Jagermaster
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 654
- 321
'MUUNGANO FEKI USHATUCHOSHA WAZANZIBARI
HATUUTAKI'
Hiyo ni link kwenye u tube inayoashiria ni kiasi gani vuguvugu la wazanzibari kuitaka Zanzibar yao lilivyo juu. Just type hayo maandishi kwenye youtube.
Viongozi wa kitaifa hawawezi kuwa wawazi juu ya kile wananchi wao wanachokiamini. Kauli ya wananchi ni kauli ya viongozi, sema katika uongozi wa kisiasa ukweli huwekwa kando hadi pale utakapopata ufa wenyewe na kuamua kuvujia nje. Tusijidanganye kuwa hakuna tatizo.
Mkuu Raia Fulani,
Jisikie aibu kuongea uongo ulio dhahiri tena mbele ya hadhara!! Uongo wa namna hii haupendezi hata kidogo!!
Hili lipo wazi kabisa. Inajulikana sasa kuwa Wazanzibari wanaitaka Zanzibar yao kwa hali na mali. Wako wahafidhina toka kada mbalimbali huko visiwani walio wazi na walio ufichoni ambao, katika siasa, uchumi, n.k. wakitaka kujitenga na Tanganyika. Hili linathibitishwa na kauli za kina Jussa na wengine, na hii ni baada ya kuona kuwa Zanzibar ina rasilimali kadhaa ikiwa ni mafuta na gesi.
Wazanzibar walioko visiwani hawasiti kuonyesha hisia zao juu ya nia hii ya kujitenga. Wazanzibari walioko Tanganyika hawaonyeshi dalili yoyote ya wazi ya kupingana na ndugu zao wa visiwani, kama kwa njia ya makongamano na hata taarifa rasmi kwa umma. Hili suala wanaachiwa tu viongozi kulisemea wakati walengwa wakuu ni wananchi wa kawaida. Wazanzibari walio Bara wanafaidika sana na utulivu, amani na uelewa wa watu wa Bara. Watanganyika walioko vosiwani hawana amani kama hawa wazanzibari wa Bara.
Enyi wazanzibari mlioko Bara toeni tamko kulaani manyanyaso wayapatayo wa Bara huko visiwani, la tunajua lenu moja. Mnachuma Bara kama waasia wanavyochuma Tanzania. Toeni tamko sasa.
Hebu leta ushahidi wa hayo manyanyaso!
Jamani hawa watu mnawabembeleza wa nini? Waacheni tu wajitenge.
Hebu someni hii blog muone tunavyotukanwa:
FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI
Hebu leta ushahidi wa hayo manyanyaso!
mie naona unafiki anao nyerere na baba yenu wa tanganyika,kutaka muungano na znz,hebu na uvunjike hatuutaki kwani lazima
Nime-note kitu kimoja toka zamani kwenye chokochoko hii ya kutaka kujitenga.. Kwamba Wapemba wengi na Waunguja wachache wenye asili ya kiarabu ndo wanaonekana kuwa mstari wa mbele kutaka muungano uvunjike.. Waunguja wengi (na haswa weusi) wanaonekana wasiopenda suala la muungano kuvunjika.. Jee inawezekana kuna kikundi cha watu wachache wenye ajenda yao iliojificha..? Kwamba wanataka muungano uvunjike ili iwe rahici kuuvunja na uzanzibari..? Maana nimeshamsikia mpemba mmoja (na ni rafiki yangu na anapata riziki zake hapa bara) akidai angependa Pemba iwe Jamhuri na Maalim awe ni raisi wao.. Wako wangapi hawa (wapemba) wenye mawazo kama haya..?
Ndugu yangu wa damu kawepo Zanzibar kipindi cha mfungo. Mji mzima utakula wapi? Utanunua kitu cha kula wapi? Alibembeleza kununua maji ya kunywa kwa mwenye duka mmoja na hadi alipokubaliwa akaambiwa atafute chombo awekewe maji. chakula utapata hoteli za kitalii tena kwa tsh elf 15 kupaa, kisa mfungo! Halafu tunadanganywa kuwa wakati wa mwezi wa ramadhani hata wakristo hufunga kuwaunga waislam mkono. Kufunga kwa kulazimishwa?
Yalishatabiriwa hayo. Muungano ukivunjika haitaishia hapo. Hawa wapemba na hawa waunguja. Na hawa wenye asili ya kiarabu ndio wenye chokochoko zaidi
Na sasa kama wazanzibar wanaongelea tumboni tu na hawana kiburi cha kuhitimisha Muungano, basi na waache chokochoko wanazowafanyia watanganyika walioko visiwani. Nao wanatafuta kama wapemba na waunguja wanavyotafuta huku Bara. Period!
Angalizo tuu:Sema Dini Zao (kuna dini nyingine)+kujipeleka??Hii haimaanishi kunaoondoa haki ya msingi ya kikatibaIkiwa umefika nchi ya watu wakiwa na dini yao, mila zao na utmaduni wao unatakiwa ufuate sheria sio ulalamike, kwani ulilazimishwa kwenda huko Znzbar si ulijipeleka mwenyewe.
Pole sana mkuu hujui kama Znz ni nchi nyengine na sio Tanzania.
Ikiwa umefika nchi ya watu wakiwa na dini yao, mila zao na utmaduni wao unatakiwa ufuate sheria sio ulalamike, kwani ulilazimishwa kwenda huko Znzbar si ulijipeleka mwenyewe.
Pole sana mkuu hujui kama Znz ni nchi nyengine na sio Tanzania.
Tuwache kueneza propaganda zisizo na ukweli, mimi nilikuwepo Zenji karibu miezi 4 hv na hiyo mikutano na mihadhara inaendeshwa na Waznzbari weusi na wala sio waarabu kama tunavojisemea uongo tukiwa huko Tanganyika na kiongozi wa hiyo mihadhara ni jamaa yake Shamhuna wa damu anaitwa SHEIKH MSELEM ALI ambae ndie mwenyekiti wa hiyo Jumuia ya UAMSHO (jamaa huyu anashahada ya mambo ya anga na anapoongea wewe mwenyewe unahisi kama huyu jamaa kichwa chake kinatuma na ni mtaalamu mambo ya kiislam), hebu Watanganyika wenzangu tusiwe wavivu kufuatilia haya mambo huku Zenji ikiwa tunataka kuwaelewa hawa jamaa tusikurupuke na kutoa pumba zetu za kitoto.
Na ktk jumuia hiyo wapo baadhi ya viongozi wenye asili ya kiarabu kama AZAN na FARID, na hii ndio hali ya visiwa vyote ulimwenguni, sio ZNZ tu.
Na ukweli uko pale pale WAznzbari takriban 78% hawautaki huu muungano na naamini kura ikipigwa leo hii basi wenye kutaka muungano hawatozidi 15%.
Hili ninalisema kwa ushahidi nilioupata hapo Zenji na huko kwa Wapemba ndio kabisaaa mambo hayasemeki.
TUSISIKILIZE PUMBA ZA HAPA JF NA NYINYI NENDENI MKAJIONEEE WENYEWEE