TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,836
Habari za Alhamisi ndugu zangu?! Bila Shaka mu bukheri wa afya.
Leo ninaelekea upande wa watangazaji, inazidi kunisikitisha namna fani hii inavyozidi kudharaulika kila kukicha, ama ukubali au ukatae uhalisia upo wazi kabisa.
Watangazaji sidhani kama wanazingatia vigezo vya utangazaji siku hizi. Nitakupa mifano michache.
-Kipindi cha The base show ITV
-Kipindi cha 5 Selekt Channel 5
-Kipindi cha Climax Tv One
-Watangazaji wote wa Clouds Fm
Ninashangazwa na namna wanavyotangaza, uvaaji wao yaani wahuni wameongezeka sana katika kada ya utangazaji, hivi kweli hayo ndio maadili ya Watangazaji au ndio utandawazi unazidi kuharibu fani mbalimbali za Tanzania?!
Yaani unakuta mtangazaji amenyoa bonge la jogoo, kavaa mnyonyo yaani nguo za Dada zao kwa wanaume na kwa wanawake Watangazaji ndio hatari kabisa. Namna wanavyoongea wenyewe wanaita Swagger kama huyo aitwaye Tbway au yule wa Kipindi cha Friday Night..
Yaani fani imezidi kuharibika sana na hakika siamini kama kweli kuna wasomi kati yao, wanaonekana kama ni wahuni waliotolewa mtaani na kupelekwa kutangaza.
Hali hii inanisikitisha sana kwa kweli, sijasoma uandishi wala utangazaji ila kama mchambuzi na mfuatiliaji wa baadhi ya mambo hakika sipendezwi na namna hali inavyozidi kuwa mbaya.