Baadhi ya vingozi kuanza kutowaamini madaktari Muhimbili, nini hatma yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baadhi ya vingozi kuanza kutowaamini madaktari Muhimbili, nini hatma yake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mcfm40, Jul 29, 2012.

 1. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,023
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu, kwa siku za karibuni inaonekana wazi baadhi ya watu na viongozi wa serikali wamekuwa wakigwaya kwenda kutibiwa Muhimbili. Kwa tetesi zilizopo licha ya baadhi ya askari na watu wa usalama wa Taifa kuwa na hofu kubwa kuhusus kupelekwa muhimbili pindi wapatwapo na ajali au kuugua, ina semekana kwamba wengi wa viongozi sasa hasa wa CCM wana kwenda hospitali za binafsi hasa Agakhan na Regency, kwa madaktari wanaowaamini tu! Hii inaonekana ni kwa kile kitendo chao cha kufurahia kupigwa ulimboka na kuwadhihaki madaktari. Pia inaelezwa kwamba sababu nyingine ni hofu kuhusu mgomo baridi unaondelea sasa katika mahospitali yetu, hasa kutokana pia na kufukuzwa baadhi ya madaktari na madaktari wanafunzi kwa kudai maboresho katika sekta ya Afya.

  Je hii hali ya kutoamiana kati ya "wagonjwa' na madaktari iliyotengenezwa na serikali itaendelea mpaka lini? Hata wananchi wa kawaida siku hizi huwa hawana imani na tiba wanazopewa hospitalini km kweli ndio best possible ya matibau wanayoweza kupata kutoka kwa madaktari wao! Hii inatokana na kinyongo ambacho bado madaktari wamebaki nacho!

  Je serikali inalijua hili na ni nini wanachofanya kuhakikisha watu wa kawaida na viongozi hasa wa CCM wanarudisha imani kwa madaktari wetu? Na ni nini serikali inafanya kuhakikisha wanamaliza kinyongo na manunguniko waliyonayo madaktari ili warudishe moyo wao wa kufanya kazi kwa ufanisi na kujtolea?

  Njia ya kutumia nguvu na vyombo vya dola kama mahakama kweli inaweza kurudisha ari, kuaminiana na kujitolea kwa madaktari wetu katikas kuokoa maisha ya watanzania? Tunaomba serikali imalize huu mgogoro na madaktari na washikane mkono na "tuwaone kwenye picha na TV wakicheka" kwa ajili yetu sisi wagonjwa kuturudishia imani hasa na madaktari wetu wa muhimbili ambapo ndipo penye rufaa ya maisha yetu. Imefikia mahali hata ndugu yako akipewa rufaa ya muhimbili roho inakudunda! Tafadhali serikali hebu turudishieni amani ya roho! Tafadhali sana tunaomba sana!
   
 2. a

  artorius JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hali ni mbaya,baadhi ya wabunge kutoa lugha ya kuudhi na kejeli ndio iliyochangia kuzorota kwa huduma za afya
   
 3. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,026
  Likes Received: 9,389
  Trophy Points: 280
  Kiongozi gani ulishaona akienda tibiwa Muhimbili aisee wakati APPOLO ndiyo karibu kushinda muhimbili.
   
 4. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,716
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  pale ni Mtakuja Hospital
   
 5. Xidian

  Xidian JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hata juzi shemeji yake ****** mbona walimleta Muhimbili na akafariki siku moja baadaye? Muhimbili ni mtakuja tu hata walete kiburi kipi maana kabla hata hawajaenda Appolo lazima wapitie hapo.
  Wamasema Lugalo eti imependishwa hadhi na kuwa referral hospital , je kwanini bado wanapeleka wagonjwa Muhimbili ? Siasa za kibabe sio siri inatuua watanzania
   
 6. k

  kigogo2011 Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr ni mchawi mtaalamu, akiamua kukufanyizia hata ukafanye postmortem wapi hauwezi jua chanzo! cheza na daktari wewe! ila maadili ndo yanawalinda.
   
 7. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 14,450
  Likes Received: 6,122
  Trophy Points: 280
  ni hofu ya viongozi isiyokuwa na msingi.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 8. Micro E coli

  Micro E coli JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 940
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu hilo unalosema ni kweli dawa hizihizi i can use it and kill ukafa kifo chema bila kufurukuta na hakuna DR anaweza fanya post mortam na kugundua kabisa.
   
 9. Andy1

  Andy1 Senior Member

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sure mkuu umenena vema na naomba nikuunge mkono kwa hili maana hali imekua mbaya zaidi kwa askari wetu hasa wa usalama wa taifa imetokea jana nilikua hospitali moja binafsi natafuta matibabu akaletwa mama mmoja mjamzito kwenye kadi ya clinic ilionyesha huyu mama ni askari na mme wake ni usalama wa taifa kutokana na vyumba kujaa pale ma dr na manes wakawaambia waende muhimbili kwa kweli jamaa alikataa na akawa analia anasema mhn wakimjua ni usalaama wanaweza wakamzembea, sijajua ishu iliishaje maana jamaa alikua analia mi nikawa nimeondoka lakini inaonyesha still kuna hali tata kati ya mdr na askari kitu ambacho inabidi kishughulikiwe mapema
   
 10. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,591
  Likes Received: 9,524
  Trophy Points: 280
  ndio LIWALO LISHAKUA HILO MKUU......
   
 11. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,197
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana. We mfano kuna kijana mmoja (ni mfanyakazi wa UDOM-Tutorial Assistant-Anaitwa Juma Mbega) aliwahi kusema facebook kama angekuwa rais basi Dr wote angeweza kuamrisha wakatwe vichwa. Na baada ya siku chache Dr Ulimboka akapigwa. Sasa je mtu kama huyu akiugua hata hospital binafsi akikutana na Dr watakuwa na moyo wa kumtibu? Na je kama yeye aliamini kuwachinja Dr ni suluhisho vipi imani yake kwa hao Dr? Ukweli inasikitisha sana kwa watu wa CCM!
   
 12. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hofu ya bure, madaktari si watu wa vinyongo, ila wanasia.. Ndio wenye kuweka moyoni visasi!
   
 13. M

  MTZmakini Member

  #13
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waswahili husema, mtu ukiwa hujashikwa na haja huoni thamani ya choo, ni sawa pia na mtu ukiwa huna matatizo ya afya huoni maana ya Hospitali na thamani ya daktari. Hawa wote wanaokebehi madaktari ngoja waugue ndiyo watajua nini maana ya hospitali kuwa na vifaa vya kutibu na nini maana ya daktari. Inasikitisha sana suala la madaktari linavyochukuliwa kisiasa, mpaka watu wanaamua kumtesa daktari wakidhani madai yao yanamkono wa siasa. Haya sasa wameshalikoroga hofu inawapanda kwenda kutibiwa Muhimbili, bahati mbaya kwao MUHIMBILI NI MTAKUJA, iko kazi.
   
 14. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 4,982
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  umeniwahi mkuu. Muhimbili ni mtakuja. Watazunguka weee huko kote baadaye wanatua mnh! There is every one there isipokuwa vifaa tu. Hata huko wanakokimbilia wanawategemea watu wa mnh. Hii vita wanasiasa waliianzisha na madaktari hawataimaliza haraka. Hospitali zote hapa mjini zinategemea emergency ya mnh.
   
 15. m

  manucho JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa ubaya ubayani, akuanzae mmalize
  Hawa wanasiasa ukiwaambia ukweli hawataki wanataka kuleta siasa zao kwenye serious issue wanafikiri udaktari ni sawa na kupiga blablaa pale dodoma na jangwani, sasa kumpiga Dr. Ulimboka wameona wamemaliza OK fine and Gud.
  Labda wawafanye watoto wao wawe madaktari otherwise tutakutana ahera.

  Kuna haja ya kuanzisha shule ya Urais, Uwaziri, Ubunge, ukuu wa Mkoa, wilaya, kila kitu ili watu wawe wanaomba kazi kulingana na alichosomea na alivyofaulu. kazi itangazwe kama zinavyotangazwa kazi nyingine siyo kuweka mbumbumbu hizi matokeo yake ndiyo haya.
   
 16. M

  Mwl.wanaharakati Member

  #16
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua ukiwa Mama ni muhimu kuwa na mtoto. Na ukipata mtoto ni vyema akajua umuhimu wa mama. Yani mtoto akiwa mtoto anafahamu umuhimu wa mama lakini akiota tumavuzi anajiona amekuwa kumpita mama. Yani wadau wote tujue kwamba hawa Madaktari ndo walio tufanya tuzaliwe bila matatizo. Kama hv leo tunawafanyia v2 vya upumbavu wakidai haki zao za msingi kweli haki kweli. Wanakimbilia hospitali za watu binafsi si wanajua wamelikoroga na walinywe tu. Usimtukane mama kwa maana hujui amekutunzia siri ngapi. Sasa serikali itambue. Watu kama Madaktari ndo wameshikilia maisha ya walipa kodi, wapiga kura na wengi wanaoibiwa haki zao. Watakuja tu jamani.
   
 17. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani Huko AGHAKHAN na REGENCE wapo akina NANI kama SIO haohao wa MUHIMBILI? na HATA kama SIO si ndo hao hao MACOLIGUE WAO? hakuna MUHIMBILI nyingine tanzania wataenda tu kutibiwa ndo Pale watakapochomwa Insuline na Kufa bila kutikisika kwa Hypoglycemia halafu nenda sasa ukafanye hiyo postmotam..


  Kiburi ni Tabia ya shetani na viongozi wa aina hiyo ni nashetani tu.
   
Loading...