Baadhi ya Nyakati Ngumu alizovuka Hayati Magufuli

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Wakuu,

Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wetu shujaa John Pombe Magufuli. Hayati JPM ndiye Rais pekee hapa Tanzania aliyetawala kwa kipindi kifupi ( 5 years) lakini alifanya mambo mazito yaliyoshindikana miaka mingi kwa visingizio vingi. Nimeona nigusie mambo machache ambayo utawala wake ulipitia nyakati ngumu lakini kwa misimamo yake alivuka.

HUJUMA ZA KUPANDISHA BEI YA SUKARI

Wafanyabiashara wa sukari kwa makusudi walitengeneza uhaba wa sukari ili ipande bei kihuni. JPM mwenyewe alitoa onyo na kuagiza vyombo vyote vya usalama kuchunguza wanaoficha sukari na kuwachukulia hatua ya uhujumu uchumi. Ndani ya siku chache hali ilitulia, wananchi tukaona sukari imerejea madukani.

HUJUMA YA VITUO VYA MAFUTA KUPANDISHA BEI YA MAFUTA
Hapa pia mnakumbuka kuibuka kwa ghafla uhaba wa mafuta kwa wafanyabiashara hao kutaka kupandisha bei kinyume na maelekezo ya serikali. JPM mwenyewe aliagiza vituo ambavyo havitauza mafuta kwa bei elekezi vifutiwe leseni mara moja na haraka. Hali ilitulia, mafuta yakaendelea kuuzwa kama kawaida.

UGAIDI WA KUTISHA HUKO KIBITI
Hili ni tukio ambalo lilitesa wananchi wa kibiti na vyombo vya usalama. Viongozi wengi wa serikali za mitaa, mabalozi wa nyumba kumi na askari Polisi wengi walikufa kwa kuuawa kinyama kwa risasi au kucharangwa mapanga! Kibiti ikiwa kama haitawaliki na kutishia usalama wa nchi na hasa ukaribu wake na jiji kuu la nchi kibiashara na kiserikali.

Kutokana na ugumu wa operation yake. Vyombo vya usalama viliagiza marufuku vyombo vya habari kuripoti matukio ya huko. Ikalazimu majeshi yetu kuingia mzigoni kuendesha operations dhidi ya vikundi hivi hatari. Mengi yalitokea huko lakini ukafanyika usafi hadi wakakimbilia nchi jirani na kuzua songombingo kubwa na kulazimu majeshi ya nchi mbalimbali kuungana kuisaidia Msumbiji. Kibiti ikatulia shughuli za wananchi zikarejea.

HUJUMA DHIDI YA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA
Hii hayati JPM alishauriwa vizuri sana ingawa vita yake haikuwa nyepesi. Jirani yetu mmoja alimwaga majasusi akisaidiwa na mabeberu waliokuwa hawampendi tufanikiwe kutokana na namna mkuu wetu alivyokuwa anatawala. Mnakumbuka baadhi yao yaliyowatokea Airport na huko mipakani huku wataalam wetu wakipambana kizalendo kuthibitisha competitive advantages bomba likipita Tanga badala ya hapo jirani. Hatimaye tukashinda!

Hitimisho
Hayati JPM alikutana na vikwazo vingi sana vya ndani na nje kwenye harakati zake za kuijenga nchi yetu. Hapa nimegusia vichache sana ambavyo si maarufu ili kuchokoza mada. Tunajua yaliyotokea kwenye nyakati za COVID19, Madini, kuhamia Dodoma, ujenzi bwawa la Nyerere, SGR n.k

Hayati JPM alikuwa na mapungufu mengi lakini ana mambo mengi ya viongozi wa sasa wanapaswa kujifunza hasa kwenye udhubutu na kutoogopa chochote akidhamiria jambo. Nchi ilipita miaka mitano ambayo kila mwananchi atakumbuka daima kwa namna yake.

Roho ya Marehemu John Pombe Magufuli ipate rehema kwa Mungu apumzike kwa amani!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kukosekana kwa soko la korosho zilizonunuliwa na serikali
Hii ilikuwa big issue! Biashara huko nje zina wenyewe na alifikiri kwasababu ya mahitaji ya kisoko angefanikiwa kuuza.

Hapa alihujumiwa vibaya na kwa hulka yake ya ubishi asingetoboa. Hapa ilihitajika business intelligence sio maguvu! Another lesson kwa viongozi wetu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kenya kuzuia Tourist company's zetu kupokea wageni wao Jomo Kenyatta. Lakini pia zuio lao la miaka mingi kwa ndege za Tanzania kufanya biashara Kenya.

Ulitumika ubabe ikiwemo Kenya Airways kupunguziwa route za Tanzania! Baada ya negotiations na kuvutana sana hatimaye Air Tanzania inatua Kenya hadi leo baada ya miaka mingi ya vikwazo. Pia kupokea wageni zuio likaondolewa na kuwekwa utaratibu mzuri.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Leo ni kumbukumbu ya kifo cha Rais wetu shujaa John Pombe Magufuli. Hayati JPM ndiye Rais pekee hapa Tanzania aliyetawala kwa kipindi kifupi ( 5 years) lakini alifanya mambo mazito yaliyoshindikana miaka mingi kwa visingizio vingi. Nimeona nigusie mambo machache ambayo utawala wake ulipitia nyakati ngumu lakini kwa misimamo yake alivuka.

HUJUMA ZA KUPANDISHA BEI YA SUKARI

Wafanyabiashara wa sukari kwa makusudi walitengeneza uhaba wa sukari ili ipande bei kihuni. JPM mwenyewe alitoa onyo na kuagiza vyombo vyote vya usalama kuchunguza wanaoficha sukari na kuwachukulia hatua ya uhujumu uchumi. Ndani ya siku chache hali ilitulia, wananchi tukaona sukari imerejea madukani.

HUJUMA YA VITUO VYA MAFUTA KUPANDISHA BEI YA MAFUTA

Hapa pia mnakumbuka kuibuka kwa ghafla uhaba wa mafuta kwa wafanyabiashara hao kutaka kupandisha bei kinyume na maelekezo ya serikali. JPM mwenyewe aliagiza vituo ambavyo havitauza mafuta kwa bei elekezi vifutiwe leseni mara moja na haraka. Hali ilitulia, mafuta yakaendelea kuuzwa kama kawaida.

UGAIDI WA KUTISHA HUKO KIBITI

Hili ni tukio ambalo lilitesa wananchi wa kibiti na vyombo vya usalama. Viongozi wengi wa serikali za mitaa, mabalozi wa nyumba kumi na askari Polisi wengi walikufa kwa kuuawa kinyama kwa risasi au kucharangwa mapanga! Kibiti ikiwa kama haitawaliki na kutishia usalama wa nchi na hasa ukaribu wake na jiji kuu la nchi kibiashara na kiserikali.

Kutokana na ugumu wa operation yake. Vyombo vya usalama viliagiza marufuku vyombo vya habari kuripoti matukio ya huko. Ikalazimu majeshi yetu kuingia mzigoni kuendesha operations dhidi ya vikundi hivi hatari. Mengi yalitokea huko lakini ukafanyika usafi hadi wakakimbilia nchi jirani na kuzua songombingo kubwa na kulazimu majeshi ya nchi mbalimbali kuungana kuisaidia Msumbiji. Kibiti ikatulia shughuli za wananchi zikarejea.

HUJUMA DHIDI YA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA

Hii hayati JPM alishauriwa vizuri sana ingawa vita yake haikuwa nyepesi. Jirani yetu mmoja alimwaga majasusi akisaidiwa na mabeberu waliokuwa hawampendi tufanikiwe kutokana na namna mkuu wetu alivyokuwa anatawala. Mnakumbuka baadhi yao yaliyowatokea Airport na huko mipakani huku wataalam wetu wakipambana kizalendo kuthibitisha competitive advantages bomba likipita Tanga badala ya hapo jirani. Hatimaye tukashinda!

Hitimisho,

Hayati JPM alikutana na vikwazo vingi sana vya ndani na nje kwenye harakati zake za kuijenga nchi yetu. Hapa nimegusia vichache sana ambavyo si maarufu ili kuchokoza mada. Tunajua yaliyotokea kwenye nyakati za COVID19, Madini, kuhamia Dodoma, ujenzi bwawa la Nyerere, SGR n.k

Hayati JPM alikuwa na mapungufu mengi lakini ana mambo mengi ya viongozi wa sasa wanapaswa kujifunza hasa kwenye udhubutu na kutoogopa chochote akidhamiria jambo. Nchi ilipita miaka mitano ambayo kila mwananchi atakumbuka daima kwa namna yake.

Roho ya Marehemu John Pombe Magufuli ipate rehema kwa Mungu apumzike kwa amani!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Nidhamu maofisini ilijaa haswa,wahudumiwa tulipokelewa kama wafalme,kwa sasa hovyooo!
 
Back
Top Bottom