Baada ya vita ya Ukraine, Nchi za Afrika zinatakiwa kupata Mateso Makali ya Kiuchumi kutoka kwa EU & USA

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,171
Vita ya Ukraine endapo itamalizika salama nchi za Afrika zinatakiwa kupata mateso makali kwa sababu zimeonekana Kumuunga mkono dikteita Putin dhidi ya uvamizi wake kwa nchi ya Ukraine.

Nchi za Afrika zikiongozwa na Senegal, Afrika kusini, Mali, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Nigeria, zinatakiwa kukatiwa misaada yote ya kiuchumi kuanzia elimu, afya, miundombinu, kupambana na Ugaidi, Njaa, ulinzi ili zitie adabu na iwe fundisho kwa watu wote Wanaosapoti madikteita duniani.

IMF & WB zinatakiwa kupunguza mikopo kabisa kwa nchi za Afrika ili zijitegemee au zikakopeshwe na Bank of Russia na China.

Misaada ya Vifaa tiba, madawa, teknolojia na mingineyo ya taasisi mabali mbali (USAIDS, ICAP, MDH , WORLD VISION, TASAF n.k) za kupambana na magonjwa hatari kama ukimwi, cancer, kisukari, pressure, ini, figo, Malaria inatakiwa kupunguzwa ili nchi za Afrika zipate akili.

Nchi zote zilizo piga kura ya hapana kwa Urusi, zinatakiwa kukatiwa misaada yote moja kwa moja ili zikafadhiliwe na Urusi.

Nchi zote ambazo hazikupiga kura zikiongozwa na Tanzania, zinapaswa kupunguziwa misaada kwani kutopiga kura ni kuogopa na ina maanisha wanakubaliana na Putin anachokifanya Ukraine.

Marais wote wa chi za Afrika ambao wameficha fedha zao Ulaya, zinatakiwa kutahifishwa kwa sababu hizo fedha ni kodi za wananchi.

Viongozi wote wa nchi za Afrika hakuna kwenda kutibiwa Ulaya, watibiwe kwenye nchi zao.

Wakimbizi wote kutoka Afrika kwenda Ulaya wawekewe sheria kali za kuwazuia kuvuka kwenda Ulaya kuliko na maisha mazuri, wabaki Afrika, wawe wakimbizi kwenye nchi za bara lao.

Rais Ramaphosa, Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Rais wa Cameroon, Rais wa Senegal, Rais wa Nigeria hawatakiwi kuendelea kubaki madarakani kwa sababu wanamuunga mkono Putin.

USA & EU zinatakiwa kukata kabisa misaada kwenye nchi za Kiislamu zote duniani, kwani nchi hizo zinamuunga mkono Putin na zinajinasibu kuwa na utajiri wa mafuta, Putin atazipatia misaada.

Baada ya hatua hizi kuchukuliwa nchi zote zinazosapoti udikteita zitakuwa zimepata somo.

Bara la Afrika linatakiwa liendelee kubaki kwenye lindi la umasikini kwa sababu viongozi wa nchi za Afrika ni wanafiki na waliowengi wanapenda udikteita na hawako tayari kuleta mageuzi ya haki kwa ajili ya maendeleo ya bara la Afrika.

View attachment 2270692
 
Marais wote wa chi za Afrika ambao wameficha fedha zao Ulaya, zinatakiwa kutahifishwa kwa sababu hizo fedha ni kodi za wananchi.

Viongozi wote wa nchi za Afrika hakuna kwenda kutibiwa Ulaya, watibiwe kwenye nchi zao.

Wakimbizi wote kutoka Afrika kwenda Ulaya wawekewe sheria kali za kuwazuia kuvuka kwenda Ulaya kuliko na maisha mazuri, wabaki Afrika, wawe wakimbizi kwenye nchi za bara lao.
 
Sasa unahubiri Nini hapo? Huoni kuwa unajichanganya? Tumia akili Yako vema!

Unapinga udikteta halafu unashauri hatua Kali zichukuliwe dhidi ya nchi ambazo zilitumia haki Yao kidemokrasia kupiga kura kwenye Baraza la umoja wa mataifa!

Kama kura zilipaswa kuwa za aina Moja, msingi wa kura ni Nini? Yaani unipe karatasi nipige kura nitakavyo halafu baadaye uje uniwajibishe Kwa aina ya kura nitakayopiga? Una akili kweli? Si ndio udikteta Huo huo unaojaribu kuukemea?

Tumia Kichwa chako vizuri, Kichwa sio Kwa ajili ya kubebwa macho na masikio Yako tu!
 
Marais wote wa chi za Afrika ambao wameficha fedha zao Ulaya, zinatakiwa kutahifishwa kwa sababu hizo fedha ni kodi za wananchi.

Viongozi wote wa nchi za Afrika hakuna kwenda kutibiwa Ulaya, watibiwe kwenye nchi zao.

Wakimbizi wote kutoka Afrika kwenda Ulaya wawekewe sheria kali za kuwazuia kuvuka kwenda Ulaya kuliko na maisha mazuri, wabaki Afrika, wawe wakimbizi kwenye nchi za bara lao.
Kisa waafrica wametumia haki Yao ya kidemokrasia kupiga kura kama watakavyo huko UN!🤣🤣
Hata hamuelewi mnatetea Nini!
 
Sasa unahubiri Nini hapo?Huoni kuwa unajichanganya?Tumia akili Yako vema!
Unapinga udikteta halafu unashauri hatua Kali zichukuliwe dhidi ya nchi ambazo zilitumia haki Yao kidemokrasia kupiga kura kwenye Baraza la umoja wa mataifa!Kama kura zilipaswa kuwa za aina Moja,msingi wa kura ni Nini?Yaani unipe karatasi nipige kura nitakavyo halafu baadaye uje uniwajibishe Kwa aina ya kura nitakayopiga?Una akili kweli?Si ndio udikteta Huo huo unaojaribu kuukemea?
Tumia Kichwa chako vizuri,Kichwa sio Kwa ajili ya kubebwa macho na masikio Yako tu!
Hakuna haki yeyote, mtu anavamia nchi ya watu analipuwa na Kupiga Mabomu alafu mtu anaona ana haki ya kufanya hivyo, hicho kitu hakipo ni lazima wale wote wanaomuunga mkono Putin wawajibishwe .

Hatuwezi kuendelea kulea udikteita, dunia inahitaji Demokrasia.
 
Sisi wenyewe hatujitambui kutwa kuokoteza mitumba yao na kila siku kwenda kuombaomba tu kwao

Nasema hata wakitengeneza simu wakaweka sumu ili tufe wote sawa tu maana hatutaacha kuomba
Hao haki za binadamu na hizo sheria zao ndio zinawafanya wasaidie wazembe wa kutumia akili

Potelea mbali liwalo na liwe
Wakate kila kitu akili itukae sawa
 
Hakuna haki yeyote, mtu anavamia nchi ya watu analipuwa na Kupiga Mabomu alafu mtu anaona ana haki ya kufanya hivyo, hicho kitu hakipo ni lazima wale wote wanaomuunga mkono Putin wawajibishwe .

Hatuwezi kuendelea kulea udikteita, dunia inahitaji Demokrasia.
Hivi akili Yako inafanya kazi kweli? Sasa kama Dunia inahitaji demokrasia, kwanini uiwajibishe nchi Kwa kutumia hiyo hiyo demokrasia kupiga kura? Kura ipo Kwa ajili ya Nini kama Matokeo yanatakiwa yawe ya aina Moja? Sisi kama Tz, tulichagua kutofungamana na upande wowote inapotokea mzozo kwa mataifa haya makubwa, huu ndio msimamo wetu kama nchi! Sasa aje mtu atulazimishe tufanye atakavyo, hiyo ndio demokrasia?Demokrasia haitetewi kwa kukiuka demokrasia!
Yaani utumie udikteta kuimpose demokrasia, unakuwa unafanya Nini?
 
Sisi wenyewe hatujitambui kutwa kuokoteza mitumba yao na kila siku kwenda kuombaomba tu kwao

Nasema hata wakitengeneza simu wakaweka sumu ili tufe wote sawa tu maana hatutaacha kuomba
Ni haki za binadamu na hizo sheria zao ndio zinawafanya wasaidie wazembe wa kutumia akili

Potelea mbali liwalo na liwe
Wakate kila kitu akili itukae sawa
Wakate kabisa haiwezekani wawe ndumila kuwili, sijawahi kuupenda unafiki, inatakiwa ujitambulishe ni black au white basi.
 
Wengi hawakupiga kura ni wanafiki tu, wanasubiria atakayepoteza ndo watembee naye, ilo halikubaliki.
Halikubaliki Kwa nani? Labda kwako na ufinyu wako wa fikra, nchi ambazo hazijapiga kura hazitaki kujiingiza kwenye mzozo na upande wowote! Hiyo Inamaana baada ya vita tutaendelea kushirikiana na wote!

Kwanza Africa tuna matatizo mengi tu, halafu tujifanye kiherehere wa kuchagua upande! Tudeal na ya kwetu,hao wenye uchumi mkubwa acha washughulikie hayo ya vita! Sisi tuwaze kupambana na umasikini, maradhi na Ujinga halafu tuongeze na Vita, hell no!
 
Hivi akili Yako inafanya kazi kweli?Sasa kama Dunia inahitaji demokrasia,kwanini uiwajibishe nchi Kwa kutumia hiyo hiyo demokrasia kupiga kura?Kura ipo Kwa ajili ya Nini kama Matokeo yanatakiwa yawe ya aina Moja?Sisi kama Tz,tulichagua kutofungamana na upande wowote inapotea mzozo kwa mataifa haya makubwa,hui ndio msimamo wetu kama nchi!Sasa aje mtu atulazimishe tufanye atakavyo,hiyo ndio demokrasia?Demokrasia haitetewi Kwa kwa kukiuka demokrasia!
Yaani utumie udikteta kuimpose demokrasia,unakuwa unafanya Nini?
Kutofungamana na upande wowote ni unafiki na uchawa, maana yake unaogopa kuweka msimamo wako wazi.

CCM mnajulikana kwa udikteita, mnatumia hadi kuiba kura za wananchi, kutopiga kula maana yake mnakubaliana na Putin kufanya Uvamizi Ukraine, Kwhy inabidi mpunguziwe misaada ili akili iwakae sawa na mtambue kwamba udikteita hauna maana.
 
1. WB na IMF haziwezi Kufanya hivyo kwasababu hazimilikiwi na Nchi Moja au Mbili au Bara, Zenyewe zinajiendesha kutokana na Michango ya wanachama na Bonds! Japo Marekani na Ulaya ni wadau Wakubwa kwny hii mifuko

2. Pili Hizo Nchi ulizozitaja Haziwezi kujiendesha hata kwa Mwaka mmoja tu kama Wakilikosa Soko la Africa, Maisha yatakua Bei Juu sana Kwa karibia Kila kitu chao maana Makampuni Yao Yako huku kuhakikisha Maisha Yao kule yanaenda. The Future is in Africa.
 
Halikubaliki Kwa nani?Labda kwako na ufinyu wako wa fikra,nchi ambazo hazijapiga kura hazitaki kujiingiza kwenye mzozo na upande wowote!Hiyo Inamaana baada ya vita tutaendelea kushirikiana na wote!
Kwanza Africa tuna matatizo mengi tu,halafu tujifanye kiherehere wa kuchagua upande!Tudeal na ya kwetu,hao wenye uchumi mkubwa acha washughulikie hayo ya vita!Sisi tuwaze kupambana na umasikini,maradhi na Ujinga halafu tuongeze na Vita,hell no!
Huo ni unafiki kama umekukubali kushirikiana na mtu, lazima hata wakati wa shida uwe naye, ukishindwa maana yake wewe siyo rafiki wa kweli upo kwa lengo la maslahi tu.

Sasa nchi za Afrika Zinatakiwa zipunguziwe misaada kutoka US& EU, Russia naye yupo ataziba gap. Unafiki haukubariki kamwe.
 
1. WB na IMF haziwezi Kufanya hivyo kwasababu hazimilikiwi na Nchi Moja au Mbili au Bara, Zenyewe zinajiendesha kutokana na Michango ya wanachama na Bonds! Japo Marekani na Ulaya ni wadau Wakubwa kwny hii mifuko

2. Pili Hizo Nchi ulizozitaja Haziwezi kujiendesha hata kwa Mwaka mmoja tu kama Wakilikosa Soko la Africa, Maisha yatakua Bei Juu sana Kwa karibia Kila kitu chao maana Makampuni Yao Yako huku kuhakikisha Maisha Yao kule yanaenda. The Future is in Africa.
Nchi za Afrika zitatumia point yake ya pili kujikwamua zenyewe kama kweli sisi Africa ndo tunawafanya EU wawe hapo walipo, zikishindwa zitaelekea kwa Putin & China, lakini unafiki ukomeshwe.
 
Kutofungamana na upande wowote ni unafiki na uchawa, maana yake unaogopa kuweka msimamo wako wazi.

CCM mnajulikana kwa udikteita, mnatumia hadi kuiba kura za wananchi, kutopiga kula maana yake mnakubaliana na Putin kufanya Uvamizi Ukraine, Kwhy inabidi mpunguziwe misaada ili akili iwakae sawa na mtambue kwamba udikteita hauna maana.
Wewe utakuwa mtoto na hujui historia!Kasome kisa Cha Nyerere kuwaambia watanzania wakaze Mikanda!

Israel inachofanya huko Palestina, US alichofanya huko Afghan, Yugoslav na kwingineko, ni wapi ambapo tulichagua upande?

Tuliamua hatutafungamana na upande wowote, na Huo ndio msimamo wa nchi yetu!

Hii vita imekuja imetukuta tayari tuna msimamo wetu, Wala halikuwa jambo la kwenda kutafakari!

Baada ya vita, tutashirikiana na yeyote ambaye Yuko tayari! Ambaye hataki, ruksa kuondoka!
 
Huo ni unafiki kama umekukubali kushirikiana na mtu, lazima hata wakati wa shida uwe naye, ukishindwa maana yake wewe siyo rafiki wa kweli upo kwa lengo la maslahi tu.

Sasa nchi za Afrika Zinatakiwa zipunguziwe misaada kutoka US& EU, Russia naye yupo ataziba gap. Unafiki haukubariki kamwe.
Ili ujue kuwa mawazo Yako ni ya kijinga, hata EU na US hawajawahi kupendekeza hivyo! Na hilo jambo haliwezi kutokea, ni kama mnajifurahisha tu humu jukwaani!

Hao wenyewe waweka vikwazo wanaangalia maslahi ya nchi zao kwanza, kwanini waliweka vikwazo kwingine lakini sio kwenye gas ya Urusi? Kama ni urafiki wa shida na Raha, kwanini wasipeleke majeshi? Kwanini waondoe vikwazo kwenye Mbolea na chakula kutoka Russia na Ukraine? Hapo ni maslahi kwanza ya nchi Yako kabla ya chochote! Kuna wengine humo humo wanajifanya marafiki wanampa silaha Ili vita ichukue muda mrefu, baada ya vita Ukraine itakuwa na madeni ya muda mrefu kama Uingereza ilivyohenya kulipa madeni Kwa US!

Eti wananchi wako wafe Kwa njaa kisa US kakwambia muwekee vikwazo Urusi, Shwain!
 
Nchi za Afrika zitatumia point yake ya pili kujikwamua zenyewe kama kweli sisi Africa ndo tunawafanya EU wawe hapo walipo, zikishindwa zitaelekea kwa Putin & China, lakini unafiki ukomeshwe.
1. Unafiki wameuanza wao sisi tunamaliza, Wametutawala kimabavu, wametuua na Kutuibia Mali nyingi sana, wamevamia Nchi nyingi sana bila sababu kuiba Mali, Afghanistan, Iraq, Syria nk. nk.

2. Pili, Dunia inatakiwa iwe na Balance of Power, Africa itamsapoti yoyote atakayekua kinyume na wamagharibi Nikimaanisha Ulaya na Marekani Ili kuhakikisha kunakua na Balance of power. Kwa muda mrefu sana tumekua mateka maana hakuna anaeweza kumuwajibisha Marekani anapofanya Dhuluma. Ndo maana unaona anafanya anachotaka Duniani.

3. Tatu, Tunarudisha fadhila Kwa Urusi, wao walilisaidia sana Bara la Africa kujitawala na kupinga Ukoloni .
 
Back
Top Bottom