Baadhi ya kanuni za kudumu za bunge zinakinzana na katiba- hoja

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Inavyoelekea uwezekano wa kuyaona mapambazuko kwasasa haupo-angalau mpaka miaka mitano ijayo. Katika hali hiyo, tegemeo pekee tulilonalo ni hao wenzetu wakina Mbowe, Lissu, Mnyika n.k waliofanikiwa kupenya kwenye tundu la sindano na kuwa wabunge.

Kwa wadhifa wao huo tunaamini watakuwa na fursa nzuri ya kuibana serikali kuachana na ubadhirifu ili rasilimali za nchi zitumike kwa faida ya wananchi wote. Wasiwasi nilionao ni hizi kanuni za kudumu za bunge, ambazo baadhi yake zinampa uwezo mkubwa spika, wa kuwabana wabunge kiasi cha kusababisha washindwe kutimiza wajibu wao.

Tuchulie kwa mfano hii kanuni inayomtaka mbunge kabla hajawasilisha hoja yeyote bungeni, haiwasilishe kwanza kwa spika, aipitie ndipo amuruhusu mbunge huyo kuiwasilisha bungeni. Hivi kweli kanuni hii ina mantiki yeyote, ikitokea spika wa bunge akawa kibaraka wa serikali iliyoko madarakani, (na kuna uwezekano mkubwa hilo likatokea safari hii) itawezekana kweli spika wa aina hiyo akaruhusu mbunge kuwasilisha hoja inayoikaba kweli kweli serikali! Kama hilo aliwezekani nini maana ya kuwa na bunge?

Kwa mujibu wa ibara ya 62(2) ya katiba yetu bunge ndicho chombo chenye madaraka ya kusimamia serikali kwa niaba ya wananchi; bunge inawezaje kutekeleza jukumu hilo ikiwa mbunge mmoja mmoja hawezi kuanzisha hoja bila ya kuwa na kibali cha spika. Ni rai yangu kanuni hiyo na nyinginezo za aina hiyo zinakinzana na katiba yetu na hivyo ziondolewe.
 
Back
Top Bottom