Baba Askofu Mokiwa na tafsiri potofu ya Ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba Askofu Mokiwa na tafsiri potofu ya Ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by watenda, Oct 25, 2011.

 1. w

  watenda Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Juzi na jana, vyombo vya habari vimeripoti juu ya harambee iliyofanyika huko Yombo Dovya kwa ajili ya ujenzi wa taasisi moja ya kidini (dhehebu la Anglikana). Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mh. Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu na sasa Mbunge wa Monduli.

  Katika hotuba yake, mbali ya kumuomba Mh. Lowassa kurejesha shule za madhehebu ya dini zilizokuwa zimetaifishwa na serikali atakapokuwa rais, alitumia fursa hiyo kumsafisha Lowassa na kumuelezea kwamba asitishwe na kelele zisizo na msingi kuhusu tuhuma za ufisadi dhidi yake.

  Kauli hii ya kushangaza sana, imetolewa na mmoja wa viongozi wa dini wanaoheshimika sana nchini na mtu aliyekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ufisadi nchini na hata kuichagiza serikali kuchukua hatua dhidi ya wale wote wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi. Ni huyu huyu baba Askofu aliyepongeza hatua za kujivua gamba kama zilivyoasisiwa na rais Kikwete. Sasa leo, anapokuwa katika shughuli ya kumtakasa kinara mkuu wa mafisadi, tena baada tu ya kufanikisha kuendesha harambee yenye mafanikio (na yeye binafsi kuchangia milioni 20) anatueleza nini? Je, ana maana kwamba ghafla Lowassa amekuwa si yule aliyemshutumu sana na kushinikiza hatua dhidi yake? Au kwake baba Askofu Mokiwa, ufisadi unatafsiriwa tofauti hasa pale fisadi huyo anapokuwa na mchango katika kile anachokipigania yeye baba Askofu?

  Kwa maoni yangu, Baba Askofu amepotoka na tafsiri yake ya ufisadi imejaa makengeza na hata kumuondolea imani ya kiroho (moral authority) ya kukemea maovu katika jamii, ufisadi ukiwa moja katika maovu hayo.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Jamaa kaacha kazi ya uchungaji amekuwa kishoka sasa .Mbele ya pesa kweli kila kinawezekana.Matamshi yana maana kubwa sana .Kwanza yana kampeni ndani yake na kuwaponda wanao lia na lowasa kwamba ni fisaidi .Haya sasa .
   
 3. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Vita ya ufisadi ni magumashi, Dr. Slaa pekee ndio aliyethubutu kuwataja mafisadi lakini the rest wana generalise.
  List ya mafisadi mpy muhimu kwa sasa
   
 4. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Viongozi wa dini-vigeugeu!, wanasiasa -vigeugeu! n.k, n.k,................(Ndivyo dunia ilivyo tuizoee)
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Ni huyu askofu aliyetoka kifua mbele mwaka jana akasema kuna watu wamempelekea rushwa ya shs.11million kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi 2010, leo anasimama kupigia debe fisadi.Ule uchungu wa kufikia kukataa rushwa umetoweka ghafla!!!!! ama kweli pesa sabuni ya roho!! kanyaga twende Lowassa wataelewa somo tu.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaka labda ka million 11 labda kalikua hakatoshi kwene wallet yake akatafsiri Kama wamemdharau..
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  What people tend to forget ni kwamba these viongozi wa dini, wafanyabiashara (most of them r dhulumat), wanasiasa etc etc ni watu walioko on top of food chain ktk socioeconomic pyramid, they collect what they didn't sow, fatten their plates on expense of the poor and the weak. Bahti mbaya wengi wetu tunawaamini na kudhani wapo kututetea.
   
 8. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acheni Unafiki. Ni kweli Lowasa alituingiza kwenye matatizo ya Richmond. Lakini ni nani kati yetu asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe! Kila mtu ana upande mzuri na Upande mbaya pia. Je hamuamini kwamba mtu mwenye dhambi anaweza kutubu? Tutajieni katika CCM waliopo ni nani asie na dhambi mpaka mumkomalie Lowasa tu! Hata akifanya jema bado miongoni mwa watu wanataka tu aonekane mbaya! Acheni hizo! Mhukumuni mtu kwa haki. Si kila anapokwenda basi ni fisadi fisadi, mbona wengine hamuwasemi?Wacheni chuki binafsi mnakera!
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kosa la Baba askofu ni kutoa utabiri na kufanya kazi ya marehemu sheikh yahaya.Mokiwa anaheshimika saana hatukutegemea kujiingiza ktk kuligawa kanisa lake.Haoni kama waumini wake wasio-wana-ccm kawakwaza??????. Viongozi wa kanisa lazima wajifunze kujiheshimu wasije wakabomolewa heshima zao na kuanza kulaumu jamii.Mhashamu askofu Kilaini aliwahi kuwaudhi waumini wa RC kwa kutamka kikwete ni chagua la mungu hakina aliumiza sana wasio-wana-ccm.Leo hii Mokiwa ameingia kwenye mtego.Viongozi mnatukwaza sisi tusio-CCM.tafakarini kauri zenu
   
 10. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  We haya wee!! Napita njia tu!!!!!
   
 11. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Toka lini Mokiwa amekuwa mtu wa kuheshimika, uaskofu kaupata kwa rushwa na Lowasa ni mwenzake kwenye business ya ufisadi. hawezi kumrushiwa jiwe, unajua Lowasa mjanja sana anaenda kwa watu anaojua mambo yao ili waogope kusema yake.
   
 12. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamani ebu tuwekane wazi hapa! ivi kuna mtu anaweza kutuwekea wazi hapa ni ufisadi upi EL amefanya?
   
 13. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Heeh!! Uko dunia gani ndugu yangu?
   
 14. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Mokiwa na wenzake wamezungumziwa ktk kitabu cha ufunuo wa Yohanna.
   
 15. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  hivi hawa viongozi wa dini wameshindwa kabisa kufanya kazi waliotumwa na mwenyezi wamejiingiza kwenye siasa,kwanza ni wezi wa sadaka,pili ni wauza unga pamoja na kadhalika.
   
 16. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hivi umesahau usemi wa pesa sabuni ya roho?
   
 17. k

  kingtuma Member

  #17
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 18. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  nijuavyo mie nitaomba kurekebishwa kama nitakuwa nimekosea! Huyu bwana alijiuzuru uwaziri mkuu kuuonyesha kwamba anakubaliana na uzembe alioufanya kwa kuipigia debe kampuni ya richmond kupata deal la kuiuzia tanesco umeme wakati ilikuwa haina sifa.
   
 19. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Leo hii ni miaka 4 kama sikukosei toka alipojiuzuru lakini Richimond bado ipo tena kwa jina la symbion na enaendelea kuuza umeme tanesco kwa bei mbaya na ninavyosikia ni kwa inataka kusaini mkataba wa miaka 20 kama ilivyokuwa iptl. EL bado anahusika vipi na hili au kuna kashfa nyingine alifanya mie siijui.
   
 20. T

  Tiote Senior Member

  #20
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa dini ninayoamini mimi, unafiki ni moja ya dhambi kubwa sana kwa binadamu, ikizidiwa na shirki na kuua peke yake. Kitendo cha kiongozi mwenye dhamana ya kiroho kama huyu kuwa na selective memory kuhusu suala la ufisadi ni unafiki na kwa kweli unaona wazi kabisa kwamba kila mtu ni fisadi kama hajala nae na ni msafi kama atakula nae, hata kama fedha yake ni chafu. Tunaelekea wapi? Nani anaponya majeraha ya kihoro ya kondoo wa bwana?
   
Loading...