Baada ya Tabora Lowassa aunguruma Shinyanga

Baada ya Tabora Lowassa aunguruma Shinyanga

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
Kwa mahasimu wa Lowassa kwa habari zilizopo tu ni kwamba baada ya kupewa uchifu Tabora,asubuhi yaleo ameonekana Shinyanga Kahama.

Duru za kisiasa zinasema huku amekuja kwa kazi maalumu ya kupewa uongozi wa mila ya Kisukuma.

Kwa wale mahasimu wake jipangen tena,naona EL anazidi kutimua vumbi tu kila kukicha.

Kwa wana jamvi mliopo Shinyanga tunaomba mtupatie picha ya matukio mazima,ili kwa wale ambao hatuja udhuria sherehe hizo tuweze kuzipata kupitia jamvi.

Nawasilisha.
 
Mimi bado sielewi kabisa strategic plans za EL ziendavyo na nini matokeo yake baadae, am totally blind.
 
inasemekana anaaga wananchi , amepima upepo ameamua kuachana na siasa , kila la heri huko uendako ndugu lowasa , siasa siyo ajira .
 
Man of actions! anakubalika. Ni katiba tu inayoweza kumuengua ikiweka kigezo cha umri. Lakini kama siyo hivyo na issue ya mgombea binafsi ikawepo CCM wanaweza kuwa na kazi ya ziada. Maana huyu Mh. anapendwa na watu wengi. Wanaomchukia siyo wengi ki hivyo na kimtazamo inaonekana hawana hoja ya msingi
 
Tunafahamu ni jin7i gani wazee wa kimila walivyoathiriwa na umasiki huku kwetu siku hizi hata ukitaka upewe urithi ambao alistahili kupewa mdogo wako we kaa nao vizuri tu, hivyo kwasabdu ya kipato jamaa anatumia uzaifu huo kukuaminisha wewe na wengine wasiujua haya mambo kuwa jamaa anakubalika, jiulize Nyerere alipendwa na wazee wangaph mbona hakupewa iivi vyeo kwa kas4 hivi hata kule umasaini ambako yeye ni mgeni maana ye ni mmeru ni kweli kwana haku mzee wa heshima na anayejua mila zaidi na mkubwa zaidi yake, wako ila? Pesa. Kuwa makini
 
Lowasa amesha fanikiwa misikitini na makanisani, amehamia kwenye mila na makabila, nape hana ujanja tena, fisadi kupeperusha bendera ya ccm mwaka 2015, hahaaa....
 
Sijui EL ana mpango gani na Tanzania hii sio siri sielewi lakin ngoja niendelee kufuatilia huenda nikaja tambua lengo kuu la bwana Lowasa.
 
Lowassa akiwa kwa chairman Hamis Mgeja Shinyanga ni sawa yupo Monduli juu, akina Lembeli wanatafuta blanket kwenye Jua la Utosi, kumkataa Lowassa ni kugomea Matokeo ya Uchaguz Mkuu! Hata kura Zikipigwa na Bavicha peke yao Lowassa lazima aibuke Kidedea!
 
Teh teh, fisadi kaanza safari ya kuelekea magogoni! Ccm na ufisadi ni pete na kidole!
 
Lowassa akiwa kwa chairman Hamis Mgeja Shinyanga ni sawa yupo Monduli juu, akina Lembeli wanatafuta blanket kwenye Jua la Utosi, kumkataa Lowassa ni kugomea Matokeo ya Uchaguz Mkuu! Hata kura Zikipigwa na Bavicha peke yao Lowassa lazima aibuke Kidedea!

mkuu nimekukubali
 
Back
Top Bottom