Baba Askofu Bagonza ameandika kitu cha kweli

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
INAHITAJIKA MIAFAKA siyo MUAFAKA.

Kuna harufu ya mparaganyiko kila mahali. Ni kama tuna nchi moja yenye mataifa mengi ndani yake. Badala ya muafaka wa kitaifa, inahitajika miafaka kadhaa ili kuunda muafaka mmoja.

1. CCM si moja. Kuna CCM-Mpina na CCM-January. Kuna CCM-Mwendazake na CCM-Samia. Kuna CCM-Asili na CCM-Yatima. Hizi CCM zote zinahitaji muafaka ili tupate CCM moja.

2. Wapinzani si wamoja. Kuna wapinzani-Katiba Mpya na Wapinzani-Nusu Katiba Mpya. Kuna wapinzani-Mtungi na Wapinzani-Mahela. Kuna Wapinzani-Zanzibar huru na Wapinzani-Zanzibar Mkoa. Unahitajika muafaka kati ya wapinzania kabla ya muafaka wa kitaifa.

3. Serikali si moja. Kuna serikali awamu ya 5 rais wa sita na Serikali awamu ya sita rais wa sita. Kuna serikali-2025 na Serikali-2030. Hizi serikali zinahitaji muafaka.

4. Kuna bunge-live na bunge-giza. Kuna bunge-haramu ndani jengo halali na bunge-halali nje ya jengo halali. Kuna sheria halali zilizotungwa na bunge haramu.

5. Kuna Polisi-Tii sheria bila shuruti na Polisi-Tii shuruti bila sheria. Kuna IGP bila Polisi na Polisi bila IGP.

Unashangaa? Tanzania ni eneo la utalii. Kila kitu ni kiburudisho. Hatuambukizani Corona, tunaambukizana tabia. Mwenyekiti wa msiba anamuiga Spika namna ya kuongoza kikao cha mazishi. Askofu anamuiga OCD ili kuongoza kanisa. Kocha wa Simba anamuiga kocha wa Yanga lakini anafungwa mengi kuliko Yanga.

Bei ya mafuta imepandisha hata rushwa ya barabarani.
 
Hii nchi tuna vitu viwili tu tukiamua kuwa serious tutatoka. Kuna Ardhi na rasilmali watu. Wote twendeni tukalime kila siku kwaanzia asubuhi hadi jioni miaka mitano. Kwanzi watoto vijana hadi wazee. Tukifanya hivi tutapiga hatua sana. Na hatutakuwa tegemezi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom