Baadhi ya Mawaziri katika serikali ya Rais Magufuli wameanzisha mgomo wa kimyakimya?

Habari za muda huu.

Ni muda sasa nimekua nikifuatilia utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya 5 na kiukweli nimejiridhisha kwamba baadhi ya mawaziri hawako "active" kama uongozi wa juu wa nchi unavyotaka. Hili limethibitishwa na Mkuu wa nchi Mh. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli wakati anaongea na baraza la biashara la Taifa kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Ni kama wameamua kunyamaza au "kumsusia" kazi zote Rais na Waziri Mkuu. Hili jambo si la afya njema katika uendeshaji wa Serikali na taasisi zake. Nitoe wito na kumshauri Mh. Rais ni muda mufaka sasa wa kufanya mabadiliko makubwa katika Baraza lako la Mawaziri kwa ustawi wa serikali unayoiongoza.

Ahsante na nakutakia kazi njema!
Ni kweli walikuwa na mgomo baridi wakiongozwa na moja ya viongozi waandamizi ambaye ni sehemu mhimu ya mwili ambaye ..........................collective responsibility ilikuwa kitendawili kipindi hicho.
1. Kichwa
2. Kifua
3. Tumbo
4. Mikono
5. Miguu

*Code: Kunusa, kugusa, ladha ya ulimi, kusikia, kuona na akili pambanuzi
 
CCM inaweza kuigeuka dola au dola kuigeuka CCM ? kwangu mimi sioni dalili yoyote kwa mfumo uliopo sasa kwamba Rais akiutaka urais hakuna wa kupinga.
 
Back
Top Bottom