri hukumu ya maisha jela!
 
Hivi watu wamekuwaje siku hizi?Hizi roho za kishetani vipi?Kwani wakati unampata mama haukujua ana watoto?Nina maswali kama gunia kumi hivi.Huu ni zaidi ya ukichaa.Kwamba mtu unawapa watoto sumu halafu unakaa pembeni ukisubiri wafe!
Nyakati za mwisho hizi
 
Hallo hii ni balaa kubwa.Mara yule kakata mapanga watoto.Yule kule kanyonga watoto wake.Mara,mwingine katupa mtoto chooni.Huyu naye kawapa watoto sumu.It's a hell in whole!
Ni visasi kwa kwenda mbele. Hakuna upendo! Tumegeuka kuwa binadamu wa mwituni!!
 
Hivi watu wamekuwaje siku hizi?Hizi roho za kishetani vipi?Kwani wakati unampata mama haukujua ana watoto?Nina maswali kama gunia kumi hivi.Huu ni zaidi ya ukichaa.Kwamba mtu unawapa watoto sumu halafu unakaa pembeni ukisubiri wafe!
Binadamu wa siku hizi wanafanya mambo ya ajabu mpaka shetani mwenyewe anashangaa
 
Sasa jitu kama hilo eti linasubir uchunguzi!!
Alitakiwa mpka sasa awe hana macho mikono na miguu huku akisubiri hukumu ya maisha jela!
Sheria lazima ifuatwe kikamilifu hata kama aliwapa sumu mbele ya Polisi na hakimu
 
Kwani wanawake wasio na watoto wameisha? Ndio shida za kupenda kitonga hizi, na hajui pengine baba mzazi alipokuwa akituma pesa za matumizi ndio zilikuwa zinamlisha na yeye pia.
 
Back
Top Bottom