Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Baadhi ya mabweni ya Wanafunzi wa kike pamoja na stoo ya Shule ya Sekondari ya Jenista Mhagama iliyoko Halmashauri ya Songea Mkoani Ruvuma yameharibika kwa kuwaka moto siku chache zilizopita na kusababisha hasara ya mali.
Baadhi ya vitu vilivyoharibika ni matranka na vifaa vya Wanafunzi, huku kukiwa hakuna Mwanafunzi aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Inadaiwa moto huo ulitokea Usiku wa Saa Nane ambapo sauti za Wanafunzi waliokuwa wakipiga kelele zilisikika wakisema "moto, moto” na waliotoka nje wakashuhudia moto huo hali iliyozua taharuki miongoni mwa Wanafunzi.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi, lakini inadaiwa kuna Mtu alihusika kwa makusudi kuchoma majengo hayo.
Inadaiwa kuwa mtu anayedhaniwa kuhusika na tukio hilo alikuwa akivizia nyakati ambazo Wanafunzi hawapo bwenini ndipo alipotekeleza kitendo hicho cha kuchoma majengo.
Shule hiyo ina majengo mbalimbali takribani 126
Majibu ya Mkuu wa Wilaya ~ DC Songea: Mwanafunzi amechoma moto shule ili ifungwe apate nafasi ya kupumzika