Baba Askofu Mokiwa na tafsiri potofu ya Ufisadi

Baba Askofu Mokiwa na tafsiri potofu ya Ufisadi

Jamani ebu tuwekane wazi hapa! ivi kuna mtu anaweza kutuwekea wazi hapa ni ufisadi upi EL amefanya?

ndo wale wale. Kaa na kujidanganya kwako na maswali yako yasiyo na kichwa wala miguu. Wewe ni nani kuhoji hilo wakati unayejaribu kuntetea anachosema ni kwamba si yeye peke yake ambaye ni fisadi.
 
nadiriki kusema kwamba kuna watu wameingia kwenye huduma za kiroho kuganga njaa na siyo kwa ajili ya kufanya kazi ya mungu. Hawa ndiyo wanaowaondolea waumini imani na hata kutukanisha viongozi wenzao ambao wana uadilifu mkubwa. Maskini nimemkumbuka baba Askofu Mtetemela.
 
Nguvu ya pesa! Hiyo ndo nguvu ya mkoloni pekee aliyekataa kuondoka baada ya wakoloni wnegine kurejea kwao. Mkoloni huyu atapata mateka wengi sana kuelekea 2015 na wale tuliowaamini sana wataendelea kutushangaza. Ilianza kwa waandishi, wakaja wahariri na wamiliki wao, sasa ni zamu ya viongozi wa dini mmoja mmoja na baadae itakuwa ni zamu ya wadilifu kurushiwa mawe na kuonekana ndo wachafu na kudhalilishwa. Mwisho itakuwa ni ile hadithi ya kijana aliyekwenda kijiji fulani kule singida na kukuta watoto wa rika lake wote wakikojoa damu kwa sababu ya kichocho na wale wakawa wanamcheka yule kijana na yeye kuonekana ndiye mgonjwa. Hatimaye kijana yule alifanya hila zote ili aambukizwe kichocho na alipofanikiwa alifurahi sana! Ndiyo Tanzania tunayoijenga kwa msaada wa wachungaji wa kondoo wetu!
 
Nyie mnashangaa hili la Mokiwa, mbona hamshangai la Kubenea au mmiliki mmoja wa vyombo vya habari ambaye kwa muda mrefu alikuwa kinara wa mafisadi na sasa ndiye anayeandaliwa kuwa mpiga debe wa fisadi huyu. Kila mtu ana bei yake!
 
nadiriki kusema kwamba kuna watu wameingia kwenye huduma za kiroho kuganga njaa na siyo kwa ajili ya kufanya kazi ya mungu. Hawa ndiyo wanaowaondolea waumini imani na hata kutukanisha viongozi wenzao ambao wana uadilifu mkubwa. Maskini nimemkumbuka baba Askofu Mtetemela.


Mnashangaa haya madogo hivi? Kuna makubwa sana yanakuja na mkakati huu utakumba majeruhi wengi sana, tena wenye hadhi na majina makubwa kwenye jamii. Hii ndiyo nguvu ya fedha haramu. Ninachojua kwa hakika ni kwamba wapo wazalendo wa kweli wenye mapenzi ya dhati na nchi hii na Mungu wa Yakobo atawasimamia ma kuwapigania ili hatimaye wemaa uushinde uovu.
 
Back
Top Bottom