Baarua Kwa Mtandao Wa Halotel.

Baarua Kwa Mtandao Wa Halotel.

exalioth

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2016
Posts
2,395
Reaction score
4,152
YAH: MALALAMIKO KUHUSU CHANGAMOTO YA MTANDAO WA HALOTEL MKOA WA GEITA

Ndugu Huduma kwa Wateja,

Husika na kichwa cha habari hapo juu.

Mimi ni mteja wenu wa mtandao wa Halotel niliyepo mkoa wa Geita. Naandika ujumbe huu kutoa malalamiko rasmi kuhusu huduma yenu ya kupiga na kupokea simu ambayo imekuwa na hitilafu kubwa kwa siku kadhaa sasa hapa mkoani kwetu.

Suala linalotokea ni kwamba, mteja anapopiga simu, haisikiki ikilia (haiiti) lakini upande wa pili inapokelewa. Baada ya kupokelewa, hakuna sauti yoyote inayosikika kutoka kwa mpokeaji. Ili kufanikisha mazungumzo, inabidi mtu akate na kujaribu kupiga tena zaidi ya mara tatu mfululizo ndipo simu inakubali kusikika.

Hali hii inatukosesha mawasiliano ya muhimu na kusababisha usumbufu mkubwa, pamoja na kupoteza fedha (salio) kwa simu zinazopokelewa bila kusikika.

Tunaomba mamlaka na mafundi wenu wa mitandao waliangalie tatizo hili la mkoa wa Geita kwa uharaka ili turudi kwenye mawasiliano bora.
Wako

Mteja wenu.
 
Mkuu ofisi za halotel hapo Geita zinapatikana wapi? nashida nao! niko hapa katoro this time...
 
Back
Top Bottom