Baba Amzawadia Mtoto Wake Atolewe Bikira

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Baba mmoja nchini Uingereza aliyekodisha kahaba wa barabarani ili amtoe bikira mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14 kama zawadi yake kwa mtoto wake huyo amenusurika chupu chupu kwenda jela miezi 10.

Baba huyo raia wa Poland mwenye umri wa miaka 42, aliendesha gari lake hadi mitaa ambayo makahaba wanapatikana kwa wingi katika mji wa Nottingham nchini Uingereza na kumwambia mtoto wake amchague kahaba yoyote anayemtaka kati ya makahaba wengi waliokuwa wamesimama pembeni ya barabara.

Kwa bahati yake mbaya, mtoto huyo alimchagua mwanamke ambaye alikuwa ni askari kanzu aliyejifanya kahaba.

Baba huyo aliyepandishwa mahakamani kwenye mahakama ya Nottingham, alikiri kumtongozea kahaba mtoto wake mwenye umri wa miaka 14.

Mahakama iliambiwa kuwa baba huyo na mwanae walipofikishwa kituo cha polisi, walihojiwa kila mmoja peke yake na ndipo ukweli wa mambo ulipofichuka.

Mtoto wake alielezea jinsi baba huyo alivyoendesha gari lake hadi eneo hilo la mahakaba na kumwambia achague mmoja.

Mtoto huyo ambaye hakutajwa jina lake kutokana na masuala ya kisheria alisema kwamba baba yake aliamua kumtafutia kahaba kwakuwa alikuwa bado ni bikira na baba yake alitaka kumpa zawadi hiyo ili aweze kuitoa bikira yake.

Baba huyo alinusurika kwenda jela miezi 10 baada ya hakimu kuona kwamba baba huyo alikuwa ni mwenye tabia nzuri ukiondoa zawadi yake hiyo mbaya kwa mtoto wake.
 
Back
Top Bottom