Baadhi ya magari ya serekali kutumika nje ya vituo husika

Mroojr

Member
Nov 15, 2010
65
8
Jamani watanzania wenzangu labda mnisadie kunifahamisha hili huenda ufahamu wangu ni mdogo. Mfano mdogo tu, serikali ya Mkapa ilijitahidi kugawa magari ya wagonjwa ktk kila zahanati za tarafa zaidi vijijini ili kujaribu kuokoa maisha ya wagonjwa waliozidiwa kwa kuwawahisha hospitali za mikoa na wilaya, lakini kila uchao tunayaona hayo magari ya wagonjwa yakiranda mjini nje kabisa na vituo vyao vya afya vya kila tarafa. Endapo mgonjwa atahitaji huduma ya gari hiyo ataipataje wakati haipo ktk kituo husika? Je huu kweli ni utaratibu mzuri wa matumizi ya magari ya umma? Mambo haya yanatokea zaidi mikoani sijui kwa walioko Dsm.
 
Waliokabidhiwa hayo magari peke yao can't be trusted, kwanza ukiwa na mgonjwa unaombwa pesa za mafuta!
 
Back
Top Bottom