Baadhi ya wana JF shule hawajaenda japo darasani wameingia

Prosper C Manasse

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
635
690
"Kuingia darasani sio kwenda shule"

Falsafa hii inathibitika pale yule anayejiita msomi anaposhindwa kujitambua katika jamii wakati jamii inamtambua kama msomi.

Napenda kutoa pongezi kwa wana JF wote wanaojitambua na kutimiza wajibu wao kwa nafasi zao katika jamii ikiwemo kulitumia jukwaa hili vyema ipasavyo.

Chakushangaza mambo haya hufanywa na watu wanajiita wasomi na pia ni watu ambao hutegemea kuitwa viongozi katika jamii yetu.

Sheria za jukwaa zipo wazi kuhusu kuzuia matusi, kejeli ama kusanifu watu na mambo mengine kama hayo lakini watu tumekuwa wajinga japo tunajiita wasomi.

Jambo ambalo tunapaswa kulitambua ni kwamba,

"The threads u post identfy urself while ur comments determines ur thinking capacity.

Kutokana na wengi wetu kutumia majina feki tumejikuta tunafanya vitu ambavyo si vyema na kujikosea heshima lakini kutumia jina feki kwa kujificha ili kutusi, kukejeli, kudharau, kutapeli na mengineyo, hakuondoi uhalisia wako zaidi ya kujitia aibu moyoni mwako mwenyewe.

Nini tatzo la wengi wetu.

Wengi wetu huwa hatupost chochote lakini tunasubiri wengine wapost ili tuwatusi, tuwakosoe, tuwaite wajinga, matapeli, hawajasoma na mengineyo.

Sasa kama wewe si mjinga wala si tapeli na pia umesoma sana, mbona hatuoni post yako hata moja japo hatq mara moja tu kwa mwezi?

Matokeo yake unaishia kuona post za wengine za kijinga kwa kukoment matusi ama maneno ya dharau kwa wengine.

Nini tofauti zetu humu.

Tofauti kubwa chache na muhimu ambazo watu wachache tunazo na wengi wetu hatuna zipo katika mambo machache sana lakn muhimu.

Kujitambua,

Nidhamu

Hekima,

Busara,

Yote haya hayapatikani darasani bali hutokana na uzoefu wa maisha pamoja na hofu ya Mungu.

So kama mimi nawe hatuna mambo hayo tajwa hapo juu lakini tunaelimu kubwa na pesa nyingi, basi elimu na pesa zetu zinatusaidia tu kupata ugali na lakini jamii ilojaa welevu bado itatuona wajinga tusiye maana.

Nini tunakaribiana ama kulingana.

Ukiangalia kwa haraka, wengi wetu humu tunalingana ama kutofautiana kwa mstari mwembamba sana kama vile.

*Viwango vya elimu,(taaluma)

*Vipato vyetu,

*Makazi,

*Uelewa,

Yote hayo tunakaribiana, sasa inakuwaje umuone mwenzako mjiiinga eti kisa hukubalianinae?

*Wapo kwao wanaitwa wajinga hapa.

*Wapo ambao walishatelekeza familia zao kwa anasa.

*Wapo walochezea fursa kama vile tuwaonavyo baadhi ya PHD hoders wajinga.

Wapo ambao hukosoa wengine lakini maisha yao magumu.

Lakini tukikutana humu kia mmoja wetu anajifanya anajua kukosoa na kuwaona wengine wajinga badala ya kujifunza jambo na na kutoa mchango wenye tija jukwaani.

Nidhamu inamisingi mitatu.

1. Kujitambua.

2. Kusoma mazingira na alama za nyakati.

3. Kufuata maelekezo.

Ukikosa moja kati ya misingi hiyo ni lazima utakuwa mtovu wa nidhamu katika nyanja zote.

WanaJF, thibitisheni elimu zenu kwa kuzingatia misingi mi3 ya nidhamu ambayo itawapa faida ya kuwa waadifu katika jamii, pia msisahau kuwa na hofu ya Mungu ambayo itawapa faida ya hekima na busara ili tuisaidie jamii kwa elimu au pesa tulizonalo badala ya kuacha mambo muhimu na kuwatolea wengine matusi.

Si vyema kuudharirisha utu wako na nafasi yako kwa kuwatusi wengine, kumbuka kabla ya elimu ulonayo ulipewa akili so usiidharau na kuidharirisha akili yako kwa kigezo cha kuitanguliza elimu yako.Kama wewe ni mmoja wao na nimekukwaza basi pole maana ukweli ndiyo pekee husimama pekee bila support.
 
Umenena vema Mkuu! Ila hawa wanaotukana Ni Rika flani Hivi, Ni kizazi kilichoanza kutumia mtandao Ni Miaka miwili iliyopita.

Ukirudi Nyuma Miaka miwili , tuseme hata 2013 JF haikua Hivi Kabisa. Kuna kizazi tu kimeibuka Hivi karibuni kinatuharibia!
Sijui Tukipe Jina Kizazi Gani Maana Naona Kinazidi Cha Nyoka
 
Umenena vema Mkuu! Ila hawa wanaotukana Ni Rika flani Hivi, Ni kizazi kilichoanza kutumia mtandao Ni Miaka miwili iliyopita.

Ukirudi Nyuma Miaka miwili , tuseme hata 2013 JF haikua Hivi Kabisa. Kuna kizazi tu kimeibuka Hivi karibuni kinatuharibia!
watakuwa na ndio hapo.... labda wataacha, wamenifunza na mie kutukana maana huwa mtu anaanza kutukana tu badala ya kujibu hoja .......
 
Jf kila mtu anajiona mkubwa kiumri especial wewe mtoa mada.
embu fikiri.. kama kutakuwa hakuna kizazi kinachokuja na kurithi unafikiri nyie mnaojiona wakubwa kiumri mkishakufa na Jf si ndio itakuwa imekufa?

au tugome tuwaachie mtandao wenu nyie mnaojiita wakubwa kiumri mtumie wenyewe? (just kidding)
 
Back
Top Bottom