Baada ya uchaguzi, maisha yarejee

Baada ya uchaguzi, maisha yarejee

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Posts
5,909
Reaction score
10,562
Jamanii eeh, uchaguzi umeshamalizika salama, hongera kwa walioshinda na pole kwa walioshindwa. Wajipange wakati mwingine.

Mitandao ifunguliwe na shughuli ziendelee.

Hatuwezi kuendelea kuwa watumwa wa uchaguzi. Mambo yameshakamilika, maisha yarejee kwenye mstari wake.

Wanaohusika na mitandao tafadhali waifungue.
 
Niko hapa Star Park mji kasoro bahari (ingawa kulikuwa na matarajio ya Mzee Hashimu Rungwe kupitisha bahari ikielekea Dodoma lakini ndiyo hivyo tena...). Sasa jirani na meza 2 moja iko kulia na imejaa jamaa wanafurahia ushindi wa sunami... Nyingine iko kushoto ya jamaa wanaosononeka na kushindwa uchaguzi. Wote wanapiga maji vibaya wengine huku wakicheza, wengine huku wananungunika. Hata hivyo hawa walioshindwa inaonekana wako vyema kifedha kwani vinywaji vimejaa plus mbuzi choma, ndizi, mara kongoro mara mkia etc... Wenzao upande wa pili meza imeanza kuwa na chupa tupu na huduma imedorora. Jamaa mmoja wa meza iliyodorora akaona isiwe tabu akaja meza ya pili (naona wanajuana) kimbembe jamaa kuomba kinywaji jamaa akamnongoneza mhudumu, daah jamaa si akaletewa chupa kubwa ya maji ya Uhai??
 
Kwa kweli maisha lazima yaendelee .Mimi nasubiri Arusha iwe kama Ule mji uliotajwa sijui ni Toronto au
 
Huyo magufuli ameshashinda sasa, imetosha. Turudi kwenye shughuli zetu za kila siku.
Tunaendelea na shughuli zetu mkuu, hakuna anaeomboleza wala aliejifungia ndani ila waache watu wazungumze maana siasa ni sehemu ya maisha ya kila siku, kuhusu mitandao, msiwe na wasiwasi, mnaweza msifunguliwe tena ndio mtajua kishindo cha awamu ya sita ni nini, hakichagui ccm wala upinzani yaani
 
Back
Top Bottom